Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Leopoldo Girelli kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini India, kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Palestina, Cyprus, Yerusalemu na Palestina. Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Leopoldo Girelli kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini India, kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Palestina, Cyprus, Yerusalemu na Palestina. 

Askofu mkuu Leopoldo Girelli Balozi wa Vatican Nchini India

Askofu mkuu Leopoldo Girelli alizaliwa tarehe 13 machi 1953 huko Predore, Jimbo Katoliki la Bergamo, Kaskazini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Juni 1978 akapewa Daraja takatifu ya Upadre. Tarehe 13 Aprili 2006 akateuliwa kuwa Balozi na Askofu mkuu na hivyo kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu tarehe 17 Juni 2006. Ni kiongozi mbobezi sana!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Leopoldo Girelli kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini India. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Leopoldo Girelli alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Israeli, Cyprus na Mwakilishi wa Kitume mjini Yerusalemu na Palestina. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Leopoldo Girelli alizaliwa tarehe 13 Machi 1953 huko Predore, Jimbo Katoliki la Bergamo, Kaskazini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Juni 1978 akapewa Daraja takatifu ya Upadre.

Tarehe 13 Aprili 2006 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Timor ya Mashariki, Singapore, pamoja na kuwa ni Mjumbe wa Kitume nchini Malaysia na Brunei Darussalam. Akampandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu na hivyo kuwekwa wakfu tarehe 17 Juni 2006. Tarehe 13 Septemba 2017, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Israeli, Cyprus na Mwakilishi wa Kitume mjini Yerusalemu na Palestina. Tarehe 13 Machi 2021 Baba Mtakatifu amemteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini India.

Uteuzi India
13 March 2021, 15:56