Tafuta

Vatican News
INAWEZEKANA KUZUIA HEWA CHAFUZI MJINI KWA KUTUMIA BAISKELI INAWEZEKANA KUZUIA HEWA CHAFUZI MJINI KWA KUTUMIA BAISKELI  (ANSA)

Usafiri wa mijini unaweza endeshwa na roho ya kijumuiya!

Tafakari ya Padre Joshtrom Isaac Kureethadam,mratibu wa Sekta ya Ekolojia na Uumbaji ya Kitengo cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu amesisitiza kuwa usafi jinini unapaswa uwe na roho ya kibinadamu.Katika mahojiano na Vatican News amerudia kutafakari hotuba yake aliyofanya wiki hii katika kongamano la “MobilitARS”, mafunzo ya Waraka wa Laudato sikuhusu mabadiliko ya uhamaji na nafasi ya miji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ujumbe muhimu wa Laudato si, kutoka Waraka wa Papa Francisko juu ya utunzaji wa Mazingira nyumba yetu ya pamoja, unatutaka kwamba tujue kuwa  sisi ni familia moja. Kwa njia hiyo ni lazima tufikirie kama jamuiya moja pia katika nyanja ya usafiri ili kuondokana na tabia za mahesabu tuliyonayo, na ambayo ni sekta inayosababisha karibu robo ya uzalishaji wa gesi chafu ambayo husababisha mabadiliko ya tabianchi kwa kiasi kikubwa. Ni tafakari ya Padre Joshtrom Isaac Kureethadam, mratibu wa Sekta ya Ekolojia na Uumbaji ya Kitengo cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu. Katika mahojiano na Vatican News, Mtawa huyo wa Kisalesiani amerudia kutafakari hotuba yake aliyofanya wiki hii kwenye tukio la kongamano la “MobilitARS”, la mafunzo ya kuzungumzia jukumu la Waraka wa Laudato si katika majadiliano juu ya mabadiliko ya uhamaji na nafasi ya mijini.

Katika hali ya mabadiliko ya hali ya hewa inayoendelea, Padre Joshtrom ameelezea, kuwa hakuna wakati mwingi wa kubadilisha njia kwa kuzingatia kwamba kilio cha dunia pia ni cha maskini.  Dhana ya jumuiya kwa njia hiyo inakuwa muhimu hasa katika nyanja ya usafiri. Kwa mfano katika jiji kama Roma mara nyingi ni kuona  magari mengi yakiwa na mtu mmoja tu ndani. Badala yake, uhamaji wa jumuiya unapaswa kuimarishwa na kuhimizwa: Usafiri wa umma, ujumuishaji wa gari kushiriki safari, baiskeli, zote zikiwa na roho ya jumuiya.

Akigusia juu ya Waraka wa Laudato si uliochapishwa mnamo  2015, mratibu wa Sekta ya Ekolojia na Uumbaji wa Kitengo cha Baraza la Kipapa cha Huduma ya maendeleo fungamani ya Binadamu anarudi katika ombi la kongamano la MobilitARS, ambalo tukio lao la mwisho litakalofanyika kwa njia ya mtandao tarehe  24 Februari 2021 juu ya kaulimbiu ya “jiji lenye ujasiri” . Je! Ni ulimwengu gani tutawaachia watoto, watoto ambao wanakua, kwa vizazi vijavyo?, anajiuliza Padre huyo na   jibu kwamba lazima kuacha umimi na kuelekea katika sisi kwa sababu hata katika usafiri wa mijini, jumuiya ndiyo jamii ambayo inafupisha na kuzungukia kila kitu. Kwaresima tunayoipitia ni wakati muafaka wa kukumbatia na kupata kuishi utu na umuhimu ulioongozwa na Papa Francisko.

19 February 2021, 17:38