Tafuta

Vatican News
Hawa ni Watakatifu Mapapa:Papa Paulo VI, Yohane XXIII na Yohane Paulo II Hawa ni Watakatifu Mapapa:Papa Paulo VI, Yohane XXIII na Yohane Paulo II 

Kard.Semeraro:Utakatifu unajiinjilisha wenyewe!

Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu ametoa hotuba yake kwenye mkutano kwa njia ya wa video,ulioongozwa na kaulimbiu:“Utakatifu na uinjilishaji wa jamii”.Ni mkutano ulioandaliwa na Chuo Kikuu Katoliki cha Mtakatifu Damas,huko Madrid,Uhispania.Mtu anakuwa mtakatifu hasa unapoingia katika umoja wa kuruhusu neema imwongoze katika ukamilifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Utakatifu unazaliwa kutokana na uinjilishaji na kuzalisha uinjilishaji, kwa sababu unaonesha njia za wokovu. Amesisitiza hayo Kardinali Marcello Semeraro Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza Watakatifu wakati wa tukio la kitaaluma lilifanyika katika siku za hivi karibuni katika Chuo Kikuu Katoliki cha Mtakatifu Damaso huko Madrid Uhispania.  Rais wa Baraza la Kuwatangaza Watakatifu ametoa hotuba hiyo kwenye mkutano kwa njia ya wa video, ulioongozwa na kaulimbiu: “Utakatifu na uinjilishaji wa jamii”. Ili kumfanya mtakatifu, Kardinali Semeraro amekumbusha kuwa, anahitajika mwenye dhambi, lakini mwenye dhambi ambaye anakubali mwaliko wa Yesu katika vidonda vyake, dhambi, na kutokuweza kwake. Kujifunua mbele ya Daktari inakuruhusu kupata mguso ambao huponya. Kwa maana hii mwanadamu hukutana na upendo wa Kristo, na huchagua kuiishi na kuponesha, kwa maana nyingine unaonesha na kuwasha moto wa upendo. Ni wagonjwa tu ambao wanaopona na walioponywa ndio wanajua jinsi ya kutunza wengine.

Kardinali Semerao pia amesma kuwa watakatifu sio mashujaa wakuu, na  wala sio kadi takatifu. Katika maisha ya kidunia walikuwa na kasoro zao, mapungufu na mgogoro, wanaojulikana kama udhaifu wa vyombo vya udongo, mahangaiko ya  Mtakatifu Petro na kutokuelewana kwa mitume ; lakini walijiruhusu kujengwa kwa upya kila siku na habari njema ya Kristo. Ili kuinjilisha jamii, amesisitiza Kardinali, ni muhimu kwamba mgombea wa heshima ya altareni awasilishwe na mchakato wa njia yake ya uponyaji kibinafsi na ukuaji polepole wa imani. Kwa njia hii watakatifu hurudishwa katika hali halisi na wanazungumza na kila mtu. Kwa upande mwingine, Kardinali Semeraro amebainisha kuwa kufanana na Kristo inamaanisha kuchukulia kwa uzito na  upekee wa muungano na mtu. Mtu anakuwa mtakatifu hasa unapoingia katika umoja, wa kuruhusu neema iongoze katika ukamilifu.  Aidha alisisizia kuwa haishangazi, njia za uongofu karibu na uzoefu wetu wa watenda dhambi waliosamehewa zinazidi kudhibitishwa"

Katika suala hili, Kardinali amekumbusha uzoefu wa Mtakatifu  Paulo aliyefikiwa  na neema hiyo ambayo baadaye pia iliangazia Mkatifu  Augustino; na vile vile Mtakatifu Fransisko wa Assisi, aliyetupilia mbali ndoto zake za kuwa mkuu wa majeshi, na Mtakatifu Ignatius wa Loyola, aliyejeruhiwa katika vita vingine. Mchakato huo wa mabadiliko makubwa ya kina ulitokea kwa Mwenyejeri Charles de Foucauld, ambaye alikuwa ameachiliwa huru kutoka jeshi kwa utovu wa nidhamu, lakini akaacha alama yake juu ya maisha ya kidini, na pia Cesare de Bus, Aliyekuwa ni Kuhani wa Kifaransa na mwanzilishi wa Shirika la Makuhani wa Mafundisho ya Kikristo. Alitangazwa kuwa mwenye heri 1975 na Papa Paolo VI. Tarehe 27 Mei 2020, Baraza la Kipapa la kuwatangaza wenye heri lilitambua miujiza kwa ajili ya maombezi na kuruhusu mchakato wa  kuelekea  kutangazwa Mtakatifu. Yeye kama msaidizi asiye na wasiwasi aliongoka akiwa na umri wa miaka 31 na akawa, pamoja na utume wake, mwenezi wa uinjilishaji kupitia vyombo vya habari.

Utakatifu, kwa maana hiyo, huinjilisha wakati tunapowasiliana na mhusika mkuu wa historia hizi, ambayo ni huruma ya Mungu, upendo mkuu zaidi ambao hubadilisha huzuni wote kuwa furaha. Huu ni ujumbe wa watakatifu wengi wa hivi karibuni miongoni mwao  wengine, ni Mwenye Heri ya Kihispania Mama Speranza (2014) na Mtakatifu Faustina Kowalska (2000), au watumishi wa huruma kama vile Mtakatifu Pio wa Pietrelcina (2002) na Mtakatifu Leopoldo Mandić (1983). Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu aidha  hakukosa kusisitiza kwamba ili kuwapa watu wa Mungu  utakatifu na ambao ni mashuda wa kweli na kuepuka kuchanganyikiwa au udanganyifu, taratibu muhimu na ukaguzi zinahitajika. Leo hii, alithibitisha, ni rahisi kueneza habari a bandia, (fake news) na kujenga utakatifu wa uwongo kupitia mitandao ya kijamii. Hasa katika hitaji la kutambua mifano ya kuaminika ya maisha ya Kikristo ilipelekea, mnamo 1588, kuanzishwa kwa Baraza la Ibada la wakati huo ambalo mnamo 1969 liligawanywa na kuwekwa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza  wenyeheri na Watakatifu. Tayari tangu karne za kwanza, hata hivyo, Kanisa lilikuwa limehisi jukumu kubwa la kuthibitisha watu wake “vox populi”.

Ili kutambua utakatifu halisi, kwa haraka waliunganisha hata sifa kutoka kwa watu, ambayo ilihusishwa kwanza na idhini ya kiaskofu na makasisi na katika karne ya sita ilianzishwa kutangazwa kwa maaskofu. Kitendo hiki kiliaachwa kwa uamuzi wa Papa, kwa maana hiyo waliacha  mchakato wa uwasilishaji wa kidini upitishwe,na  ambao uliona ushiriki wa wataalam, hadi maagizo ya mchakato halisi wa kisheria. Inaweza kushangaza lakini hata leo hii, Kardinali Semeraro amekumbusha kuwa kila kitu kinatokana na vox populi, yani  kutokana kwa watu ile  sifa ya utakatifu wa hiari na ambayo imeenea. Na ni maoni ya kawaida kwamba mhusika wa mwisho wa umaarufu huo anaweza kuwa Mungu mwenyewe, ambaye anaelekeza kwa wanadamu Wakristo kwa mfano katika upendo.

16 April 2021, 15:33