Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 18 Machi 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Jean Jude Piquant, Balozi mpya wa Haiti mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 18 Machi 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Jean Jude Piquant, Balozi mpya wa Haiti mjini Vatican. 

Balozi wa Haiti Awasilisha Hati za Utambulisho Mjini Vatican

Mheshimiwa Balozi Jean Jude Piquant, alizaliwa tarehe 24 Desemba 1962, ameoa na kubahatika kupata watoto wawili. Ni mtaalam katika masuala ya umisionari, haki msingi za binadamu na haki za kimataifa. Kunako mwaka 2016 alijipatia shahada ya uzamili katika masuala hayo kutoka Chuo cha St. Thomas University, School of Law, Miami Florida. Amewasilisha hati zake za utambulisho!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 18 Machi 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Jean Jude Piquant, Balozi wa Haiti mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Mheshimiwa Balozi Jean Jude Piquant, alizaliwa tarehe 24 Desemba 1962, ameoa na kubahatika kupata watoto wawili. Ni mtaalam katika masuala ya umisionari na haki msingi za binadamu na haki za kimataifa. Kunako mwaka 2016 alijipatia shahada ya uzamili katika masuala hayo kutoka Chuo cha St. Thomas University, School of Law, Miami Florida.

Lakini kati ya mwaka 1990 hadi mwaka 2010 alijikita zaidi katika kufundisha. Kati ya Mwaka 1998 hadi mwaka 2000 alifundisha kama mkufunzi mwandamizi Chuo Kikuu cha Broooklyn, City University of NY kati yam waka 200 – 2010. Kati ya Mwaka 2011 hadi mwaka 2013 alikuwa ni Msahauri, Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa. Kati ya Mwaka 2018 hadi mwaka 2019 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu, Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa.

Haiti
18 March 2021, 15:27