Tafuta

Vatican News
LAZIMA KUFIKIRIA MADENI YA NCHI MASKINI IKIWA TUNATAKA ULIMWENGU ULIO BORA NA USAWA. LAZIMA KUFIKIRIA MADENI YA NCHI MASKINI IKIWA TUNATAKA ULIMWENGU ULIO BORA NA USAWA. 

Kufuta madeni ya Nchi za Afrika:Ni suala la haki

Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu na Tume ya Vatican kwa ajili ya Covid-19 katika harakati za kuanzisha mipango mbali mbali lakini pia inayoanzia bara la Afrika kwa ajili ya Afrika na kuenea ulimwenguni kote.Ni katika suala la kuhamasisha nchi zinazoendelea kupunguza madeni kwa nchi Maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ili kutoa mwonekano katika mpango ambao unaanzia kutoka chini na kuunda harakati ambayo ikiwa katika nyayo ya ile ya 2000 kwa ajili kufutwa kwa deni, inafika kwa mataifa haya makubwa tajiri (G7 na G20) katika kuzungumzia suala hilo. Ndivyo Katibu Mpya Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Sr Alessandra Smerilli, alivyosisitiza, kwenye Mkutano kwa njia ya Mtandao ulioandaliwa na Tume ya Baraza lenyewe kwa kushirikiana na: Caritas Afrika, Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar (SECAM), Baraza la  Wajesuiti Afrika na Madagascar (JCAM), Chama cha Watawa wa Afrika Mashariki na Kati (ACWECA). Kampeni ya kufutwa kwa deni kwa nchi za Kiafrika, ikiungwa mkono na Braza la Kipapa la Maendeleo fungamani  ya Binadamu na Tume ya Vatican ya COVID-19, inaoneshwa wazi kwa mujibu wa Sr.  Smerilli kuwa ni ya haraka zaidi kutokana na janga hilo.

Ni wakati wa kuangalia, kuhukumu na kutenda kwa jina la maskini na walio katika mazingira magumu zaidi, ameema Askofu Mkuu  Gabriel Justice Yaw Anokye, wa Jimbo Kuu la  Kumasi (Ghana) na Rais wa Caritas Afrika. “Wakati wa shida na mgogoro, tunaweza kuona matendo ya Mungu katika mshikamano. Na kwa upande wa Katibu Mkuu wa SECAM, Padre Henry Akaabiam amesema “Hatuwezi kushindwa kuchukua hatua  kwa sababu ikiwa Afrika inaishi kwa deni, ulimwengu wote utaishi kwa deni. Afrika ikienda vizuri, ulimwengu wote uko vizuri”.

Kwa upande wa Katibu mwingine wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu na mjumbe wa Maelekezo ya Tume ya Vatican kwa ajili ya Covid-19 Padre Augusto Zampini amesema ni kweli kwamba,Papa Mwenyewe mwaka mmoja uliopita alipenda hivyo na wakati tunafikiria jinsi ya kupambana na kuthibiti janga kwa upande wa kiafya, lazima kuzingatia akilini kile ambacho Papa anasema: “Tutatokaje katika mgogoro huu, bora au vibaya? Kwa sababu lazima tukumbuke kuwa mgogoro huu haujatengwa, lakini umeunganishwa na migogoro ile iliyopita, yaani mgogoro kwa sababu ya janga hili haujafanya chochote isipokuwa kuzidisha mizozo iliyopo tayari. Hatuwezi basi kukimbia kutoka katika mgogoro huu, ambao ni afya, uchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni, bila kupunguza mzigo wa deni. Sio suala tu la kiufundi au mshikamano, ambalo pia ni muhimu, lakini pia ni suala la haki. Kuhusu haki ya kizazi, kwa sababu hatuwezi kuwafanya watoto wetu na vizazi vijavyo kulipia athari zote za makosa yetu na haki ya kiroho. Na wala hatuwezi kusahau deni ya kiekolojia la wakuu, yaani wahusika wakuu wa mabadiliko ya tabianchi. Ambapo uzito  hata hivyo, unaangukia mataifa maskini zaidi, kama zile za Kiafrika”.

Deni na umaskini ni binamu, ambao wanatembe njia pamoja kwa bahati mbaya, amesema Sr. Hellen A. Bandiho, STH; ambaye ni Katibu Mkuu wa ACWECA. Sr Hellen amesema: “Fikiria idadi ya shule ambazo zinaweza kujengwa kila mwaka au madawati ambayo yanaweza kununuliwa ili kuruhusu wanafunzi kujifunza vizuri badala ya kukaa chini ya miti. Fikiria idadi ya vituo vya afya ambavyo vinaweza kujengwa au kuboreshwa ili kuwaruhusu wanawake  kutembea kilomita chache kufikia”.

Na kwa mujibu wa Padre Charlie Chilufya, mkurugenzi wa ofisi ya Haki na Ekolojia ya JCAM amesema: “ kwa hakika  ni suala la kimaadili, lakini sio tu: ni mengi zaidi.  Ukweli ni kwamba kuendelea kwa janga katika maeneo ya ulimwengu, kwa sababu ya ukosefu wa njia, kunaweka afya ya kila mtu hatarini”. Leo hii gharama ya kusubiri iliyokusanywa ingetosha kupatia chanjo kwa bara lote dhidi ya Covid. Na bado, amesisitiza , mgogoro huu, ambao ni mkali sana, pia unatoa fursa nyingi za ushirikiano ambao haujawahi kuonekana hapo awali: watu, kama sisi leo, wanakuja pamoja kupata suluhisho ili kukuza maisha katika ulimwengu”..

Dhana, ile ya ulimwengu wote wa hatua ya kufuta deni popote inapohitajika, kwa kuongeza Afrika, Amerika Kusini, Asia na nyingine, pia imesisitizwa na Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu ambaye alizindua rasmi kampeni hiyo na kuhakikisha msaada kutoka Baraza hilo  la  Vatican. Je ni jinsi gani ya kufanya hivyo katika mazoezi? Kuanzia mfano wa kuona, kuhukumu na kutenda kwa dhati ameeleza Kardinali. Aidha kwa kutekeleza vitendo vya utetezi na shinikizo katika pande mbili: katika mazungumzo na taasisi kubwa za kifedha za kimataifa na katika uhusiano na serikali na vikundi katika ngazi mikoa na kitaifa ili kuhakikisha uwazi zaidi wa shughuli. Hii inamaanisha pia kuunda mfumo wa ukaguzi na udhibiti ili rasilimali zilizotolewa kwa faida ya bara ziende mahali ambapo kuna hitaji la kweli la kukuza na kuboresha hali za watu, amesisitiza.

09 April 2021, 15:49