Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemtea Mheshimiwa Padre David Ajang kuwa Askofu  mpya wa Jimbo Katoliki la Lafia nchini Nigeria. Baba Mtakatifu Francisko amemtea Mheshimiwa Padre David Ajang kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Lafia nchini Nigeria.  (Vatican Media)

Askofu David Ajang, Jimbo Katoliki la Lafia, Nigeria

Askofu mteule David Ajang alizaliwa tarehe 31 Machi 1970 huko. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 3 Desemba 1994 akapadrishwa na kuwa ni Padre wa Jimbo kuu la Jos. Baada ya kupewa Daraja Takatifu ya Upadre amewahi kuwa Paroko-usu, Paroko, Mkurugenzi wa Miito, Mkurugenzi wa Utume wa Vijana na Msimamizi wa Kanisa kuu la “Our Lady of Fatima.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre David Ajang kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Lafia, nchini Nigeria. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule David Ajang alikuwa ni Paroko wa Parokia ya “Immaculate Conception na Dekano wa Dekania ya Zaramaganda, Jimbo Katoliki la Lafia. Askofu mteule David Ajang alizaliwa tarehe 31 Machi 1970 huko Zaria. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 3 Desemba 1994 akapadrishwa na kuwa ni Padre wa Jimbo kuu la Jos, nchini Nigeria.

Baada ya kupewa Daraja Takatifu ya Upadre amewahi kuwa Paroko-usu, Paroko, Mkurugenzi wa Miito, Mkurugenzi wa Utume wa Vijana na Msimamizi wa Kanisa kuu la “Our Lady of Fatima. Baadaye akateuliwa kuwa ni mlezi Seminari kuu ya Mtakatifu Augustine Jimbo kuu la Jos kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2012. Tangu mwaka 2012 hadi mwaka 2015 alikuwa ni kati ya wajumbe washauri wa Jimbo kuu la Jos, Nigeria. Kuanzia mwaka 2018 hadi kuteuliwa kwake amekuwa ni ni Paroko wa Parokia ya “Immaculate Conception na Dekano wa Dekania ya Zaramaganda, Jimbo Katoliki la Lafia.

Nigeria
01 April 2021, 16:17