Tafuta

Uzee ni zawadi kwa Mungu.Pendkezo la Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha ni kwamba wazee wasindikizwe katika nyumba zao za kifamilia Uzee ni zawadi kwa Mungu.Pendkezo la Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha ni kwamba wazee wasindikizwe katika nyumba zao za kifamilia 

Tutunze wadhaifu na wazee&uzee ni zawadi ya Mungu!

Imewakilishwa Hati ya Taasisi ya Kipapa ya Maisha kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungaani ya binadamu kuhusu hali ya waze baada ya janga.Wito kwa Jumuiya yote ya kiraia,Kanisa na tamaduni zote za kidini ulimwenguni,shule,watu wa kujitolea,tasnia za burudani,uchumi na mawasiliano kijamii kuwa lazima kuhisi jukumu na kuunga mkono hatua ya kuwasindikiza katika mazingira ya familia.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Janga limeleta mwamko maradufu wa utambuzi kwa upande mmoja kutegemeana kati ya kila mtu na kwa upande mwingine hukosefu mkubwa  wa usawa. Sisi sote tuko katikati ya dhoruba sawa, lakini kwa maana nyingine inawezeka  kusema kuwa tunapanda mitumbwi tofauti yaani ile dhaifu zaidi inayozama kila siku. Ni muhimu kufikiri tena mtindo wa maendeleo wa sayari nzima. Kila mtu anaalikwa: siasa, uchumi, jamii, mashirika ya kidini, kuanzisha utaratibu mpya wa kijamii ambao unaweka katikati wema wa  watu. Hakuna tena faragha ambayo haitoi changamoto ya umma ya jamii nzima. Upendo kwa ajili ya wema wa wote sio ubishani wa Kikristo, ni katika usemi wake halisi wa sasa ambao umekuwa suala la maisha au kifo, kwa kuishi pamoja kunastahili heshima ya kila mjumbe wa jumuiya. Ndivyo inaadikia Taasisi ya Kipapa ya Maisha katika Hati iliyoopewa kichwa Uzee: wakati wetu ujao. Haki za wazee baada ya janga”  iliyochapishwa Jumanne, tarehe 9 Februari 2021, kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu.

Wazee katika janga wameathirika sana

Katika hati hiyo inabainisha kuwa wazee wamekuwa miongoni mwa walioathirika zaidi na janga hilo. Idadi ya vifo kati ya watu wenye umri zaidi ya 65 ni ya kushangaza. Wakati wa wimbi la kwanza la janga , sehemu kubwa ya vifo vya Covid-19 ilitokea katika taasisi za kutunza wazee, maeneo ambayo yalipaswa kulinda walio dhaifu wa kijamii, lakini ikawa ni mahali pa vifo kuathiri vibaya zaidi kuliko wale waliokuwa nyumbani na katika mazingira ya familia. Kulingana na mahesabu  ya takwimu, inaweza kuonekana kuwa familia, kwa upande mwingine, imekuwa na ulinzi zaidi wa wazee zaidi. Kuwekwa kwa wazee, hasa walio katika mazingira magumu zaidi na upweke katika vituo vya kutunza kama suluhisho pekee linalowezekana la kuwatunza, katika mazingira mengi ya kijamii limeonesha ukosefu wa umakini na unyeti kwa walio dhaifu, ambao ingefaa kutumia njia za kuwekeza zinazofaa kwa dhamana ya utunzaji bora zaidi kwa wale wanaohitaji zaidi, katika mazingira ya kifamilia. Njia hii inadhihirisha wazi na kile ambacho Baba Mtakatifu Francisko alikifafanua kuwa ni “utamaduni wa kibaguzi ”. Ni zaidi ya wakati wowote unaofaa kuanza tafakari makini, yenye kuona mbali na uaminifu juu ya jinsi gani jamii ya kisasa inapaswa kuwafikia wazee, hasa pale ambapo ni wadhaifu. Kwa kuongezea, kile kilichotokea wakati wa Covid-19 kinazuia suala la utunzaji wa wazee kufutwa na utaftaji wa nani mwenye makosa, mhalifu mmoja na kwa upande mwingine, kwamba ni kama kuibuka kwaya ya kutetea matokeo bora ya wale ambao wameepuka kuambukiza katika nyumba za wazee. Tunahitaji maono mapya, dhana mpya inayoruhusu jamii ya kuwatunza wazee, inasisitza hati.  Kwa mujibu wa Taasisi ya kipapa ni muhimu kuifanya miji iweze kuishi pia wazee. Ni muhimu kuifanya miji yetu kujumuisha na maeneo ya kukaribisha wazee, kwa jumla, kwa kila aina ya udhaifu.

Jukumu la kuunda mazingira bora zaidi ili wazee waweze kuishi maisha yao

Kwa ngazi ya kiutamaduni na dhamiri ya raia na ya Kikristo hati hiyo inaendelea kueleza kwamna kufikiria kwa upya, kwa kina mitindo ya kutoa msaada kwa wazee ni nafasi nzuri sana. Kujifunza kuwaheshimu wazee ni muhimu kwa mustakabali wa jamii zetu na hatimaye, kwa ajili ya maisha yetu ya baadaye. Ni wajibu na jukumu la kuunda mazingira bora zaidi ili wazee waweze kuishi wakati huu wa maisha, kadiri iwezekanavyo, katika mazingira yao ya kifamilia na urafiki wa kawaida. Huduma ya nyumbani lazima ifungamanishwe, na uwezekano wa huduma ya matibabu nyumbani na usambazaji wa kutosha wa huduma katika eneo lote. Ni muhimu na ya dharura kuwatunza wazee mahali popote walipo katika maisha yao. Yote hayo  yanahitaji mchakato wa uongofu kijamii, kiraia, kiutamaduni na kimaadili. Vivyo hivyo, ni wazi hitaji la kusaidia familia ambazo, hasa ikiwa zinaundwa na watoto na wajukuu wachache, haziwezi kujimudu peke yao, nyumbani, jukumu ambalo wakati mwingine linakuwa gumu sana la kutunza mgonjwa ambaye anahitaji, gharama kubwa kwa maana ya nguvu na fedha. Mtandao mpana wa mshikamano lazima uanzishwe tena, sio lazima na msingi wa uhusiano wa damu, lakini ambao kulingana na urafiki, hisia za kawaida, ni ukarimu wa kurudi katika kujibu mahitaji ya wengine. Kuporomoka kwa mahusiano ya kijamii kunaathiri wazee kwa njia fulani, hati imesisitiza.

Mchango wa Kanisa Katoliki

Kanisa Katoliki pia limetoa na linaendelea kutoa mchango wake katika usimamizi wa nyumba nyingi ambazo zinahifadhi na kuwatunza wazee. Uwepo wa wafanyakazi wa kidini ni sababu ya thamani isiyo na shaka kwa taasisi za kizamani na zilizoheshimiwa, ambazo kwa muda mrefu zimekuwa suluhisho halisi kwa shida ngumu ya kijamii, kama vile kuzeeka. Majimbo, parokia na jumuiya za kikanisa Taasisi ya Kipapa ya Maisha inatoa inawaalika kutafakari kwa umakini zaidi katika ulimwengu wa wazee. Katika miongo ya hivi karibuni mapapa wameingilia kati mara kadhaa kuomba hali ya uwajibikaji na utunzaji wa kichungaji kwa wazee. Uwepo wao ni mali kubwa. Inatosha  kufikiria jukumu la uamuzi walilochukua katika kuhifadhi na kurithisha imani kwa vijana katika nchi zilizo chini ya serikali za wasioamini Mungu na za kimabavu. Uinjilishaji lazima ulenge ukuaji wa kiroho wa kila kizazi, kwani wito wa utakatifu ni wa kila mtu, hata kwa babu na bibi. Sio wazee wote tayari wamekutana na Kristo na hata ikiwa mkutano huo ulifanyika, ni muhimu kuwasaidia kugundua kwa mara nyingine tena maana ya Ubatizo wao wenyewe, katika kipindi maalum cha maisha .

Ushuhuda wa wazee unaweza kutafsiriwa kama mafundisho ya maisha

Kwa kuhitimisha hati hiyo inabainisha juu ya thamani ya ushuhuda ambao unaweza kutolewa na wao walio wadhaifu. Hii inaweza kutafsiriwa kama magisterium, yaani mafundisho ya maisha. Wazee wanatukumbusha udhaifu mkubwa wa kila mwanadamu. Katika udhaifu ni Mungu mwenyewe ambaye, kwanza kabisa, ananyoosha mkono wake kwa mwanadamu. Uzee lazima pia ueleweke katika upeo huu wa kiroho: ni umri wa kupendeza wa kujikabidhi  kwa Mungu. Jamii ambayo inajua jinsi ya kukaribisha udhaifu wa wazee ina uwezo wa kumpa kila mtu tumaini la siku zijazo. Kuondoa haki ya kuishi ya wale ambao ni dhaifu, kwa upande mwingine, inamaanisha kuiba matumaini, hasa hasa kwa vijana. Hii ndiyo sababu kuwatupa wazee, hata kwa lugha, ni tatizo kubwa kwa wote. Hii inamaanisha ujumbe wazi wa kutengwa, ambao ndiyo msingi wa ukosefu wa kukaribisha: kuanzia kwa mjamzito hadi mlemavu, kutoka kwa mhamiaji hadi kwa yule anayeishi barabarani.

Watu wadhaifu hawakubaliwi katika jamii

Hati hiyo inendelea kufafanua kuwa maisha hayakubaliwi ikiwa ni dhaifu sana na yanahitaji utunzaji, hayapendwi katika mabadiliko yake, hayakubaliwi katika kukumbatiwa kwake. Kwa bahati mbaya sio tukio la mbali, lakini ni jambo linalotokea mara kwa mara, ambapo kuachwa, kama Papa anavyorudia,kusema inakuwa aina ya euthanasia iliyofichwa na inapendekeza ujumbe ambao unaweka jamii nzima katika hatari. Kuwanyima wazee jukumu lao la unabii, kuwaweka kando kwa sababu zenye tija, husababisha ufukara usiohesabika, upotevu wa busara na ubinadamu usiosameheka. Kwa kuwatupa wazee, mizizi inakatwa ambayo inaruhusu jamii kukua kuekelea juu na siyo kujipendekeza kwa mahitaji ya wakati uliopo. Kwa maana hiyo wito ni mkuu ni kwamba Jumuiya yote ya kiraia, Kanisa na tamaduni mbalimbali za kidini  ulimwengu wa utamaduni, shule, watu wa kujitolea, tasnia za burudani, uchumi na mawasiliano ya kijamii lazima zihisi jukumu la kupendekeza na kuunga mkono hatua mpya na za busara kwa sabababu inawezekana kwa wazee kwasindikiza na kusaidiwa katika mazingira ya kifamilia, yaani nyumbani kwao na kwa hali yoyote katika mazingira ya nyumbani ambayo yanaonekana kama nyumba kuliko hospitali. Hii ni hatua ya kugeuza utamaduni na kutekelezwa!

09 February 2021, 17:39