Tafuta

Vatican News
Balozi Rene' Juan Mujica Cantelar wa Cuba tarehe 29 Machi 2021 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Balozi Rene' Juan Mujica Cantelar wa Cuba tarehe 29 Machi 2021 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican.  (Vatican Media)

Balozi Renè Juan Mujica wa Cuba Awasilisha Hati za Utambulisho!

Mheshimiwa René Juan Mujica Catelar, Balozi mpya wa Cuba mjini Vatican. Balozi René Juan Mujica Catelar alizaliwa tarehe 24 Novemba 1948, ameoa na kubahatika kupata watoto watatu. Ni kiongozi aliyebobea katika masuala ya siasa za mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa. Amewahi kuwa Balozi wa Cuba nchini Ubelgiji, Luxembourg, Umoja wa Ulaya na Ujerumani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 29 Machi 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa René Juan Mujica Catelar, Balozi mpya wa Cuba mjini Vatican. Balozi René Juan Mujica Catelar alizaliwa tarehe 24 Novemba 1948, ameoa na kubahatika kupata watoto watatu. Ni kiongozi aliyebobea katika masuala ya siasa za mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa. Katika maisha yake, kitaaluma kati ya mwaka 1967 hadi mwaka 1969 alikuwa ni Afisa katika Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Umoja wa Vijana wa Kikomunisti. Kati ya Mwaka 1969 hadi mwaka 1970 aliteuliwa kuwa mtaalam wa Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa. Kati ya mwaka 1970 hadi mwaka 1973 alifanya kazi kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa.

Na kati ya mwaka 1973 hadi mwaka 1977 aliteuliwa kuwa mtaalam wa ushirikiano kati ya Cuba na Marekani hadi mwaka 1979. Amewahi pia kuwa ni Mshauri wa ushirikiano kati ya Cuba na Marekani; Mwakilishi wa kudumu wa Cuba kwenye Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 1990 hadi mwaka 1993. Kati ya mwaka 1993 hadi mwaka 1996 alikuwa ni Mshauri wa uhusiano kati ya Cuba na Marekani. Amewahi pia kuwa ni Balozi wa Cuba nchini Ubelgiji, Luxembourg na Umoja wa Ulaya, EU. Pia amewahi kuwa Balozi wa Cuba nchini Ufaransa, Uingereza na Ireland na Marekani. Kati ya mwaka 2013 hadi mwaka 2017 aliteuliwa kuwa ni Balozi wa Cuba nchini Ujerumani na mtaalamu wa masuala ya kisiasa na uhusiano wa nchi za nje, hasa zaidi na Marekani.

Cuba
30 March 2021, 15:33