Tafuta

Vatican News
Watawa wanaalikwa kupeleka mwanga penye giza na maisha yao yaangazie kile walichojufunga kifunfo Watawa wanaalikwa kupeleka mwanga penye giza na maisha yao yaangazie kile walichojufunga kifunfo  (AFP or licensors)

Miaka 25 ya Wosi wa kitume wa Maisha ya kitawa

Katika fursa ya miaka 25 ya kuchapishwa Wosia wa Kitume wa Mtakatifu Yohane Paulo II,Kardinali João Braz de Aviz,Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Maisha ya Kitawa na Vyama vya Kitume, anawaelekeza watawa wote,kike na kiume wawe mashuhuda wa uzuri kutoa mwamko na mvuto kwa wengine kwa kile ambacho wanakiona kizuri na cha kweli,kimojawapo kati ya vyote ni uso wa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Watawa wa kike na kiume wameelezwa wao binafsi kuwa na uwezo wa kuamsha kwa upya dhamiri sana kwa wote ya maana ya tumaini , kwa namna ya pekee katika kipindi hiki kigumu ambacho si tu kwa sababu ya janga, lakini hasa madhara yake ambayo yanatuguswa kwa karibu katika maisha ya kila siku kwenye jumuiya nzima ya kiraia na kikanisa. Aliyekumbusha hayo kwa watawa wote ni Kardinali João Braz de Aviz, Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Maisha ya Kitawa na Vyama vya Kitume katika barua ambayo inafanya kumbu kumbu ya miaka 25, tangu kuchapishwa kwa Wosia wa Kitume wa Maisha ya Kitawa na Mtakatifu Yohane Paulo II.

Utambulisho na Utatu

Wosia wa Kitume ulichapishwa mnamo tarehe 25 Machi 1996 kama tunda la tafakari ya Sinodi ya IX ya Maaskofu mnamo Oktoba 1994, na kuhapishwa katika wakati usiookuwa na uhakika, katika wakati wa jamii legevu, katika utambulisho uliochanganyikiwa na uwepo wa udhaifu na kwa maana hiyo barua ilitaka kuimarisha kwa uhakika katika kipinid hicho kwa mujubu wa Kardinali. Ni njia asili ya kuelewa maisha ya wakfu  ambayo inaunganisha kimungu na kibinadamu,ili kugundua uhusiano wa fumbo la  kushangaza na lenye kung'aa wakati wa  kupaa na kushuka, kati ya urefu uliopitiliza na kuzamishwa katika pembezoni mwa mwanadamu, kati ya uzuri wa hali ya juu wa kutafakari na umaskini wenye maumivu ya kuhudumia. Kardinali katika barua hiyo anaandika kwamba "Utambulisho unasimika mzizi juu ya uhusianao na Utatu kwa sababu ni picha halisi ya Kristo aliyebadilika na ambaye anajionesha utukufu na uso wa Baba katika mwangaza wa Roho", anandika Kardinali.

Uhusiano na Kanisa na ulimwengu

Vikwazo vya uhusiano huu, anaandika, wokovu ambao hupitia katika maisha ya wale wanaochuku jukumu la mwingine, ushuhuda wa udugu na ambao unaishi kile unachotangaza na kufurahia, utakatifu sio wa masharti ya ukamilifu, lakini ni ya wenye dhambi maskini na kujitoa ambao hawakubaliani na maadili ya ulimwengu na kiu cha ulimwengu cha furaha, ambapo kwa leo hii inamaanisha maisha ya wakfu yanahisi kuwa ni maskini kuliko hapo awali, lakini yanaishi kwa neema na  zaidi kuwa na uhusiano na Kanisa na ulimwengu, pamoja na wale wanaoamini na wale ambao hawaamini, pamoja na wale wanaoteseka na wako peke yao.

Hisia za kuwa mwana wa Mungu

Hii ni kweli hasa wakati Wosia wa Kitume unapoanza kukabiliana na mada ya  malezi kupitia uhusiano ambao unafikia mawasiliano ya namna hii  ya kina kama vile kugundua tena ndani binafsi ule unyeti wa kuwa Mwana, unyeti wa Baba kujifanya mwili na unyeti wa Mungu ambaye anasikilia kilio cha wanaokandamizwa, anasikilizwa maombi ya wajane na anataka kua mtu na kwa ajili ya mtu. Akiendelea Kardinali De Avis anaandika kuwa “Tunataka kuamini kwamba maisha ya kitawa na karama zake nyingi ndio kielelezo cha unyeti huo" na kwamba "kila taasisi inasisitizia kwa manaa nyingine hisia ya kimungu ikiwa inaelekeweka kama machakato wa malezi yanayoendelea katika wakati yaani kwa maisha yote hata zaidi kutekelezwa leo hii. Ni katika kupeleka kupata hisiza zile zile mapendo, shauku, ladha, maratajio, ugumu, ndoto ya mwana, mtumishi na kondoo.

Kushangazwa na uzuri

Mtu aliyeweka wakfu kwa maana hiyo Kardinali anasema, ameitwa kuwa shuhuda wa uzuri. Ikiwa Mungu ni mzuri na Bwana Yesu ndiye mzuri zaidi kati ya watoto wa wanadamu, anaandika Kardinali Braz de Aviz, kwa maana hiyo basi kuwekwa wakfu kwake ni uzuri. Ni kupitia njia ngumu ambayo inaonekana kuwa njia pekee ya kufikia ukweli, au kuifanya iwe ya kuaminika na ya kuvutia. Uzuri lazima uwe ushuhuda na neno linalotolewa, kwa sababu uzuri ni uso ambao tunatangaza, na lazima uwe wa kidugu na ambao kweli unapumua hali hiyo ya kidugu. Uzuri lazima uwe hekalu na liturujia, ambayo wote wanaitwa kuwa hivyo, kwa sababu ni vizuri kusali na kuimba sifa za 'Aliye Juu' na kuacha husomwe kama neno lake. Uwepo wetu wa kuwa wasafi wa moyo ni kwa sababu ya kuweza kupenda kwa moyo wake: Tabia ya kuwa kwetu maskini ni kusema kwamba yeye ndiye hazina pekee. Kutii mapenzi yake ya wokovu, pia kati yetu ni kumtafuta yeye peke yake.  Uzuri ni kuwa na moyo ulio huru wa kukaribisha uchungu kwa wale wanaoteseka ili kuelezea huruma ya Milele kwao na hata mazingira lazima yawe mazuri, kwa unyenyekevu na kiasi cha ubunifu, ili kila kitu katika makao kiruhusu uwepo na kiini cha Mungu.

25 March 2021, 16:07