Tafuta

Vatican News
Wakati umefika kwa Jumba la Kioo kuchukua jukumu lake kwani sasa ni wazi kuwa ni suala la usalama wa ulimwengu. Wakati umefika kwa Jumba la Kioo kuchukua jukumu lake kwani sasa ni wazi kuwa ni suala la usalama wa ulimwengu.  (ANSA)

Turkson:Nchi kusini mwa dunia zipewe hati miliki ili ziweze kuzalisha chanjo zenyewe!

Nchi za kusini mwa dunia zinakosa hati miliki na ambayo inazuia kusambazwa kwa chanjo kwa njia hiyo Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu anasisitizia umuhimu wa kuwezeshwa utengenezaji wa Chanjo katika nchi za kusini wa dunia na kuhimiza utumiaji wa tiba asili ili kutibu virusi.Ni katika muktadha wa Siku ya Wagonjwa duniani sambamba na sikukuu ya Bikira Maria wa Lourdes tarehe 11 Februari.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Katika fursa ya Siku ya Wagonjwa Duniani, sambamba na siku kuu kiliturujia ya Bikira Maria wa Lourdes inayoadhimishwa kila tarehe 11 Februari ya kila mwaka, Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu ametoa maoni yake juu ya kampeni ya chanjo inayoendelea. Kwa mujibu wa Kardinali anasema: “Sasa, wasiwasi huo pia umehusishwa na ubora wa chanjo kwa sababu bidhaa kutoka China, Urusi, India zinawasili katika sehemu tofauti za ulimwengu ambazo zina mashaka juu ya ufanisi wao”.  Mkuu Baraza la Kipapa la  Hudum ya Maendeleo ya Binadamu anatafakari  hali halisi ya nchi zilizo katika mazingira magumu zaidi na kusema “Ulimwengu wa kusini unaelekeza kichwa chake kaskazini ili kupata chanjo, ukipuuza kwamba unaweza kuzalisha chanjo moja kwa moja wao wenyewe huko waliko”.

Mfumo huu sio endelevu tena, anaongeza Kardinali anayehimiza mashirika ya kimataifa kuingilia kati, akianza na Baraza la Usalama la (UN) kufuatia wito wa hivi karibuni uliozinduliwa pamoja na rais wa Caritas Internationalis, Kardinali Luis Antonio Tagle. “Wakati umefika kwa Jumba la Kioo kuchukua jukumu lake kwani sasa ni wazi kuwa ni suala la usalama wa ulimwengu. Lakini Shirika la Biashara Ulimwenguni linaweza pia kufanya sehemu yake ya kulegeza matundu ya miliki inayohusiana na uzalishaji wa chanjo. Mazoezi haya yanawakilisha kikwazo kwa utengenezaji wa chanjo katika nchi nyingine isipokuwa zile ambazo zina hati milki.

Kardinali anayo matumaini na  Afrika yake. Katika nchi tofauti za bara amesema kuna maabara yenye uwezo wa kuweka chanjo hiyo katika mzunguko, na kuwezesha upatikanaji wa kila wakati unaombwa na Papa Francisko. Lakini hiyo sio yote. Pia kuna hali halisi inayotumika mbele ya tiba asili ambayo inaweza kusaidia kutibu virusi. Kardinali Turkson ametaja hasa kisa cha Senegal ambapo dawa kama hiyo imekuwa ikipewa kwa maelfu ya watu. Hakuna vifo, alibainisha, akikumbuka hata huko Ujerumani kwamba kuna majengo ambayo yanahusika katika suala hilo.  Kwa hiyo amethibitisha: “Tupo tunaangalia ikiwa inawezekana kuagiza bidhaa hizo kuzipeleka katika nchi ambazo chanjo haitafika kwa muda mfupi”.

10 February 2021, 16:57