Tafuta

2019.08.26 Salam za Al Maktoum na Kardinali Guixot 2019.08.26 Salam za Al Maktoum na Kardinali Guixot 

Kard.Guixot:Mazungumzo kati ya dini zote kwa ajili ya haki inawezekana

Papa kwa hakika anaamini kuwa neema ya dhati ya kushirikiana kati ya waamini,inaweza kutimizwa kwa kufanya kazi ili wema kwa wote uwezekane,huku akichanganua ukosefu mwingi wa haki ambao bado unasumbua ulimwengu huu na kulaani kila vurugu.Kwa hakika mwamini ni shuhuda na mbebaji wa maadili,ambayo yanaweza kuchangia sana kujenga jamii zenye haki na afya.AmethibitishaRais wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mazungumzo ya kidini ni hali ya lazima kwa ajili ya kuishi kwa amani. Kwa maana hiyo mbali na matatizo na tofauti, hakuna kuacha kushirikisha na wale ambao wanafikiria tofauti. Amesisitiza hayo hivi karibuni, Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, wakati akizungumza kwenye hotuba yake, katika mada ya “Udugu, mazungumzo ya kidini na haki kijamii, kwa kuangaziwa  na Waraka wa kijamii wa Papa Francisko wa “Fatelli tutti yaani “ wote ni ndugu”. Kwa namna ya pekee katika sura ya 8 ambayo inakwenda sambamba na mchango wa udugu wa ulimwengu ambao viongozi wa tamaduni za dini mbali mbali na jumuiya zinazoongozwa ambazo zinaweza kweli kutoa mchango mkubwa katika jamii na ambazo wanaishi na kutembea kwa pamoja.

Kardinali kwa maana hiyo hivi karibuni aliweza kuzindua tena na kuzungumzia juu ya Hati ya Abu Dhabi iliyotiwa saini mnamo tarehe 4 Februari 2019 na Papa Francisko pamoja na Imam Mkuu wa Al-Azhar,  na kuzungumzia juu ya mazungumzo ambayo kwa waamini yanageuka kuwa sala, ambayo amesema tunaweza kuitimiza kiukweli kila siku kwa jina la Udugu na ambao unakumbatia watu wote, kuwaunganisha na kuwafanya wote kufanana. Rais wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini ameeleza kuwa Baba Mtakatifu anakumbusha kwamba sisi sote tunaitwa kutimiza kile ambacho leo hii na kila mahali ni cha lazima, kwa ajili ya ulimwengu wetu, au kwa kusema kuwa sanaa ya kujua kuzungumza, kwa wote bila upendeleo, na ambao unageuka kuwa jitihada hadi kuwa njia ili kujifungulia mahitaji ya ulimwengu na kujenga urafikia kijamii.

Hii ameiweka wazi hasa kwa kuheshimu na kutafuta ukweli, kwa kufanya kuzaliwa utamaduni wa kukutana, kubadilishana katika njia mpya ya maisha, matamanio makuu na shauku na ili kwamba anayezungumza awe mkarimu, anayetambua hadhi ya mwingine na kumhesimu. Kwa kuongezea, Kardinali amesema Papa kwa hakika anaamini kuwa neema ya dhati ya kushirikiana kati ya waamini, kunaweza kutumizwa kwa kufanya kazi ili kufanya wema kwa wote, huku akichanganua ukosefu mwingi wa haki ambao bado unasumbua ulimwengu huu na kulaani kila vurugu. Kwa hakika mwamini ni shuhuda na mbebaji wa maadili, ambayo yanaweza kuchangia sana kujenga jamii zenye haki na afya. Haki, uaminifu, upendo kwa faida ya wote, umakini kwa wengine, hasa kwa wale wanaohitaji, ukarimu na huruma ni mambo ambayo tunaweza kushiriki na dini mbalimbali. Kufuatana na hili ndipo ametoa ushauri wa kutoa ushirikiano wetu kwa jamii ambazo sisi zote kama wamini ni raia na kutoa maadili yetu yote ya kawaida na imani zetu za kina ili kutetea na kukuza amani na haki, utu wa binadamu na utunzaji wa mazingira.

Katika muktadha huo mazungumzo ya kidini , Kardinali anathibitisha kuwa yana jukumu muhimu katika kujenga jamii inayojumuisha na isiyojengwa juu ya utamaduni wa kutupa, na ni hali ya lazima kwa amani ya ulimwengu. Katika ulimwengu usio na ubinadamu, ambao unatawaliwa na kutokujali na uchoyo huonesha uhusiano kati ya wanadamu, kuwa  kuna haja ya mshikamano mpya na wa ulimwengu wote. Kwa njia hiyo Kardinali Ayuso Guixot amesema jamii ya kidugu ndiyo itakayo hamasisha elimu katika mazungumzo ili kushinda virusi vya ubinafsi huku ikiruhusu kila mtu atoe ubora wake. Nyenzo mbili hasa zilizotambuliwa ni ukarimu, ambao ni kwa kweli wa kutaka uzuri wa mwingine na kujali wadhaifu kupitia watu kwa njia ya huduma bila kuwa na itikadi, kupambana na umaskini na ukosefu wa usawa. Kuanzia na dhana hiyo kwamba Mungu ndiye Muumba wa kila kitu na kila mtu, kwa maana sisi sote  ni washiriki wa familia moja na lazima tujitambue vile vile, Kardinali amesisitiza hitaji la kupitia kutoka kile kitwacho  uvumilivu  na kufikia kuishi pamoja kama ndugu, kutafsiri tofauti ambazo zipo kati yetu, ili kutuliza ghasia na kuishi kama kaka na dada.

Kwa mana hii pia ushirikiano wa kidini lazima na unaweza kuunga mkono haki za kila mwanadamu, katika kila sehemu ya ulimwengu na kila wakati. Kama wanachama wa familia moja ya wanadamu amesema Kardinali kuwa,  tuna haki sawa na wajibu kama raia wa ulimwengu huu. Kwa msingi wa ushirikiano wetu na mazungumzo yetu ndio mizizi ya kawaida ya ubinadamu wetu na kwa maana hiyo mazungumzo haanzia na chochote kwani tayari kuna hali yetu ya kibinadamu ambayo tunashiriki, na mambo yake yote ya kiuhai na ya vitendo, ambayo ni nzuri ya  uwanja wa mkutano. Kardinali amesisitiza kuwa ni kuhakikisha kuwa dini zinaweza kuwa njia za udugu badala ya kugawanya na kuleta vizuizi, pia  ni muhimu kupitisha utamaduni wa mazungumzo kama njia ya ushirikiano, kama njia ya maarifa ya pamoja na kama kigezo cha kawaida cha pamoja. Vile vile akimaanisha umuhimu mkubwa wa janga la covid-19,  amesema kuna uharaka ulioamriwa na hali ya ulimwengu wa sasa ambao lazima tuweke kando ubaguzi, ucheleweshaji na shida. Ingawa sio kukataa utambulisho wa mtu mwenyewe kwa chochote au akimaanisha umoja rahisi, kwa nguvu na ujasiri, hitaji la ushirikiano wa kibinadamu na urafiki wa kijamii lazima lithibitishwe kama hali msingi za kupata uponyaji na amani ambayo ulimwengu wote unatamani.

Kwa kifupi, Kardinali Guixot amebainisha kwamba uhusiano kati ya mazungumzo ya kidini, undugu wa wanadamu na matarajio ya amani haviepukiki na imekuwa karibu sana hivi kwamba hatuwezi hata kufikiria ukweli huu kutengana; ile ya dini zinazokutana, kuzungumza kwa kila mmoja, kujuana, kutambuana katika safari ya undugu, kila mmoja wao kama mjenzi wa amani popote anapojikuta akifanya kazi, na ile ya amani ambayo inahitaji zaidi kuliko katika zamani kuliko Kanisa Katoliki na dini nyingine ambazo zinafanya  a kazi pamojaili  kuzuia, na kuondoa, yote ambayo yanaweza kusababisha mgawanyiko na migogoro ”. Kwa kuzingatia tafakari hizi, tunaelewa ni kwanini Baba Mtakatifu Francisko, ametaka Kanisa litoke nje  na liwe  rafiki wa maskini zaidi, katika mazungumzo na kila mtu na ambaye kwa mwanga wa Injili anamkumbusha kila mtu juu ya kiini cha mwanadamu na asili yake hadhi. Anatafuta ushirikiano na marafiki hasa kati ya wale ambao wanaweza kupata urithi wa utajiri wa kiroho na hekima ya milenia ya watu wa tamaduni nyingine za kidini.

Ni  matumaini ya rais wa Baraza la Kipapa la Mazunguzo ya kidini kwamba inawezakana kujitoa kwa wote ili mada za Udugu na urafiki wa kijamii ziwe eneo la mapambano kati ya washiriki wa tamaduni tofauti za kidini na  ziwe kwa ngazi ya juu hadi kufikia ngazi ya chini. Mfano kwa maana hiyo ni maadhimisho kwa mara ya kwanza ya tarehe 4 Februari iliyopita, ya miaka miwili baada ya kutiwa saini  Hati kwa jina moja, Siku ya kwanza ya Udugu wa Binadamu, iliyotangazwa tarehe 21 Desemba 2020 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakati wa Mkutano wa kikao cha 75. Hii kwa hakika inafaa sana amesisitiza Kardinali   kwamba ujumbe wa udugu umepata mwangwi na kukubalika na jamii ya kimataifa na wale wote wanaosimamia katika maeneo mbali mbali  ya maisha ya kijamii na kiraia. Katika hafla hiyo, ambayo ilifanyika katika hali halisi yaani kwa njia ya mtando kwa sababu ya Virusi vya corona, Papa Francisko alisema: “Leo hakuna wakati wa kutokujali. Hatuwezi kunawa mikono yetu kwa njia hiyo, kuwa  na umbali, na uzembe, bila kujali. Ama sisi ni ndugu au haupo”.

18 April 2021, 16:24