Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu unatafsiri vipi tetemeko ambao mnamo 2020 umekumba ulimwengu mzima katika mtindo wa virusi vya corona? Baba Mtakatifu unatafsiri vipi tetemeko ambao mnamo 2020 umekumba ulimwengu mzima katika mtindo wa virusi vya corona? 

Papa:Hatuwezi kuendelea kutengeneza silaha badala ya kuokoa maisha!

Jumanne 16 Machi 2021 katika duka la Vitabu la Vatican(LEV),toleo jipya la kitabu linatolewa lenye kichwa:"Mungu na ulimwengu utakaokuja".Ni kitabu cha mahojiano ya Papa Francisko katika mazungumza na mtaalam wa habari za Vatican,Domenico Agazzo.Zifuatazo ni dondoo za maswali na majibu yake.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Kuna wakati wa giza maishani. Mara nyingi tunafikiri kwamba hayawezi kutokea kwetu, lakini kwa mtu mwingine tu, katika nchi nyingine, labda kutoka bara la mbali. Hayo ni maneno kutoka katika mahojiana ya Papa Francisko katika mazungumzo na mtaalam wa masuala ya Vatican, Domenico Agazzo ambapo, tarehe 16 Machi kitabu kipya kitatolewa katika Duka la Vitabu Vatican (Lev. Na yafuatayo ni mahojiano hayo:

Baba Mtakatifu unatafsiri vipi tetemeko ambalo mnamo 2020 umekumba ulimwengu mzima katika mtindo wa virusi vya corona?

Badala yake, sisi sote tuliishia kwenye handaki ya janga. Maumivu na vivuli vimevunja milango ya nyumba zetu, vimevamia mawazo yetu, vimeshambulia ndoto na mipango yetu. Na kwa hivyo hakuna mtu leo hii anayeweza kumudu kujisikia vizuri. Ulimwengu hautakuwa sawa tena kama mwanzo. Lakini ni hasa ndani ya mkasa huu kwamba inawezekana kuthibitisha ishara ambazo zinaweza kuwa msingi wa ujenzi wa lazima uonekane. Hatua hazitoshi kutatua dharura. Janga hili ni ishara ya kengele ya hatari ambayo mtu analazimika kutafakari. Wakati huu wa jaribio unaweza kuwa wakati wa uchaguzi wenye busara na wenye kuona mbali kwa ajili ya faida ya ubinadamu. Ya ubinadamu wote”

Je ni dharura zipi zinatazamiwa?

“Hatuwezi tena kukubali ukosefu wa usawa usio na maana na usumbufu katika mazingira. Njia ya wokovu wa ubinadamu hupitia kutafakari kwa upya mtindo mpya wa maendeleo, ambao unaweka ujumuishaji usiopingika kati ya watu kulingana na maelewano na uumbaji. Kwa kutambua kuwa kila hatua ya mtu binafsi haibaki imetengwa, kwa ubora au katika ubaya, lakini ina matokeo kwa wengine, kwa sababu kila kitu kimeunganishwa.  Kila kitu! Wote! Kwa kubadilisha mitindo wa maisha yanayolazimisha mamilioni ya watu, hasa watoto, kushikwa na njaa, tutaweza kuishi maisha mazito zaidi ambayo yangeweza kufanya mgawanyo mzuri wa rasilimali iwezekanavyo. Haimaanishi kupunguza haki kwa wengine katika  usawa wa chini, badala yake ni kutoa haki kubwa na pana kwa wale ambao hawatambuliki na kulindwa”.

Je! Unaona ishara zozote zenye kutia moyo?

Leo hii tayari harakati mbambali  za watu zinajaribu kuhamasisha shughuli hizo kuanzia chini lakini pia taasisi na vyama Wanajaribu kutambua njia mpya ya kuangalia nyumba yetu ya pamoja: sio tena kama ghala la rasilimali inayotumiwa, badala yake kuiona kama bustani takatifu ya kupendwa na kuheshimiwa, kupitia tabia endelevu. Na baadaye, kuna mwamko kati ya vijana, hasa katika harakati za kiekolojia. Ikiwa hatujifungi kibwewe na kuanza kushughulika kutunza dunia yetu mara moja kwa kuwa na chaguo muhimu binafsi  na serza kisiasa thabiti, na mwelekeo wa kiuchumi kuelekea ukijani na kuelekeza maendeleo ya kiteknolojia katika mwelekeo huo, mapema au baadaye nyumba yetu ya pamoja itatupwa nje ya dirisha. Hatuwezi tena kupoteza wakati.

Je! Unafikiria nini juu ya fedha na uhusiano na tawala za umma?

Ninaamini kwamba ikiwa tutafanikiwa kuiponya kutoka katika mawazo tawala kukisia na kuirejesha kwa roho, kulingana na vigezo vya haki, na wakati huo huo kuweza kulenga kupunguza pengo kati ya wale ambao wanapata mkopo na wale ambao hawapati. Na ikiwa siku moja sio mbali sana kuna hali ambayo kila mwendeshaji atawekeza kulingana na kanuni za maadili na uwajibikaji, itawezekana kupata matokeo yake ambayo yatapunguza msaada kwa makampuni ambayo yanaleta madhara kwa mazingira na amani. Katika hali ambayo ubinadamu unajikuta, inakuwa kashfa bado kufadhili tasnia ambazo hazichangii ujumuishaji wa  zilizotengwa nakuhamsisha, na ambazo zinaadhibu faida ya pamoja kwa kuchafua kazi ya uumbaji. Hivyo ndivyo vigezo vinne vya kuchagua ni biashara ipi zitakazosaidia: ujumuishaji wa waliotengwa, uhamasishaji wa walio wa mwisho , faida ya pamoja  na utunzaji wa kazi  uumbaji.

Tunakabiliwa na moja ya mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu tangu Vita vya Pili vya Kidunia. Nchi zinaenendelea kuchukua hatua za dharura kukabiliana na janga na mtikisiko mkubwa wa uchumi duniani. Ni matarajio yapi kutoka kwa watawala?

“Sasa ni juu ya kujenga kwa upya kutoka katika vifusi. Na kazi hii inawalemea sana wale walio katika nafasi za serikali. Katika kipindi cha wasi wasi juu ya  siku zijazo ambazo hazina uhakika, kwa ajili ya kazi ambayo iko katika hatari ya kupotea au imepotea, kwa kipato ambacho kinaendelea kutotosha na kwa matokeo mengine ambayo kwa sasa yanapelekea shida ni muhimu kusimamia kwa uaminifu, uwazi na kuona mbele. Lakini ni kila mmoja wetu, na sio watawala tu, wameitwa kuacha sintofahamu za kutokujali, ufisadi na ufahamu wa uhalifu.

Ni msingi gani tunaweza kupata msukumo?

“Kinachotokea kinaweza kuamsha wote. Ni wakati wa kuondoa dhuluma za kijamii na kutengwa. Ikiwa tutachukua jaribio kama fursa, tunaweza kujiandalia kesho chini ya bendera ya udugu wa kibinadamu, ambayo hakuna mbadala, kwa sababu bila maono ya pamoja hakutakuwa na siku zijazo kwa mtu yeyote. Kwa kutumia tunda la somo hili, viongozi wa mataifa, pamoja na wale walio na majukumu ya kijamii, wanaweza kuwaongoza watu wa Dunia kuelekea katika siku za usoni zenye kufanikiwa zaidi na za kindugu. Wakuu wa serikali wangeweza kuzungumza wao kwa wao, kujadili zaidi na kukubaliana juu ya mikakati. Sisi sote ndani ya akili zetu tunakumbuka kuwa kuna kitu kibaya zaidi kuliko mgogoro huu: ni  mchezo wa kutumia hovyo na kuharibu. Hatutatoka katika mgogoro tukiwa  sawa: ama tunatoka tukiwa bora au tunatoka tukiwa vibaya zaidi.

Je! Ni kwa tabia na mtazamo gani tunaweza  kuipoteza?

Kwa kujifungia sisi wenyewe. Badala yake, kwa kujenga  tena utaratibu mpya wa ulimwengu unaotegemea mshikamano, kutafiti njia mpya za kutokomeza uonevu, umaskini na ufisadi, wote kwa pamoja, kila mmoja katika sehemu yake, bila kumpa jukumu mwingine na kuchukua jukumu letu wenyewe, tutaweza kuponya dhuluma. Kufanya kazi ya kutoa huduma ya matibabu kwa wote. Kwa kufanya mazoezi hayo na kudhihirisha mshikamano, tutaweza kuinuka tena.

Kwa maneno halisi, tunaweza kuanzia wapi?

Haivumiliki tena kwamba silaha zinaendelea kutengenezwa na kusafirishwa, wakitumia mtaji mkubwa sana ambao ungepaswa kutumiwa kuponya watu, kuokoa maisha. Haiwezekani kujifanya hujuhi kuwa haujaingia mzunguko mbaya sana kati ya vurugu za silaha, umaskini, unyanyasaji na unyonyaji wa sintofahamu za mazingira. Ni mzunguko ambao unazuia upatanisho, unachochea ukiukwaji wa haki za binadamu na unazuia maendeleo endelevu. Dhidi ya mzozo huu wa sayari ambao unakandamiza mustakabali wa ubinadamu, tunahitaji hatua za kisiasa ambazo ni matunda ya makubaliano ya kimataifa. Kwa umoja wa kidugu, wanadamu wana uwezo wa kukabiliana na vitisho vya pamoja, bila ubaguzi mwingine wowote wa kuleta uhalifu, unyonyaji wa kutumia shida, utaifa usioona mbali, propaganda za kujifungia, kutenga na aina nyingine za ubinafsi wa kisiasa.”

Kuhusu uzito wa uchumi wote unaendelea kuelemea kwenye mabega ya wanawake: unafikiria nini?

“Wanawake wanahitaji msaada wa dharura juu ya uendeshaji wa utunzaji wa watoto na sio kubaguliwa katika suala la malipo na taaluma, au kwa kupoteza kazi zao kama wanawake. Badala yake, uwepo wao unazidi kuwa wa thamani katikati ya michakato ya upyaishaji wa kijamii, kisiasa, ajira na kitaasisi. Ikiwa tutakuwa na uwezo wa kuweka hayo katika ya  hali hizi chanya, wataweza kutoa mchango wa uamuzi katika ujenzi wa uchumi na jamii zijazo, kwa sababu wanawake wanaufanya ulimwengu kuwa mzuri na hufanya mantiki hizi kuwa jumuishi zaidi. Na zadi sisi sote tupo tunajaribu kuamka tena, kwa  maana hiyo hatuwezi kupuuza ukweli kwamba kuzaliwa upya kwa ubinadamu kulianza na wanawake. Wokovu ulizaliwa kutoka kwa Bikira Maria, na  ndiyo sababu hakuna wokovu bila mwanamke. Ikiwa tunajali na kuweka moyoni  juu ya siku zijazo, ikiwa tunataka kesho inayostawi, tunahitaji kuwapa wanawake nafasi nzuri.”

Je! Ungependekeza nini hasa kwa wazazi?

“Kucheza na watoto wao ni wakati mzuri zaidi ambao hautakiwi kupoteza. Ninajua familia moja ambayo imeunda kipengele cha kitaasisi nyumbani: Programu. Kila Jumamosi au Jumapili, baba na mama wanashika karatasi pamoja na watoto, wanakubaliana na kuandika miadi yote ya mchezo kati ya watoto na wazazi katika wiki inayofuata, na baadaye wanaitundika kwenye kibao kidogo jikoni. Kwa watoto wanafurahi sana na kuridhika wakati wa kuandika “programu”, ambayo sasa imekuwa jambo la kawaida yao. Mama na baba hawa wanapanda elimu. Niliwaambia hivi: Pandeni elimu”. Kucheza na baba na mama, mtoto hujifunza kuwa pamoja na watu, hujifunza juu ya uwepo wa sheria na hitaji la kuziheshimu, hupata ujasiri huo ambao utamsaidia wakati wa kujitambulisha katika ukweli wa nje, ulimwenguni.  Wakati huo huo, watoto husaidia wazazi wao, hasa katika vitu viwili: kutoa dhamana kubwa kwa wakati wa maisha; na kubaki wanyenyekevu. Kwao wao, awali ya yote ni baba na mama, wengine huja baadaye: kazi, safari, mafanikio na wasiwasi. Na hii hulinda dhidi ya vishawishi vibaya na ubinafsi usi ona kipimo mahali ambamo kuna hatari ya kuangukia humo kila siku.”

Vurugu za Covid zimepunguza matarajio tayari ya hatari ya mamilioni ya watoto ulimwenguni. Vijana wanahangaika kutokuwa na uhakika, upunguzaji wa masomo, kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo unawanyima haki ya baadaye. Je! ungeweza kuwambia nini vizazi vya Covid?

“Ninawapa moyo wasiipe ushindi hali mbaya. Wasiache kuota ndoto kwa macho wazi. Wasiogope kuota yaliyo makubwa. Kwa kufanya kazi kwa ajili ya ndoto zao, wanaweza pia kuwalinda hata kwa wale ambao wanataka kuwafanya wapige gwaride; yaani wenye tamaa, wasio waaminifu na wanaofaidika. Kwa hakika labda kamwe kama katika milenia hii ya tatu vizazi vipya ndiyo wale ambao wanalipa gharama kubwa zaidi ya shida ya uchumi, kazi, afya na maadili. Lakini kujililia haileti chochote cha maana, na kwa kufanya hivyo mgogoro utashinda. Badala yake, ni kuendelea kupambana kama walio wengi tayari wanafanya, vijana hawatabaki wasio na uzoefu, wachanga na hawajakomaa. Hawataacha katika kutafuta fursa. Na baadaye, kuna maarifa. Katika kitabu cha Mwanzo tunasoma (sura ya 2) kwamba Bwana, baada ya kuumba mbingu na dunia, alimchukua mwanadamu na kumweka katikati ya bustani ya Edeni, ili ailime na kumjua. Hakumstaafisha, au kumpa likizo au kukaa kwenye sofa: alimtuma kujifunza na kufanya kazi.

Mungu alimfanya mwanadamu awe na uwezo na shauku ya kujua na kufanya kazi. Na kupenda. “Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe”, hakuna amri nyingine muhimu kuliko hii, Yesu aliwaambia wanafunzi wake (Mk 12:31). Tazama, hapa vijana wana ukweli mpya na nguvu ya kuzindua majukumu ya msingi waliyopewa na Mungu, na kwa maana hiyo kuwa wanaume na wanawake wa maarifa, upendo na kujitoa kwa upendo. Kwa kufungulia kukutana na kushangaa, wataweza kufurahiya uzuri na zawadi za maisha na asili ya maumbile, hisia, upendo na aina zote. Kwa kusonga daima mbele ili kujifunza kitu kutoka kwa kila uzoefu, kueneza maarifa na kukuza tumaini asili la ujana, watachukua hatamu za maisha mikononi mwao na wakati huo huo kuweka uhai wa nguvu ambayo itafanya ubinadamu kuendelea, kuufanya uwe huru. Kwa mana hiyo, hata ikiwa usiku unaonekana kuwa hauna mwisho, lazima tusife moyo. Na, kama alivyokuwa anasema Mtakatifu Philipo Neri  wasisahau kuwa na furaha iwezekanavyo.

MASWALI NA MAJIBU YA PAPA KUHUSU MUNGU NA WAKATI UJAO
15 March 2021, 17:26