Tafuta

Vatican News
11 03.2021:Imekabidhiwa zana mpya katika kituo cha Afya cha "Madre di Misericordia" yaani "Mama wa Huruma mjini Vatican kwa ajili ya wahitaji wasio kuwa na makazi. 11 03.2021:Imekabidhiwa zana mpya katika kituo cha Afya cha "Madre di Misericordia" yaani "Mama wa Huruma mjini Vatican kwa ajili ya wahitaji wasio kuwa na makazi.   (ANSA)

Kituo cha afya pembeni mwa Uwanja wa Mtakatifu kupata mashine

Zana ya uchunguzi itapanua uwezekano wa kupima na kutambua matatizo ya afya za watu wasio na makazi wanaohitaji matibabu.Mashine hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa Sadaka ya Kitume kutoka katika chama cha Siloe. Kardinali Krajewski amesema kwamba hiyo ndiyo huruma ya dhati.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Uchunguzi wa haraka wa damu na uchunguzi zaidi katika kituo kiitwacho “Mama wa Huruma, kilichopo pembeni mwa uwanja wa Mtakatifu Pietro, kimepata zawadi ya chombo kipya cha (biochemical VChemy-S) kilichotolewa na chama cha Siloe kwa kukikabidhi katika Ofisi ya Sadaka ya Kitume. Hii ni Mashine ya uchunguzi na uchambuzi wa kikliniki, hasa kwa ajili ya magonjwa ya wale wanaoishi barabarani, kwa namna ya pekee magonjwa yenye asili ya chakula na ulevi, kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa rais wa chama hicho Bwana Andrea Benassi.

Huruma ya matendo ya dhati na siyo maneno

Huruma ya kweli iko katika matendo, na siyo katika maneno, amesema hayo  Kardinali Konrad Krajewski, Msimamizi wa Sadaka ya Kitume baada ya kubariki kifaa hicho kipya, kilichofika katika Kituo hicho tarehe 11 Machi 2021.  “Ni jambo thabiti sana kwa maskini wetu,  wanapokuja hapa hutoka wakiwa salama kwa maisha yao. Kwa njia hii tutajua vizuri ni wapi tunaweza kuwatibu na ni dawa gani tunaweza kuwapatia kwa sababu, hakuna mtu anayetoka hapa bila dawa” amebainisha. Kwa kuongezea Kardinali amefafanua kuwa uharaka huo  wakati wa uhitaji kwa hakika ndiyo mojawapo ya sifa za huruma, wakati Yesu alipokuwa akikutana na wagonjwa, hakusema 'njoo wiki moja baadaye  au mwezi, ndipo tutaona', lakini alipokutana nao aliwatibu mara moja! Kardinali Krajewski alisisitiza hayo kwa tabasamu, akikumbuka jinsi Kituo hicho cha Mama wa Huruma  kilivyopendwa sana na Baba Mtakatifu Francisko, ambaye alitaka kuwa maskini wakaribishwe nyumbani kwake, katika nafasi kubwa ambayo ni pendwa kwa Wakristo.

Kupanua uchunguzi kwa waliobaguliwa

“Tunapokea watu ambao hawapati uchunguzi wa aina yoyote, ambao ni watu waliokataliwa kutoka katika mfumo wa kitaifa wa afya kwa sababu ni tofauti, kutokana na uchumi, hadi ukiritimba, kutokuwa na bina ya kiafya kwa sababu ya uwepo katika nchi ambao haujarekebishwa katika eneo la kitaifa”, amekumbuka hayo Daktari Lucia Ercoli, meneja wa afya wa Taasisi ya Tiba ya Mshikamano na daktari katika kituo hicho. Aidha Dk, Ercoli amesema “Kutumia mashine hii mpya ili kufanya vipimo vya damu, itawawezesha kukuza utambuzi, pia vigezo vinavyoonesha hali ya ugonjwa huyo na jinsi gani ugonjwa huo unavyoibuka shukrani kwa dawa”.

Watu 1200 wamesaidiwa wakati wa janga

Kituo cha afya cha  “Mama wa Huruma” ni mojawapo tu ya zana zinazotumiwa na Baba Mtakatifu Francisko, kupitia  Sadaka ya Kitume, kusaidia maskini walio karibu naye. Katika mwaka huu wa janga kumekuwa na hatua nyingi, kuanzia na  usimamizi wa vipimo vya haraja vya kujua maambukizi ya virusi  na chanjo kwa wasio na makazi hadi msaada wa mitungi ya kupumua katika hospitali za Italia na ulimwenguni kote. Hasa, katika janga hili alitoa msaada kwa watu 1200  walioko pembezoni, kwa nchi 96 tofauti. Kwa mujibu wa Dk, Ercoli amesema hii imekuwa sasa kituo ambacho vifaa vingi vimekusanywa na hii inaonekana kwake ishara nzuri zaidi, kwamba ni kituo kinachokaribisha watu wa pembezoni na kilichopo katikati ya pembezoni.

15 March 2021, 17:19