Tafuta

2021.03.12 Mkurano wa Papa FRancisko na Rais wa Jamhuri ya Ureno Bwana Marcelo Rebelo de Sousa, 2021.03.12 Mkurano wa Papa FRancisko na Rais wa Jamhuri ya Ureno Bwana Marcelo Rebelo de Sousa, 

Papa Francisko amekutana na Rais wa Ureno Rebelo de Sousa

Mahusiano mema kwa pande zote mbili na masuala ya hali ya kikanda na kimataifa katikati ya janga la zasa zimekuwa ndizo mada msingu kati ya Papa Francisko na Bwana Marcelo Rebelo de Sousa, rais wa Jamhuri ya Ureno katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi baada ya kuchaguliwa tena.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika jumba la kitume Vatican, Papa Francisko Ijumaa tarehe 12 Machi 20201 amekutana na Rais wa Jamhuri ya Ureno, Bwana Marcelo Rebelo de Sousa ambaye baadaye ameweza kukutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akisindikizwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na Mataifa.

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari amesema kuwa katika mazungumzo yao, ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kwenda nchi za nje baada ya kuchaguliwa tena wamependezwa mahusiano yao  mema yaliyopo kati ya Vatican na Ureno, kama pia mchango wa Kanisa Katoliki katika nchi hiyo hasa katika masuala ya uendeshaji wa sasa wa mgogoro wa kiafya, ulinzi wa maisha na kuishi amani kijamii.

Katika muktadha wa urais wa Ureno kwa ajili ya  Jumuiya ya Ulaya, masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa yamezungumziwa,  ambayo kwa upande mwingine mtazamo wa ugumu na kushinda dharura ya janga na kwa ajili ya kutoa kwa amani.

12 March 2021, 16:43