Tafuta

Vatican News
2021.03.31 Kampeni ya Chanjo ya kuzuia covid 2021.03.31 Kampeni ya Chanjo ya kuzuia covid   (Vatican Media)

Kard.Turkson:Lengo la chanjo ya afya iwe kwa wote!

Utegemezi kwa pande zote umeoneshwa na janga la covid-19 na suala la upatikanaji huduma sawa ndiyo kiini cha ujumbe wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya Binadamu,katika tukio la Siku ya Afya Duniani ambayo imeadhimishwa tarehe 7 Aprili:janga limekithiri na kuonesha pengo kati ya Nchi mbali mbali,kwa maana hiyo uoanishaji wa haki ya ulinzi wa afya unahitajika kwa haraka.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Kujenga ulimwengu wenye haki zaidi na wenye afya” ndiyo kauli mbiu iliyochaguliwa kuongoza Siku ya Afya Duniani 2021. Maadhimisho hayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe7 Aprili katika kumbuka kuanzishwa kwa Shirika la fya Ulimwenguni (WHO)manamo 1948,  likiwa na makao yake makuu mjini geneva, Uswisi. Hata hivyo mada iliyopendekezwa na Umoja wa Mataifa  ni ya dharura sana tangu janga la Covid-19 lisimike mguu wake kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa na  limeongeza ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa huduma na huduma za afya na wakati huo huo umeonesha kuwa hakuna mtu aliye salama maadamu sio kila mtu atakayekuwa salama kama hatari zinazohusiana na chanjo , ikiwa zinakuwa duni katika maeneo ya mbali zaidi na maskini zaidi ulimwenguni. Katika fursa hiyo Kardinali Peter K. A. Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya binadamu ametoa ujumbe wake ambao unaangazia hali halisi ya janga hili na huduma hizo.

Kardinali anandika kuwa Suala ambalo linastahili kwa namna ya pekee kupewa umakini ni afya ya akili, ambayo kwa hakika imejaribiwa sana katika kipindi hiki cha janga. Kwa upande huo ameandika kuwa  Baraza la kipapa la Maendeleo Fungamni ya binadamu limefanyia kazi kuhusu Hati moja ambayo inapatikana hata kwenye tovuti yao yenye kichwa “Kusindikiza watu katika mateso ya kisaikolojia katika muktadha wa janga la Covid-19. Wajumbe wa mwili mmoja wapendea wa upendo mmoja”.  Hati hiyo inapendekeza baadhi ya mambo ya tafakari kwa wale walio karibu na watu walioambukizwa na janga na wale ambao wanaalikwa kuwasindikiza katika umbu la familia ambazo ndani mwake kuna miundo ya kiafya.

Kardinali Peter Turkson anaandika kuwa “Ni dharura ya kutunza wale ambao walitutunza. Serikali na wahusika wa sera za kisiasa na kiuchumi, na kiafya ambao ni wahusika wa kuhakikisha hali za kazi bora ya wahudumu wa kiafya”. Hiyo inatakiwa kuwekeza kiuchumi bila kikomo, busara na maadili, ambayo yana sura ya kusindikiza maendeleo ya nguvu za binadamu: na suala linalo fanana na hilo, “ni kuelekeza mafunzo ya wahudumu wa kiafya katika afya fungamani, kama wema wa kila mtu na kwa ujumla. Hii inahitaji uhamasishaji wa kinga, matibabu na ufundishaji elimu ya afya fungamani”.

Kardinali Turkson aidha ameweka bayana kuhusu umakini wa taasisi za kifya kwa namna ya pekee zinazokosa msaada wa kifedha kutoka katika Serikali mbambali duniani na , kama vile ya Makanisa na Jumuiya za kidini ambazo zipo kila kona ya Dunia na mara nyingi mbali sana na miji na zinawakilisha kinga pekee za kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya. Ukosefu wa usawa wa kiafya sio sawa, lakini pia unaweza kuzuilika kwa njia ya mikakati ambayo inakusudia kuhakikisha upatikanaji sawa wa huduma za kiafya, hasa kwa vikundi vilivyo hatarini sana na vilivyotengwa.

Usawa mkubwa katika ulinzi wa afya ulimwenguni unaweza kupatikana ikiwa ni kupitia njia ya kujitoa kwa upya katika  maadili na nchi zilizo na rasilimali kubwa kwa ajili ya nchi zinazohitaji sana. Kardinali Turkson kwa kuhitimisha  anatumaini kuwa “chanjo ya afya kwa wote iweze kuhakikishwa kwa watu wote na jumuiya zote. Ni lengo la haraka la kupatikana ili kujenga ulimwengulio bora na wenye afya,ulimwengu wa amani ambao tunaota na kuamini kuwa bado unawezekana”.

07 April 2021, 17:17