Tafuta

Vatican News
2021.03.09  Sr. Nuria Calduch-Benages 2021.03.09 Sr. Nuria Calduch-Benages 

Katibu mpya wa Tume ya Kipapa ya Kibiblia ni mtawa

Ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana na mtalam wa kozi ya Maandiko matakatifu Sr. Nuria Calduch-Benages,Mwanashirika wa Familia Takatifu ya Nazareth ambaye ameteuliwa na Papa Francisko kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi kama hiyo.Aliwahi kushiriki katika kazi ya Tume ya Utafiti juu ya ushemasi wa wanawake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Uwepo mpya wa wanawake unaibuka kati ya majukumu ya hali ya juu ya taasisi ya Vatican kwa utashi wa Papa. Aliyepewa jukumu hilo leo hii tarehe 9 Machi 2021, kuwa katibu wa Tume ya Kipapa ya Kibiblia kwa mara ya kwanza ni mtawa kutoka Baracellona, Sr. Nuria Calduch-Benages, ambaye tangu mwaka 2014 aliingia kwa mara ya kwanza katika kiungo hicho cha Vatican na kuthibitishwa tena Januari uliyopita kwa miaka mitano hadi 2025.

Heshima inayomstahilisha kuwa msomi wa kibiblia na kwa takriban miaka kumi, baada ya uzoefu wa hapo awali, amekuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, ambapo anafundisha Agano la Kale. Miongoni mwa nyadhifa nyingine, yeye ni profesa mgeni katika Taasisi ya Kipapa ya Bibilia ya Roma, mshiriki mwenye bidii katika huduma kwenye Shirikisho la Bibilia Katoliki,  mjumbe  wa majarida maarufu pia Kamati ya Sayansi ya Historia ya jarida la Wanawake (Chuo Kikuu cha Firenze, Italia) na safu ya “Tesis y Monografías” iliyochapishwa na Neno la Kimungu (Estella). Mnamo 2008 alishiriki katika Sinodi ya Neno kama mtaalam na mnamo 2016, Papa Francisko alimwita kuwa sehemu ya kundi la tume ya utafiti juu ya ushemasi wa wanawake (2016-2019).

09 March 2021, 16:15