Tafuta

Vatican News
2021.04.05  Mahojiani ya Radio Cope kwa Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican. 2021.04.05 Mahojiani ya Radio Cope kwa Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican. 

Kard.Parolin:Kanisa liungane kushuhudia Injili kiaminifu ulimwenguni

Kati Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican akihojiwa katika Radio ya COPE amekabiliana na mada nyingi zikiwemo wito wake wa kikuhani hadi uhusiano wake na Papa;kuanzia vipingamizi vya sasa katika jumuiya ya kanisa,hali halisi ya Kanisa nchini China,na ushuhuda wa ziara ya Papa nchini Iraq.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mahojiano aliyoacha Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican kwa José Luis Restán, Mkurugenzi wa Mtandao wa uhariri wa Radio ya Kispanyola  iitwayo COPE, katika fursa ya Siku kuu ya Pasaka amesema kuwa: “tupo katika huduma ya muungano hata na ulimwengu, ya uhamasishaji wa uhuru wa Kanisa, na wa uhuru wa kidini. Na zaidi pia shughuli ya amani ulimwenguni. Fikirieni kwa maana hiyo ni jinsi gani Kanisa lina jukumu kwa ajili ya amani. Hii ndio namna yangu ya kuona shughuli ya kidiplomasia”. Katika mahojiano hayo mada zilizokabiliana wito wake Katibu wa Vatican na huduma yake akiwa karibu na Papa, mageuzi ya Vatican, migogoro ndani ya Kanisa, hali halisi ya Kanisa la China, ziara ya kitume ya Iraq na utume wa Kanisa barani Ulaya.

Wito na huduma ya Kidiplomasia

Akiwa na uwezo mkuu wa kujua hali halisi ya Kanisa katika mabara matano, Kardinali Parolin amezungumzia kuhusu wito wake na jinsi ambavyo  kwa miaka 40 iliyopita ameweza kuwa  katika huduma ya Kipapa, bila hata kujua ni kwa jinsi gani. “Ninaamini kuwa wito wangu msingi ni ule wa kuwa kuhani. Ninahisi kuitwa, ninahitaji bado kuitwa kuwa kuhani, mtumishi wa Bwana ambaye anafanya kazi katika Kanisa kwa ajili ya roho, huku nikikumbuka jinsi ambavyo sisi sote tuko tofauti katika hutoaji wa huduma kwa ajili ya roho. Na kama mwanadiplomasia wa Kikanisa hayo yote yanaingiliana moja kwa moja. “sikuwahi kuwa na kipingamizi kati ya kuwa kuhani na kuwa mwanadipolasia kwa sababu hasa baada ya Mtaguso II wa Vatican, inaeleaza kuwa shughuli ya Mabalozi ni ya kichungaji, shughuli ambayo inajitahidi kudumisha uhusiano kati ya Vatican na makanisa mahalia, ameeleza Kardinali.

Mageuzi ya Vatican

Shughuli yake kama Katibu wa Vatican, ameongeza kusema, itaendelea hata ikiwa kuna mabadikio ya Vatican ambayo Papa yuko anaandaa yatakapokuwa yamemalizika. Katiba mpya ya Kitume itabadilisha ile ya sasa iliyopo kisheria kwa kuendelea kuhifadhi bila shaka neno la Praedicate Evangelium yaani Hubirini Injili. Katibu wa Vatican ataendelea kuratibu Ukatibu wa Vatican, kiungo ambacho kinasaidia kwa karibu sana Baba Mtakatifu kuliongoza Kanisa, katika vitengo vyake vitatu: kwa ajili ya mambo ya ndani kwa ujumla, kwa ajili ya uhusiano na ushirikiano na mataifa  na Watu binafsi wa Kidipolasia. Na kwa maana hiyo Katibu ataendelea kutaritbu vitengo hivyo vitatu na kufanya kazi hasa akifikiria kwa ajili ya diplomasia ya Kikanisa.

Ushirikiano na Papa Francisko

Ushuhuda maalum wa Kipapa na Papa Francisko Kardinali amekumbusha mshangao wake wakati akiwa Balozi wa Kitume nchini Venezuela, ambapo Baba Mtakatifu Miaka 8 iliyopita, baada ya miezi miwili tangu achaguliwe kuwa Papa alimetua kuwa Katibu wa Vatican. Na amesimulia jinsi ambayo tofauti zao za kitabia zimewakilisha faida kwa ajili ya huduma ya Kanisa. “Hii ni kutokana na kamba kubadilisha tofauti zetu kuwa utajiri kwa ajili ya ulimwengu kama vile asemavyo mara kadhaa Papa. Tabia zisiwe kizingiti bali ushirikiano na kila mmoja kwa mtazamo wake, na mtindo wake, hisia zake, majiundo yake, utamaduni wake, tasaufi yake, vyote vikiwa katika  kushirikiana na mwingine”.

Kufanya Kanis liaminike katika kutangaza Injili

Akizungumiza juu ya sura ya Papa, Kardinali Parolin ameongelea kile ambacho kinamshangaza juu yake hasa urahisi mkubwa alio nao. “Anapomkaribia, ndipo unatambua roho yake iliyo rahisi bila kuwa na  protokali, mtu ambaye anajua kutunza sana uhusiano na ukaribu na wengine ambao wanatafuta kukutana na mtu huyo na  ndiyo tabia yake ya kufanya kazi na ambayo shauku ni ile ya kufanya Kanisa liweze kuaminika zaidi katika kutangaza Injili.

Wasiwasi wa mizozo katika Kanisa

Kuhusiana na suala la mizozo katika jumuiya ya kikanisa la kinachojulikana kama mrengo wa kuhifadhi na kile kinachoitwa mrengo wa kimaendeleo, Kardinali amesisitiza jinsi hali hii inavyosababisha uharibifu kwa Kanisa, baada ya Kristo kuombea umoja wake. “Kuna sababu ya wasiwasi amesema, akionesha jinsi tatizo labda linatokana na ukweli kwamba Papa anaweka mkazo sana juu ya mageuzi ya Kanisa na kuna mkanganyiko mwingi juu ya hili”. Muundo wa Kanisa, amana ya imani, sakramenti, huduma ya kitume haiwezi kubadilishwa, lakini kuna “maisha yote ya Kanisa ambayo yanaweza kupyaishwa”, maisha ambayo watu wenye dhambi hufanya kazi na ambayo kwa hivyo inahitaji kuendelea kufanywa kwa upya”. Wakati mwingine ameeleza ​​mgawanyiko huu na upinzani huu unatokana na mkanganyiko, kutokana na kutoweza kutofautisha kati ya yale ambayo ni muhimu na ambayo hayawezi kubadilika na yale ambayo sio muhimu na lazima yarekebishwe, na lazima yabadilike kulingana na roho ya Injili”.

Tumaini ya siku zijazo ya Kanisa nchini China

Akikabiliana kuzungumzia ukweli wa Kanisa nchini China, Kardinali Parolin amesisitiza jinsi Vatican inavyoiangalia kwa heshima kubwa, kwa historia yake ya mateso makubwa, lakini pia kwa matumaini makubwa. Hatua zilizochukuliwa hadi sasa, hata ikiwa hawajasuluhisha shida zote ambazo bado zipo na ambazo labda zitachukua muda mrefu amesema  ziko katika mwelekeo sahihi kuelekea maridhiano ya ndani ya Kanisa”. Kile ambacho wamejaribu au wanaendelea kufanya amebainisha Kardinali ni kulinda jumuiya hii ambayo bado ni ndogo lakini ambayo ina nguvu kubwa na uhai. Yote ambayo hufanywa ni kuhakikisha maisha ya kawaida katika Kanisa nchini China ili kuhakikisha nafasi za uhuru wa kidini, wa ushirika kwa sababu mtu hawezi kuishi katika Kanisa Katoliki bila ushirikiano na mfuasi wa Petro, yaani na Papa”.

Ushuhuda mkubwa wa Wakristo wa Iraq

Akikumbuka ziara ya kitume nchini Iraq na kukutana na Kanisa linaloteswa, ambalo linaendelea kuteseka na kuishi katika hali ya kutokuaminiana na kutokuwa na uhakika ambayo hairuhusu Wakristo kuona siku zijazo katika nchi, Kardinali Parolin amezungumzia mafundisho makuu aliyojifunza kutoka katika mkutano huo na waamini wa Iraq. “Walichotufundisha ni ushuhuda wa imani ambao unafikia hatua ya kuuawa. Hili ndilo somo kubwa tunaloweza kupata kutoka kwa Wakristo wa Iraq”. Licha ya mashambulio na vifo, Wakristo wanaendelea kukiri imani yao Katoliki kwa ujasiri mkubwa. “Haya ni mafundisho mazuri na kuongeza kuwa ni wito wa mshikamano. “Wanatufundisha uwezo huu wa kuwa waaminifu licha ya shida lakini wakati huo huo wanatuomba mshikamano zaidi”.

Kupoteza imani Ulaya

Akizungumzia bara la Ulaya na kuibuka kwa sheria mpya juu ya masuala ya kimaadili ambayo yanakwenda mbali zaidi na mizizi ya Kikristo, Kardinali Parolin amekiri kuhisi sana kupotea kwa imani katika haya mabadiliko ya elimu ya binadamu  inayofanyika, huku akisisitiza kwamba “ kupoteza utambulisho wa mwanadamu, zaidi ya kupoteza imani inawakilisha kupoteza sababu. Kama vile Papa Francisko alivyosema mara nyingi, kwa mfano, suala  la utoaji mimba sio suala la kidini, lakini ni  suala la sababu. Na labda leo, hii  kama Papa Mstaafu Benedikto  XVI alivyosema, tatizo  msingi ni sababu, na sio imani”. Kardinali kwa maana hiyo  ameonesha jinsi utume wa Kanisa Ulaya ni ule wa ushuhuda. “Lazima tushuhudie imani yetu, lazima tushuhudie tumaini letu, lazima tushuhudie upendo wetu”, bila kulazimishwa, lakini kwa kutoa tu “ushuhuda thabiti na wenye kusadikika wa maisha ya Kikristo, kama ilivyotokea katika karne za mwanzo wa Kanisa, wakati mitume na wanafunzi walipofika katika jamii isiyo na maadili ya Kikristo na kupitisha ushuhuda wao waliweza kubadilisha fikira na kuanzisha maadili ya Injili katika jamii ya wakati huo”.

Haja ya kuwa na sala

Leo hii zaidi ya wakati wowote, Kardinali Parolin amehitimisha, kuwa tunahitaji maombi, ili kutuunganisha sisi sote katika maombi, na ili Bwana atusaidie kuwa waaminifu  kwa utume wa kushuhudia Injili na pia kuwa mali yetu Kanisa katika ulimwengu wa leo hii”

05 April 2021, 16:20