Tafuta

Vatican News
2021.02.24 SIKU YA KIMATAIFA YA MAGONJWA NADRA TAREHE 28 FEBRUARI 2021.02.24 SIKU YA KIMATAIFA YA MAGONJWA NADRA TAREHE 28 FEBRUARI 

Siku ya magonjwa nadra:Hospitali ya Vatican yagundua magonjwa 4 mapya!

Katika siku ya tukio la Siku ya magonjwa nadara kimataifa,tarehe 28 Februari,chumba cha dharura cha hospitali ya Vatican,Bambino Gesu kitawashwa mwanga kwa lengo la kuonesha hali halisi ya magonjwa nadra kuwa yanaweza kutibiwa mapema ikiwa utafiti inafanyika mapema kwa njia ya teknolojia mpya.Mwaka 2020 wamegundua magonjwa nadra 13.Lengo ni kutaka kufanya uchunguzi zaidi katika familia na kupata data badala ya wagonjwa.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Jumapili, tarehe 28 Februari, ukumbi wa chumba cha dharura huko Hospitali cha Bambino Gesù, Roma, kitaangazwa na maandishi kwa neno “cu-RARE”, yaani “kutibu”,  wakati wa Siku ya Kimataifa  ya magonjwa Nadra, sekta ambayo hospitali ya Vatican  inahusika sana pia katika kipindi hiki cha janga. Mwaka 2020 wamegundua magonjwa mapya nadra 13. Lengo ni kupunguza janga hili katika uchunguzi wa familia na kupata data badala ya wagonjwa. Kiukweli, ni aina nne zilizotambuliwa hivi karibuni katika miezi miwili iliyopita ambazo zimefanya uwezekano wa kugundua magonjwa mengi meni ambayo uchunguzi wake haujulikani bado hadi sasa. Haya ni mabadiliko katika magonjwa nadra ambayo huathiri ukuaji wa mifupa ya watoto na magonjwa mengine matatu ya ugonjwa wa neva, ambayo ni pamoja na aina nyingine za magonjwa 13 zilizoainishwa mnamo 2020.

Utafiti huu uliwezeshwa shukrani kwa mpango wa utafiti wa hospitali uliowekwa kwa wagonjwa wanaougua magonjwa “yasiyo na  jina”, na ambayo uliofadhiliwa na Mfuko wa “Vite Coraggiose”,  usio wa Kiserikali wa  Bambino Gesù na Wizara ya Afya ya Italia. Tangu 2015, uendekeshwa katika hospitali hiyo wa mpango wa kusaidia watoto yatima na wengine ambao wanagunduluwa kuwa na magonjwa nadra na kutoa matokeo ya utambuzi mapema kwa magonjwa nadra au ambayo hayana jina na sababu inayotambulisha ugonjwa huo, kuchambua idadi kubwa ya data, kwa kutumia teknolojia mpya za ufuatiliaji.

Kwa maelezo ya  Marco Tartaglia, mkuu wa eneo la Utafiti wa Magonjwa ya Vinasaba na Magonjwa nadra na mratibu wa tafiti hizi, amesema ndio mahali pa kuanza kwa kila mgonjwa kwa matibabu maalum, kuanzia tiba zilizolengwa wakati zinapatikana, kwa ushauri wa maumbile unaofaa kwa familia. Kuwa na fursa ya kupima  unaolenga watoto wanaougua ugonjwa nadra, hata ule ambao haujulikani kufika hivi karibuni, ni fursa nzuri kwa wagonjwa na familia zao. Ujuzi wa matokeo ya mabadiliko yaliyopo katika aina hizi mpya na athari zao za kliniki zimewawezesha leo kuwapa zana bora ya uchunguzi na kuanzisha njia za kujitoa kufikia malengo tiba sahihi.

Kwa zaidi ya miaka 7 iliyopita, mpango wa Hospitali ya Bambino Gesu uliowekwa kwa ajili ya wagonjwa wanaougua magonjwa nadra na yatima, na ambao umewezesha kutambua aina hizi mpya za magonjwa hamsini na kuainisha au kuorodhesha magonjwa kadhaa mapya. Hospitali ya watoto ya Bambino Gesù pia inasimamia safu zaidi ya kitaifa za wagonjwa nadra katika umri wa watoto (zaidi ya wagonjwa 15,000). Tangu 2016 imezindua kliniki maalum iliyowekwa kwa wagonjwa nadra bila uchunguzi ambapo uchambuzi zaidi ya 40,000 umefanywa katika mwaka 2020.

26 February 2021, 16:29