Tafuta

Vatican News
2019.10.04 Maeneo ya Nchi Takatifu 2019.10.04 Maeneo ya Nchi Takatifu 

Nchi Takatifu:Janga limezuia sadaka 2020,mwaka huu tusigeuke upande mwingne

Katika barua ya Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki inazungumzia juu ya mkusanyo wa sadaka ya kila Ijumaa Kuu ambayo hutolewa kusadia nchi Takatifu:Dharura ya kiafya anaandika Kardinali Sandri imezidisha kutengwa kwa wakristo.Sadaka ya mwaka huu iwe fursa tena ya kugeuza macho bila kupuuza ambayo ni ishara ndogo ya mshikamano na ushirikiano.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kardinali Leonardo Sandri Rais wa Baraza a Kipapa la Makanisa ya Mashariki ameandika barua ya kuhamasisha kutoa mchango ambao ni wa kiutamaduni wa Siku ya Ijumaa Kuu  kwa ajili ya Nchi Takatifu. Mkusanyo huo wa sadaka  2021 uwe fursa kwa kila mtu ili asigeuze macho yake upande mwingine, asipite, asipuuze hali za uhitaji na ugumu wa kaka na dada zetu wanaoishi katika Mahali Patakatifu. Ikiwa ishara hii ndogo ya mshikamano na kushirikiana itakoma, itakuwa ngumu. Katika barua hiyo Kardinali anaandika kuwa, "kila Wiki Takatifu tunafanya mahujaji kwenda Yerusalemu na kutafakari fumbo la Bwana wetu Yesu Kristo aliyekufa na kufufuka".  Na Mtume Paulo, ambaye alikuwa na uzoefu hai na wa kibinafsi fumbo hili alifikia kusema, katika Barua kwa Wagalatia kwamba “Mwana wa Mungu alinipenda na akajitoa mwenyewe kwa ajili yangu!” (Gal 2:20). 

Kile alichoishi Mtume pia ni msingi wa mtindo mpya wa udugu ambao unatokana na kazi ya upatanisho na utulivu uliofanywa na Msalabani kati ya watu wote, kama vile Mtakatifu Paulo anavyo andika hata  katika barua yake kwa Waefeso.  Mwaka 2020 , Papa Francisko alipendelea kukumbusha matokeo ya zawadi hiyo ya upatanisho na alifanya kwa njia ya Waraka wake wa "Fratelli tutti". Katika maandiko hayo Papa anaanzia na ushuhuda wa kinabii ambao unapendekezwa na Mtakatifu Francis wa Assi na anataka kutusaidia kusoma katika mwanga wa kidugu kwa wote katika mahusiano na mantiki ya maisha yetu kama vile kidini, kiuchumi, kiekolojia, kisiasa na kimawasiliano.  

Barabara zilizoachwa karibu na Kaburi Takatifu na Jerusalemu ya Zamani zimekuwa mwangwi wa Uwanja wa Mtakatifu Petro  na mvua, mnamo tarehe  27 Machi 2020, akielekea Msalabani: mbele yake ulimwengu wote ulikuwa  kama  kama umepiga magoti, ukiomba mwisho wa janga la virusi vya corona, na kumfanya kila mtu ahisi kuunganishwa na fumbo lile lile la uchungu. Mwaka 2020 umekuwa mwaka wa majaribu na hata kwa Kanisa la Mji Mtakatifu na kwa jumuiya ndogo ya kikristo inaioyisha huko Mashariki ya Kati na ambayo inataka kuwa mwaga , chumvi na chachu ya Injili. Katika mwaka huo Wakristo wa nchi hizo wamefanya uzoefu wa kutengwa   suala ambalo liliwafanya wahisi kuwa  mbali zaidi, kutokuwa na mawasiliano muhimu na ndugu zao kutoka nchi mbali mbali  za ulimwengu. Walipata shida ya kupoteza kazi, kwa sababu ya kukosekana kwa mahujaji, na shida ya kuishi katika hadhi na kutunza familia zao na watoto. Katika nchi nyingi, kuendelea kwa vita na vikwazo vimeongeza athari za janga la corona. Kwa kuongezea, kumekosekana hata misaada ya kiuchumi ambayo mara kadhaah hufanyika katika mkusanyiko kwa ajili ya Nchi Takatifu kila mwana ambao umekuwa ukuwahkikishia uwezekano kwa sababu ya ugumu wa kuifanya makusanyo ayo katika nchi nyingi mnamo  mwaka 2020.

Papa Francisko aliwapatia Wakristo wote sura ya Msamaria Mwema kama kielelezo na kiini cha  upendo wa kuvutia na wa kuunga mkono na mshikamano.  Pia kilichochea kama baraza kutafakari juu ya mitazamo tofauti ya wahusika katika fumbo ili la kushinda kutokujali kwa wale wanaomuona kaka au dada yao akiwa katika shida na kupita mbali “ je ujaitambulisha na nani? Je! Ni yupi kati yao anayeonekana? Lazima tutambue jaribu ambalo linatuzunguka kutopenda wengine, hasa wadhaifu. Tukabiliane na hali hiyo, tumekua katika nyanja nyingi lakini hatujui kusoma na kuandika katika kusindikiza, kutunza na kusaidia jamii dhaifu na wadhaifu wa jamii zetu zilizoendelea. Tumezoea kuangalia upande mwingine kupitia karibu na kupuuza hali hadi zinatuathiri moja kwa moja ”(Fratelli tutti, 64). Swali hili ni gumu, moja kwa moja na linaamua.

Mkusanyo wa sadaka kwa ajili ya Nchi Takatifu 2021  Kardinali Sandri anaandika kuwa uwe fursa kwa kila mtu asigeuze macho yake, asipite, asipuuze hali za uhitaji na ugumu wa kaka na dada zetu wanaoishi katika Mahali Patakatifu. Ikiwa ishara hii ndogo ya mshikamano na kushirikiana itakoma (Mtakatifu Paulo na Mtakatifu Francis wa Assisi wangeiita marejesho) itakuwa ngumu zaidi kwa Wakristo wengi katika nchi hizo kujaribu kuondoka  na hali hiyo nchini mwao, itakuwa kuwa ngumu kusaidia parokia katika utume wao wa kichungaji, na kuendelea na kazi ya kuelimisha kupitia shule za Kikristo na kujitoa kijamii kwa kupendelea maskini na wanaoteseka. Katika hali hii ngumu, iliyooneshwa na kukosekana kwa mahujaji, anasema kuhisi jukumu la kutumia maneno yawe yake ambayo Mtume wa Mataifa aliwaambia Wakorinto miaka elfu mbili iliyopita, kuwaalika kwenye mshikamano ambao hautegemei uhisani lakini Hamasa za Kristo: “Kiuweli, mnaijua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo: kwa kuwa tajiri alijifanya maskini kwa ajili yenu, nanyi mkawa matajiri kwa umaskini wake” (2 Wakor 8: 9).

Na baada ya kukumbuka kanuni ya usawa, mshikamano na kubadilishana mali na mali za kiroho, Mtume anaongeza maneno ya ufasaha leo hii kama wakati huo na ambayo hayahitaji maoni yoyote: “Kumbuka hili: yeyote apandaye haba, atavuna kwa shida na yeye ambaye hupanda kwa upana atavuna kwa upana. Kila mtu na atoe kadiri alivyoamua moyoni mwake, si kwa huzuni au kwa kulazimishwa, kwa sababu Mungu huwapenda wale wanaotoa kwa furaha. Kwa kuongezea, Mungu anao uwezo wa kufanya neema zote kuzidi ndani yenu, ili kila wakati mkiwa na mahitaji ya kila jambo, mpate kufanya ukarimu matendo mema yote ”(2Kor 9,6-8). Barua ya Kardinali inahitimishwa akisema: "Ninayo tayari  furaha kwa ajili yenu, na kuwapatia kutoka moyoni shukrani za Baba Mtakatifu Francisko, Mapadre, Watawa na Waamini ambao manajikita katika  kazi njema ya  kufanikisha Ukusanyaji, kwa uaminifu kwa kazi ambayo Kanisa linawataka watoto wake wote kutekeleza kulingana na njia zinazojulikana".

 

11 March 2021, 16:35