Tafuta

Vatican News
Majumba ya makumbusha yatafunguliwa kwa upya tarehe 3 Mei Majumba ya makumbusha yatafunguliwa kwa upya tarehe 3 Mei  (� Vatican Media)

Majumba ya Makumbusho Vatican yatafunguliwa Mei 3!

Lazima kutoa ombi kupitia mtandao,kujali muda,kuvaa barakoa na kutunza umbali kati ya mtu na mtu.Mtu yeyote ambaye anatakwenda kinyume na kanuni za usalama wa kiafya anaweza kurudishwa nyuma.Bustani za Vatican pia zitakuwa wazi kwa wageni

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni kasi mpya ya kupeleka mbele lakini kwa tahadhari. Kama ilivyoamuriwa, Jumatatu ya kwanza ya mwezi Mei 2021, ambapo tarehe 3 Makumbusho ya Vatican yatafunguliwa tena mara baada ya kufungwa kwa mara ya  tatu tangu mwaka jana kwa sababu ya Covid-19. Kanuni za maadili ni wazi na mienendo bora  kwa wageni ambayo inatakiwa kuzingatiwa, kwanza kabisa, lazima waombe kupitia njia ya mtandao kwa kubofya kupitia tovuti rasmi ya Majumba ya makumbusho iliyopo hapa chini:

https://www.museivaticani.va/content/museivaticani/it.html

Vigezo vya usalama kuheshimiwa

Baada ya kuomba suala ambalo ni lazima, hatua tatu zifuatazo za kuheshimiwa zitakuwa ni kufika kwa muda unaotakiwa, kuvaa barakoa, na kutunza umbali wa zaidi ya mita moja. Sheria mpya na taratibu za ziara  hija hizo kila wakati zinaripotiwa kwenye tovuti rasmi.

Onyo

Ofisi ya Maelekezo ya Makumbusho ya Vatican, pamoja na kuripoti kwamba Bustani za Vatican pia zitarudi kuwa wazi, na kila wakati kufuata vigezo vya usalama vilivyowekwa, inaonya kwamba inawezekana kuondolewa kutoka ndani ya Makumbusho kwa wale ambao hawatafuata maagizo yaliyoamuliwa na hivyo kuhatarisha afya za wengine.

09 April 2021, 15:15