Tafuta

Vatican News
Bado kampeni ya chanjo dhidi ya virusi vya Covid -19 inaendelea katika mataifa mbali mbali. Bado kampeni ya chanjo dhidi ya virusi vya Covid -19 inaendelea katika mataifa mbali mbali.  (ANSA)

Sadaka ya kitume:Kufikia Pasaka maskini 1200 watapata chanjo!

Ukaribu kwa walio wadhaifu zaidi ndiyo maelekeo ulioombwa na Papa Francisko na ambao unakuwa halisi kwa mara nyingine tena katika Wiki Kuu ya Pasaka,kwa kuchangia utoaji wa dozi za chanjo zilizonunuliwa na Serikali ya Vatican kwa ajili ya Hospitali ya Spallanzani jijini Roma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Watu 1200 ambao ni maskini zaidi na walioachwa kwa maana hiyo walio na hali halisi ya pembeni ambao ni rahisi kupata virusi vya Corona, watapatiwa chanjo wakati wa Wiki Kuu Takatifu, kufuatia na mpango wa Sadaka ya Kitume, na shukrani kwa dozi za chanjo ya Pfizer-Biontech iliyonunuliwa na Makao Makuu Vatican na kutolewa zawadi kwa Hospitali ya Lazzaro Spallanzani ya Roma, Italia.

Hakuna hata mmoja ambaye abaguliwe

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa kutoka Ofisi ya Sadaka ya Kitume, inabanisha kuwa msaada huo utawafikia watu kwa sababu ya kutimiza miito mbali mbali ya Papa Francisko ambayo inasisitiza kuwa hasisauliwe hata mmoja katika kampeni ya chanjo ya kuzuia virusi vya corona au Covid-19”. Kusimamia dozi za chanjo, ambazo zitasambazwa kupitia Ukumbi wa Paulo VI, Vatican ni madaktari, wafanyakazi wa afya na watu wa kajitolea kutoka kliniki ya "Madre di Misericordia" yaani Mama wa Huruma, iliyoko chini ya nguzo Bernini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican ambao tayari wametoa msaada kwa zaidi ya watu 1200 waliotengwa, na ambao ni watu kutoka mataifa 96, pia kwa sampuli na vipimo.

Unga mkono na kushiriki katika kutoa upendo kwa ajili ya ndugu 

Kwa kuongezea, kushiriki muujiza wa hisani kwa ndugu walio katika mazingira magumu zaidi na kuwapa fursa ya kupata haki hiyo, inawezekana kutoa mchango kupitia mtandaaoni kwenda katika mfuko wa matendo ya kitume wa Baba Mtakatifu Francisko unaosimamiwa na na Mfuko wa Kitume kupitia Tovuti: www.elemosineria.va. Kwa hakika ni aina ya chanjo ambayo inataka kusisitizia kama alivyokumbusha mara nyingi Papa kuwa lazima kila mtu apate chanjo hiyo, na hasiwepo yoyote anayetengwa kwa sababu ya umaskini.

Tangu Januari maskini wanaioshi pembeni mwa Vatican wamepatiwa chanjo

Tayari Januari iliyopita, wakati wa kampeni ya chanjo ilipoanza Vatican, watu 25 wasio na makazi wanaoishi karibu na Uwanja wa Mtakatifu Petro walikuwa wamepewa chanjo na wanasaidiwa na kukaribishwa na vituo vya kutoa misaada katika eneo hilo. Wanaume na wanawake zaidi ya 60, wenye shida kubwa za mwili na shida katika kupata vituo vya afya vya kitaifa. Msaada huu umeongezwa na jitihada kubwa ambapo tangu mwanzo wa dharura ya kiafya, Papa daima amejitokeza waziwazi, akitoa misaada ya dhati kama vile, mashine za kupumulia kwa ajili ya hospitali nchini Italia na ulimwenguni kote na hata kwa kuchukuliwa sampuli na vipimo kwa watu wengi wanaoishi pembezoni mwa jamii.

Zoezi katika uwajibikaji

Kuapata chanjo kwa mujibu wa Papa Francisko ni njia ya kutekeleza jukumu kwa jirani na ustawi wa pamoja. Kwa sababu hiyo, Papa aliomba wakati wa siku kuu ya Noeli 2020 kwa wakuu wa Mataifa, kampuni makubwa, mashirika ya kimataifa, na binafsi kuhamasisha ushirikiano na sio mashindano, na kutafuta suluhisho kwa ajili ya wote. Papa alisema “Tunakabiliwa na changamoto ambayo haijui mipaka, vizuizi haviwezi kuwekwa, kwa maana sisi sote tuko kwenye mtumbwi mmoja".

27 March 2021, 14:51