Tafuta

Vatican News
2021.02.26 Kardinali Cantalamessa wakati wa mahubiri yake 2021.02.26 Kardinali Cantalamessa wakati wa mahubiri yake 

Tafakari za kipindi cha Kwaresima 2021:tubuni&kuiamini Injili

Katika tafakari ya kwanza ya ya Kipindi cha Kwaresima 2021,Kardinali Cantalamessa Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa amejikita kufafanua mada ya tubuni na kuiamini Injili:Uongofu wa kwanza ni ule ambao ulihubiriwa na Yesu katika maneno hayo(Mk 1,15),Hatua ya pili kwenye Injili ni Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama watoto.Tatu inapatikana katika kitabu cha Ufunuo.Wewe si wa baridi na wala wa uvuguvugu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Katika tafakari ya kwanza ya Kwaresima 2021, Kardinali Padre Raniero Cantalamessa(OFMcap) mhubiri wa nyumba ya kipapa, Ijumaa tarehe 26 Februari 2021, amejikita na tafakari hiyo kwa kuongozwa na kauli mbiu “Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni na kuiamini Injili”.(Mk 1,15). Kardinali amesema kuwa katika utangulizi wa kwaresima kabla ya kuingia rasmi kwenye mada maalam ya mpango mzima wa kwaresima, Injili ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresima ya mwaka B, imesikika na tangazo la Mpango wa Yesu wakati anaanza kutoa huduma yake kwa umma.  Wito huo wa Kristo daima umekuwa na mwendelezo hata sasa. Kuhusu suala la kutubu, Kardinali amezungumzia vipindi vitatu au mantiki tatu tofauti za Agano Jipya. "Hii inaweka mawazo mara moja katika mwanga mpya" amesisitiza. Katika hatua kwa hatua inawezekana kupata ukamilifu na nini maana ya mchakato wa safari ya kiinjili. Siyo lazima kuzifanyaa uzoefu zote na kwa uzito wake. Kwa maana kuna uongofu kwa kila kipindi cha maisha, jambo muhimu ni kwamba kila moja anaweza kugundua kuwa anao wakati wake wa kutubu,ameshauri.

Tubuni maana yake ni amini

Uongofu wa kwanza ni iliohubiriwa na Yesu katika maneno “ tubuni na kuamini Injili ( Mk 1,15). Je ina maana gani ya neno kutubu? Kabla ya Yesu, neno hilo lilikuwa lina maana ya kurudi nyuma (katika neno la kiyahudi shub, kugeuza dira, kurudi katika hatua zako. Ilikuwa inaamanisha kwa yule ambaye kwa namna fulani ya maisha yake anajikuta yuko nje ya barabara. Na hivyo ni mwaliko wa kusimama na kutafakari, kuamua kufuata sheria na kungia tena katika uhusiano na Mungu. Uongofu katika kesi kama hiyo ilikuwa na maana msingi kimaadili na kushauri wazo muhimu  la kutimiza kwa mfano: kubadili mtindo na kuacha kufanya hili na lile. Lakini kaatika maneno ya Yesu, maana hiyo inabadilika. Si kwamba yeye anafurahi kubadilisha maana hiyo katika maneno, bali kwa sababu ya ujio wake wa kubadilisha mambo. “Wakati umetimia  na Ufalme wa Mungu umekaribia!”. Tubuni haina maana ya kurudi nyuma tena kama ilivyokuwa ya zamani na kushikilia sheria, bali ni kupiga hatua mbele ya kuingia katika Ufalme ili kupata wokovu ambao umefika kwa watu bure, kuwakomboa na ulioanzishwa na Mungu. Tubuni na kuamini Injili haina maana mbili tofauti na mwendelezo huo lakini ni tendo msingi, la “Prima conversio fit per fidem”, ya kuwa “Uongofu wa kwanza ni ule wa kuamini”, aliandika Mtakatifu  Thomas wa Aquinas. Yote hayo yanahitaji uongofu wa kweli, wa kubadilika kwa kina kwa namna ya kutambua ule uhusiano wetu na Mungu. Unahitaji kutoka katika wazo la Mungu ambaye anataka, anapanga, ni hatari hadi kufikia wazo la Mungu anayekuja na mikono iliyojaa ili aweze kutupatia yote. Ni uongofu kutoka katika sheria na kufikia neema ambayo ilikuwa moyoni sana mwa Mtakatifu Paulo.

Msipoongoka na kuwa kama watoto

Hatua ya pili kwenye Injili ambayo inarudia kuzungumza uongofu Kardinali amesema ni pale ambapo kwenye Injili inasema: “Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”(Mt 18,1-3). Kwa mara hii, Kardinali Cantalamessa  amesema ndiyo maana ya uongofu wa kurudi nyuma hasa ule wa kuwa kama watoto. Ndiyo uongofu wa yule ambaye anaingia tayari katika ufalme, ameamaini Injili kwa maana ni katika wakati wa kutoa huduma ya Kristo. Hayo yote yalitokana na mazungumzo ya mitume wakibishania juu ya ni nani atakuwa mkubwa. Huo ulikuwa ni wasi wasi wa kupata nafasi, ambayo si ile ya ufalme, bali ya ubinafsi, ya umimi. Kwa maana nyingine ya kuwa na jina. Kardinali Cantalamessa ametoa mfano Petro alikuwa amepata ahadi ya ukuu, Yuda alikuwa anatunza hazina. Matayo angeweza kusema kuwa alikuwa ameacha wengine, Andrea ambaye alikuwa amemfuata akiwa wa kwanza, Yakobo na Yohane walikwenda naye mlimani Tabor…

Matunda ya hali hii ni dhahiri kwa maana ya mashindano, tuhuma, makabiliano, kuchanganyikiwa na kushuku. Yesu mara moja aliwafunua kitambaa. Badala ya kuwa wa kwanza, kwa hakika hawawezi kuingia. Je ni kufanya nini? Ni kutubu, kubadilisha kabisha matarajio na mwelekeo. Ule ambao Yesu alioelekeza ni mapinduzi ya kweli.  Lazima tujiondoe ndani yetu binafsi na tujikite tena kwa Kristo. Yesu anazungumza kwa urahisi zaidi juu ya kuwa mtoto. Kurudia utoto, kwa mitume, ilimaanisha kurudi jinsi walivyokuwa wakati ule wa kuittwa wakiwa  kwenye mwambao wa ziwa bila kujidai, bila majina, bila kulinganisha kati yao, bila wivu, bila ushindani. Utajiri ulikuwa  katika ahadi tu  ya “ Nitawafanya wavuvi wa watu” na uwepo, wa Yesu. Kurudi wakati wa nyuma ambapo walikuwa bado ni marafiki katika mchakato wa safari, na sio washindani wa nafa si za kwanza.  Kwa ushauri Kardinali Cantalamessa amesema hata kwetu sisi kurudi kuwa watoto kunamaanisha kurudi  wakati ambao tuligundua kwamba tuliitwa, wakati ule ambao ulikuwa wa kuwekwa wakfu wa ukuhani, wakati wa kufunga nadhiri za kitawa au mkutano wa kwanza binafsi na Yesu. Wakati tuliposema: “Mungu peke yake anatosha!" na tulikuwa tunaamini.

Wewe si wa baridi na wala wa moto

Kardinali Cantalamesa akifafanua mantiki ya tatu yenye mwaliko wa uongofu ambayo inapatikana katika barua saba za Makanisa kwenye kitabu cha Ufunuo. Barua saba zinawalenga watuna jumuiya kama sisi tunavyoishi katika kipindi cha kikristo, ambacho kinajikita katika nafasi ya uongozi.  Barua hizo ni kwa malaika mbali mbali wa makanisa mbalimbali. Kwa Malaika wa Kanisa mbalo ni Efeso. Roho Mtakatifu ajitambulishi na Malaika wahusika wa makosa na wanaokosea njia ambazo zimethibitishwa katika makanisa lakini ni mwaliko wa kuwa na uongofu kwa malaika badala ya watu. Katika barua saba za Ufunuo , ya kutafakari zaidi ni barua ya Kanisa la Laodicea isemayo: “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala uvuguvugu; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au uvuguvugu”. (Uf: 3, 15...). Hapa ni kubainisha juu ya uongofu wa ubadilishaji kutokana na unafiki na uvuguvugu ili kuwa na  bidii ya roho. Katika historia ya kikirsto mfano maarufu wa uongofu ni ule wa dhambi hadi neema kwa Mtakatifu Agostino. Mfano wa kufundisha zaidi wa uongofu wa pili, kuhusu kutoka katika uvuguvugu kwenda katika bidii ya kiroho, ni wa Mtakatifu Teresa wa Avila. Anachosema juu yake katika Maisha,  hakika anaweka chumvi na dhamira ya dhamiri yake, lakini, kwa hali yoyote, inaweza kusaidia hata sisi sote kufanya uchunguzi mzuri wa dhamiri amesahuri Kardinali.

Matokeo ya roho ya kina ya ukosefu wa furaha

Mtakatifu Teresa alindika: “Nilikuwa naanguka  na kuamka, nilikuwa nikamka vibaya sana hadi ninaanguka tena. Nilikuwa mdhaifu kabisa katika ukamilifu kiasi  kwamba hata sikuhesabu dhambi za kifo na sikuogopa kama vile nilipaswa kuwa, kwa sababu sikuepuka hatari hizo. Ninaweza kusema kuwa maisha yangu yalikuwa ya uchungu zaidi ya kufikiria, kwa sababu sikumfurahishaa Mungu, wala sikujisikia furaha ya ulimwengu. Wakati nilikuwa katika burudani za ulimwengu, mawazo ya kile nilichokuwa na deni kwa Mungu kilinifanya nitumie kwa maumivu; na wakati nilikuwa na Mungu, mapenzi ya ulimwengu yalikuwa yanarudi kunisumbua”. Kardinali amesema "Wengi wetu wanaweza kugundua matokea hayo ya kweli ya sababu ya kutotosheka kwake na kutokuwa na furaha. Ni kuzungumza juu ya uongofu kutoka katika uvuguvugu. Mtakatifu Paulo alikuwa anawashauri. Sisi tunaweza tatatibu kuangukia katika ubaridi kama mchanga unavyoanguka na hatuwezi kujiamsha peke yetu. Maisha ya Kikristo yaliyojaa juhudi za kujinyima lakini bila mguso wa  Roho, ingefanana, kama alivyosema baba wa zamani, kuwa Misa ambayo wangesoma masomo mengi, wangeteleza ibada zota na matoleo mengi lakini katika ambayo yasingewekwa wakfu kwa upande wa kuhani na yote yangesalia  jinsi yalivyo.

Joto la roho kutoa chachu kwa mitume

Ubatizo katika Roho umeonesha kwa urahisi katikati na nguvu ya kupyaisha maisha ya milioni ya waamini katika Makanisa yote ya Kikristo. Si kwa bahati mbaya watu ambao walikuwa wakristo kwa jina tu, na neema ya uzoefu huo wamegeuka kuwa wakristo wa kweli wanaojikita katika sala na sifa, katika sakramenti, uinjilishaiji hai  na utayari wa kufanya majukumu ya kichungaji katika parokia. Ni uongofu wa kweli kutoka katika uvuvugu hadi joto la kweli. Ni sababu ya kusema ndani mwetu kama alivyokuwa akirudia Mtakatifu Agostino wakati akisikiliza historia za wanaume na wanawake ambao katika wakati wake walikuwa wanaacha dunia na kumfuata Mungu “Si isti et istae, cur non ego?, yaani  “Ikiwa wameweza wanaume na wanawake hao, je mimi siwezi”. Kwa kuhitimisha amesema tumwombe Mama wa Mungu ambaye atuombee neema kutoka kwa Mwanae kuanzia Kanisa la Galilaya. Kwa njia ya maombezi yake, katika fursa ya maji yalivyogeuka kuwa divai. Tumwombe kwa maombezi ya maji ya uvuguvugu wetu upate uongofu katika divai ya kupyaishwa. Mvinyo ambao wakati wa Pentekoste ulitoa chachu kwa mitume wakalewa ulevi wa Roho na kuwafanya wawe wachangamfu katika Roho.

26 February 2021, 14:18