Tafuta

Vatican News
2020.10.02 MWENYE HERI CARLO ACUTIS 2020.10.02 MWENYE HERI CARLO ACUTIS   (Credits Diocesi di Assisi - Nocera Umbra - Gualdo Tadino)

Semeraro:Historia ya utakatifu wa mwenyeheri Carlo Acutis inakua

Rais wa Baraza la Kipapa la mchakato wa kuwatangaza wenyeheri na Watakatifu anasisitiza juu ya karama ya kijana gwiji wa Inteneti Carlo Acustis katika fursa ya toleo jipya la usasishaji wa historia yake iliyochapishwa na Duka la Vitabu Vatican na kichwa cha habari “kutoka teknolojia ya intaneti hadi mbinguni”.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kutoka teknolojia ya intaneti hadi mbingu.Carlo Acutis ni toleo jipya la kitabu lililosasishwa na ambalo lina utajiri  mkubwa wa historia ya Mwenyeheri Carlo Acustis, kitabu chenye kurasa 216 ambacho kilikuwa kinapatikana tayari kwenye Duka la Vitabu Vatican, tangu mwaka 2016 kikiwa na kichwa: “Gwiji wa teknolojia mbinguni. Historia ya Mtumishi wa Mungu Carlo Acutis”. Kitabu hicho kimeingizwa ndani ya safu za ushuhuda ambao tayari ulikuwa na utangulizi mpya wa  Monsinyo Dario Edoardo Viganò na utangulizi mpya uliotiwa saini na Nicola Gori, mwandishi na msimamizi wa mchakato wa utangazwaji wa mwenyeheri Carlo Acuts, uliopyaishwa katika hali ya sasa ya mchakato kwa mtazamo wa Utangazwaji wake wa utakatifu. Mpango huo mpya wa uhariri ni kwa ushirikiano kati ya Duka la Vitabu Vatican na VatiVision (www.vativision.com).

Carlo Acutis, ni kijana wa miaka 15 ambaye ni gwiji wa  Intaneti, ametangazwa kuwa mwenyeheri hii karibuni tarehe 10 Oktoba 2020, kifo chake kilimjia manmo 2006 baada ya kuishi utoto na ujana huku akiongozwa  na neema ya Mungu. Tangu mwanzo alikuwa na neema ya zawadi ya kuingia katika uhusiano na watu wengi na alikuwa ameeleweka kama mfano wa wenzake. Alikuwa anaona katika intaneti kama sehemu ya  Unjilishaji  wa Injili na katekesi na yeye mwenyewe aliweka uwezo wake wa kiteknolojia katika huduma ya Injili na Kanisa akimpeleka Yesu kwa njia ya Intaneti na mitandao ya kijamii, kati ya wenzake na wale ambao waliishi wakiwasiliana naye.

Katika maisha yake aliishi kwa sala, maana ya utume, upendo kwa Bikira Maria na Ekaristi ya kila siku. Katika Wosia wa Kitume baada ya Sinodi wa “Christus vivit” wa 25 Machi 2020, Papa Francisko alipendekeza Carlo kwa vijana  awe  mfano wa utakatifu katika wakati wa kidijitali. Ujumbe unaofaha wa Carlo kama anavyosisitiza,Nicola Gori katika dibaji ya toleo jipya, imethibitishwa na Kanisa wakati tarehe 10 Oktoba 2020 alipotangazwa kuwa mwenyeheri katika Kanisa Kuu la takatifu Francis wa Assisi(uk.27). Uwepo wake kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu hicho, anasema kuwa unatufundisha kuwa utakatifu hauna umri na kwamba inawezekana kwa wote na kila tamaduni yoyote ( uk.35), uzao, asili na lugha. Tarehe 19 Machi Papa Francisko atazindua “Mwaka wa Familia wa Amoris Latitiae”, utakaohitimishwa tarehe 26 Juni 2022, na “kutoka katika Tekonolojia ya intaneti hadi mbinguni” ni kitabu kinachoelekeza vijana wote na familia ili kukua pamoja, kwa kuacha waigek arama na sura ya kijana kama Carlo Acutis.

Katika mahojiano ya Vatican news  na Kardinali Marcello Semeraro Rais wa Baraa la kipapa la mchakato wa kuwatangaza watakatifu kuhusiana na kitabu cha “ kutoka teknolijia hadi mbinguni. Carlo Acutis”, anasema siyo mantiki ya uhariri, badala yake ni kusisitiza hali halli halisi ya utakatifu wa kijana huyo ambaye hakuna shaka kuwa umeongezeka. Kardinali anathibitisha kuwa umaarufu huu unazidi ukubwa wa eneo hilo na kuwa na  uhakika kwamba ameugusa kwa mkono wake huko Assisi, wakati wa sherehe ya kufungwa kwa kaburi la kijana ambalo lilibaki wazi kwa siku kadhaa ndani ya Madhabahui ya kuvuliwa kwa mtakatifu Francis huko Assisi (Spoliation). Siku zilizooneshwa kwa ukina wa ibada kubwa maarufu, na kuangazia idadi kubwa ya watu waliotoka Italia yote. Kuwa msimamizi hautajiki kuwa mtaalam wa somo hili kwa maana ya karibu sana. Carlo (Charles) alikuwa na umahiri wa ajabu, lakini alitumia njia hizi kueneza Injili na maarifa ya Ekaristi. Hadi kufikia kwamba  hata Papa Francisko akizungumza mara nyingi na vijana, ametaja mwenendo wake kama mfano wa kufuata. Msimamizi ni mtu ambaye ameishi uhusiano na vyombo hivi kwa njia ya kawaida na hasa juu ya njia sahihi kutokana na  mtazamo wa maadili”, amefafanua Kardinali Semeraro.

Kwanza, kabisa  kutangazwa mtakatifu ni muhimu, na ambapo utambuzi wa muujiza unahitajika kupitia maombezi ya Carlo (Charles). Kazi inayohitaji jukumu mwendesha mchakato huo, ambaye amezingatia huko Amerika Kusini kutokana na kwamba, ripoti za miujiza zinaendelea kutoka huko. Kwa wakati huu, dharura ya kiafya inafanya kuwa ngumu wa kuondoka mahali fulani kwenda na kukutana uso kwa uso, ambapo ndiyo njia muhimu katika  kukusanya ushuhuda  na maoni. Walakini, Kardinali Semeraro amesisitiza kuwa jukumu la msimamizi wa mchakato sio kukusanya kesi zote, bali ni kutambua na kung’amua ile ambayo kweli inauwezekano wa kushinda hatua mbalimbali. Kwa njia hiyo  ameeleza kuwa mchakato ​​ambayo hufanyika kwanza  ni katika kiwango cha ushauri wa matibabu na baadaye kwa ushauri wa wataalimungu ambapo unathibitishwa ikiwa kumekuwa na maombezi ya kweli ya mwenyeheri  na ikiwa hii ilielekezwa kwake tu na kwa maana hiyo ikiwa kuna sababu na uhusiano wa matokeo, ingawa sio kwa maneno ya kihesabu tu.

26 February 2021, 17:04