Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko nchini Iraq:kilichojiri!

Ifutayo ni video inayoonesha kwa ufupi kile kilichojiri kwa siku hizi tatu za hija ya 33 ya kitume ya Papa Francisko iliyoanza tarehe 5 hadi 8 Machi 2021 nchini Iraq.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa siku tatu za kina za Papa Francisko katika ziara yake ya kitume nchini Iraq tangu tarehe 5 Machi na kuhitimisha tarehe 8 Machi, ni matukio mbali mbali yalifanyika huko. Video fupi inaonesha matukio hayo kwa ufupi kama vile Jumapili jioni tarehe 7 Machi 2021, baada ya mapumziko mchana kwenye Seminari ya Mtakatifu Petro huko Erbil, aliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Michezo wa “Franso Hariri”. Papa ametembelea na kusali katika Jumuiya ya Qaraqosh ambapo wamesali na amesikiliza shuhuda za waamini na viongozi wa Kanisa na kuona magofu, lakini pia hata mchakato wa ujenzi mpya wa Iraq unaoendelea hadi sasa.

Akiwa nchini Iraq amewaombea wale wote waliofariki dunia wakati wa vita, ghasia na vitendo vya kigaidi nchini Iraq. Aidha aliweza kukutana na kuzungumza na viongozi wa dini na serikali ya Kurdistan ya Iraq na kuendelea na safari hadi  Mosul. Jumamosi tarehe 6 Machi 2021, Papa aliadhimisha Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu. Hata hivyo siku hiyo pia alikutana na viongozi wa dini mbalimbali kwenye Uwanda wa Uru ya Wakaldayo. Baada ya hapo alikwenda hadi mjini Najaf.

Papa Francisko aliadhimisha siku ya Sala ya Watoto wa Ibrahimu. Shuhuda zimeweza kutolewa kutoka kwa waamini kuhusu imani zao. Akiwa katika ziara hiyo,  Papa hakukosa kukutana na kutoa neno kwa Maaskofu, Mapadre, Watawana walei na kuwaombea waamini waliuwawa kikatili katika Kanisa kuu la Bikira Maria Mama wa Mkombozi.  Haitasahulika hotuba yake ya kwanza, alipofika siku ya Ijumaa tarehe 5 Machi 2021 wakati wa kukutana na viongozi wa Serikali, wanadiplomasia pamoja na viongozi wa asasi za kiraia. Mada ambazo alizigusia ni pampja na janga la sasa la virusi vya corona au Covid-19, matokeo ya uharibifu wa vita na matendo ya kigaidi, mazungumzo ya kidini na zaidi kusisistiza umuhimu wa mshikamano kidugu.

08 March 2021, 16:02