Tafuta

Vatican News

Hija ya kitume ya Papa nchini Iraq:Papa amemaliza hija yake

Shukrani kwa Mungu na kwa wote waliomsindikiza katika hija yake ya kitume aliyoanza Ijumaa tarehe 5 Machi 2021.Ndege imeanza safari kutoka Baghdad saa 1:54 asubuhi na anaratajia kufika Roma saa 6.45 hivi masaa ya Ulaya.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Imehitimishwa hija ya Papa Francisko nchini Iraq ikiwa ni ziara ya Kitume ya 33 kimataifa katika nchi ambayo Papa Francisko kamwe hakusahau katika sala zake na miito yake na matashi yake ya kutaka kuwakumbatia na kuwatia moyo watu wapendwa wa nchi hiyo. Ndege imeanza safari kutoka Baghdad saa 1.54 asubuhi, na anaratajia kufika Roma, Italia karibu saa 6.45 masaa ya Ulaya.

Video fupi inaonesha jinsi ambavyo Papa Fancisko ameacha nchi ya Iraq, na alivyoagana kabla ya kuacha mahalia ambapo alifika Ijumaa, tarehe 5 Machi  2021, akiwa mwanahija wa amani na matumaini kama nembo ya kiinjili ilivyokuwa Ninyi ni ndugu. Kwa hakika ni ziara ya kihistoria mbayo kwa mara ya kwanza Papa ametembelea katika nchi ya Ghafu hiyo na ambayo sehemu kubwa ni Washiia.

08 March 2021, 10:01