Tafuta

MAANDALIZI YA KUSUBIRI PAPA NCHINI IRAQ. MAANDALIZI YA KUSUBIRI PAPA NCHINI IRAQ. 

Kard.Filoni:Ziara ya Papa nchini Iraq ni muafaka

Katika mahojiano na Kardinali Fernando Filoni,Mkuu wa Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu Yerusalemu kuhusiana na ziara ya Papa Francisko nchini Iraq,amesema ni wakati halisi.Covid iko kila mahali.Matatizo ya usalama pia. hakuna wakati ambao haufai ili kuweza kwenda nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Hakuna wakati wa amani, wakati unaofaa kwa ajili ya kwenda. Ni wakati halisi. Covid iko kila mahali. Matatizo ya usalama pia. Ninakumbuka hata wakati Baba Mtakatifu anataka kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati, watu wengi walisema hasienda. Na mwisho Baba Mtakatifu aliamua kuwa upade wa watu wa Mungu kwenda katika ziara yake ya kichungaji na hivyo kwa sasa ni wakati unaofaa. Amesema hayo Kardinali Fernando Filoni, Mkuu wa Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu Yerusalemu wakati anahojiana na Shirika Katoliki la habari na matangazo EWTN kuhusiana na ziara ya Kitume ya papa Francisko inayotarajiwa kufanyika tarehe 5 hadi 8 Februari 2021.

Akigusia juu ya mada ya wakristo wanaoteseka, Kardinali amesema ni wazi kwa sababu anaamini kwa upo uwezekano wa kushirikishana na wengine hisia, mazungumzo, heshima na haki. Swali ni kwamba ni wapi ninatakiwa nisaidie au ni vumilie. Ninapaswa kutoa haki wapi. Ikiwa ni kuheshimu, ninayo mazungumzo ndani mwangu hayo? Aidha Kardinali amesema, swali la kujiuliza ni  ikiwa wewe ni kuhani, wewe ni mchungaji, inawezekana kweli kuacha watu wako ambao wanaishi bado huko, wanafanya kazi na ambao wanateseka huko?. Kwa kawaida watu wenyewe wana msemo wao “Inshallah”, yaani ikiwa hayo ni mapenzi ya Mungu… Mungu atawalinda. Hakuna ambaye aliwahi kufikiria kuwa wameadhibiwa na Mungu, Mungu yuko wapi na kwa sababu gani. Hayo ni matokeo ya matendo ya binadamu na hayawezi kutokana na Mungu.

Kardinali Filoni aidha akijibu juu ya ujenzi wa amani, anasema anao uhakika na kufikiria kwamba inajengwa tararibu. Lakini kuna ulazima kwamba serikali zile ndogo, dini ndogo, raia na wote kwa namna moja waweze kuelewana kwanza. Si rahisi kupatikana  amani kwa sababu mmoja analazimisha, bali ni kuijenga kwa pamoja. Kardinali anao uhakika kwamba amani imo katika harakati, japokuwa bado kuna jambo la kufanya.

Na yote hayo yanategemea moja kwa moja na wao lakini nje yake  hata kwa upande wake, lazima kuwasidia kupata hali hiyo ya amani, amethibitisha. Kardinali Filoni amezungumzia juu ya Iraq kwa sababu anao uzoefu wa nchi hiyo kwani aliwahi kuwa Balozi wa kitume  wa Vatican nchini humo kuanzia 2001 hadi 2006 mahali ambao aliweza kushirikiana katika kukabiliana na vita akiwa na watu hao. Kabla ya kuchaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu Yerusalemu, alikuwa ni Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu.

01 March 2021, 17:27