Tafuta

Vatican News
2021.02.12 Paolo Ruffini,rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, tarehe 12  Februari  katika kilele cha miaka 90 ya Radio Vatican. 2021.02.12 Paolo Ruffini,rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, tarehe 12 Februari katika kilele cha miaka 90 ya Radio Vatican.  Tahariri

Ruffini:radio inahitaji umakini wa kutoa sauti kwa wasio kuwa nayo!

Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano anaangazia hatua muhimu ya miaka 90 ya Radio ya Vatica na juu ya nguvu ya chombo ambacho hakina haraka. Katika ulimwengu wa leo ulioungana,anasema,utajiri wa mtangazaji huyo uko katika umakini kwa watu wasio na sauti,hali zilizosahaulika,kuheshimu wingi wa tamaduni na maoni.

Na Sr. Agela Rwezaula – Vatican.

Katika kilele cha Siku ya kuadhimisha miala 90 ya utume wa Radio Vatican, tarehe 12 Februario 2021, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Bwana Paulo Ruffini ameweza kujikita kuangazia kwa dhati umuhimu wa utume wa Radio, kuhusu zana hii ambayo nasema haina hara, bali unahitaji umakini na vile vile mpango mpya  wa radio katika tovuti. Yafuatayo ni maelezo ya Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika kilele hicho:

Radio Vatican inafikisha miaka 90 leo hii. Maadhimisho daima ni wakati wa kupima na kupanga. Kufanya kumbu kumbu ni vizuri kwetu, kwa sababu ni kuweka uhai kwa yaliyopita  na kunaweza kujengwa vitu vingine vipya ambavyo havijengwi juu ya mchanga. Historia yetu, hadithi zetu, ndio misingi yetu. Kufanya kumbu kumbu kwetu ni vizuri,  kwa sababu ni kwa njia hii tu tunaweza kufuata dira bila kuangukia kwenye mtego wa wale ambao (kama alivyosema Kierkegaard) hubadilishana orodha ya chakula cha siku. Kukumbuka kwa upande mmoja kunamaanisha kuimarisha utajiri wa zamani na kwa upande mwingine kutengeneza siku za usoni. Utajiri wa Radio ya Vatican tunayoisherehekea leo hii ni uwazi wake kwa ulimwengu, tofauti sana lakini kwa namna ya  kipekee, umoja, unaoiunganisha. Ni ukatoliki kwa maana halisi ya neno. Tabia yake iliyo nayo ni ufahamu, ulioandikwa katika vinasaba vyake (DNA) ya kuwa jamuiya kubwa ya kimataifa, yenye tamaduni nyingi; ikiunganishwa na kuwa katika huduma ya utume wa Papa, na jukumu la kupeleka neno lake ulimwenguni, katika lugha za ulimwengu.

Umakini kwa wasio kuwa na sauti

Ni mamlaka, utambulisho unaofafanuliwa vizuri, kuwa hatua ya kumbukumbu. Ni umakini kwa wasio na sauti, katika hali zilizosahaulika, kuheshimu wingi wa tamaduni na maoni.  Baba Mtakatifu Francisko mara nyingi anarudia kusema kuwa imani  hupitishwa kwa  njia ya lugha. Radio Vatican inazungumza kweli kama Mtakatifu Paulo VI alivyo tuhimiza tujifanye kama lugha ya msikilizaji. Ni mtangazaji wa kimataifa anayezungumza lugha zaidi (41), ulimwenguni akihifadhi lugha yake ya kidigitali kutoka katika majukwaa ya mawasiliano bila kina. Huu ndio mpaka wake. Leo tunaweza kuridhika na dhana ya kiteknolojia, au tunaweza kujaribu kujenga ulimwengu zaidi kwa kiwango cha kibinadamu kupitia mawasiliano. Inawezekana kuridhika na unganisho tasa; au unaweza kutafuta mawasiliano ya kweli. Unaweza kuamini mazungumzo ya dhati ambayo hupelekea kushirikisha, au katika biashara ya maoni na itikadi. Kwa maana hii, mtindo wa radio unaweza kuwa kipimo. Radio ni shule nzuri ya uandishi wa habari. Inajua jinsi ya kutumia maneno sahihi. Inajua jinsi ya kuchanganya mwangaza ulio tayari na tafakari. Kwa maana hii, wakati wa kidigitali hauleti mwisho wa radio. Badala yake ni kinyume kabisa.

Kuanzishwa radio ya tovuti katika vipindi vya radio Vatican

Mpango ambao unaoanza leo hii  wa radio ya tovuti inabadilisha vipindi vyetu, kwa lugha tofauti, kuwa radio halisi, kila moja ikiwa na ratiba yake. Na hufanya kila smartphone kuwa redio ndogo. Shukrani kwa teknolojia mpya, radio, pamoja na kubaki kuwa njia yenye ufafanuzi mdogo, imekamilisha uwezo wake wa kufikia kila mtu, na kusimulia kwa kina. Lakini haikatai uwepo wake. Radio ni nzuri kwa sababu inaingia ndani mwako kwa kina, kwa sababu unasikia sauti. Na kuzingatia juu ya sauti. Radio haina haraka. Inahitaji umakini. Inaheshimu maneno, na kuacha izungumze. Mahali ambapo ustaarabu wa picha huishia kwa kutatanisha ukweli na simulizi za uwongo, radio haichukui eneo hilo, inasimulia juu yake. Haiundi tamasha bali inayatafuta. Hapa ndipo kuna haja ambayo tunahitaji neno kwa kina. Badhi ya picha nyingine hazina kivuli, unene, na inakosekana uwezo wa neno tupu. Tayari tunajua mafanikio ya podcast. Tumeona jinsi hata mitandao ya kijamii ya hivi karibuni inavyo tafuta  siri ya mwanzo mpya kwa neno lililonenwa. Neno linalozungumzwa na kusikia ni dawa yenye nguvu sana katika utelezi wa mauti ya uvivu wa televisheni. Mpaka wa Radio Vatican, kwa mtazamo wa habari inabaki kuwa msingi wa magistero  ya Papa na sanduku la hazina ya kumbukumbu ya pamoja. Ni kujenga na Petro, karibu na Petro, sio mnara wa Babeli lakini muungano wa mawe yaliyo hai, jengo la mawe yaliyo hai (taz. 1 Pt 2,5).

Kazi ya radio; sauti yake yaeneo katika nchi nzima

Kazi yake ni ile iliyoelezwa na Mtakatifu Paulo katika barua kwa Warumi: “Sauti yao imeenea ulimwenguni kote, na maneno yao hata miisho ya ulimwengu” (Rum 10,18). Shauku yake nyepesi ni kuwafanya wengi wanaomfuata wajisikie na kuna mamilioni leo hii pia kupitia tovuti na mitandao ya kijamii, wahusika wakuu wa historia hiyo ambayo ni historia inafanywa nao na ambayo inahitaji uelewa wa Kikristo ili kueleweka. Kwa kifupi, kuwashirikisha badala ya kuwaacha wawe watazamaji tu. Lengo lake  baadaye sio kugeuka kuwa mkanganiko wa  maoni mazuri, au kukuza tamaa na matokeo ya haraka, lakini pia sio kuangukia katika jaribio la kufikiria kuwa  na chaguo. Ni kutamani (zaidi ya wingi wa wasikilizaji) kuendelea kuwa hatua ya kumbukumbu, inayoweza kutoa maswali, kutikisa dhamiri, kushangaza, kutafuta ushiriki wa kweli, na muungano. Ni  kutoka katika mantiki ya usambazaji kwenda katika  ule wa uhusiano; Ni kutoka katika sehemu za katikati ili  kuruhusu sehemu za  pembezoni zizungumze kutoka katika asili ya habari za Vatican, kujenga mtandao uwenye  Neno kama msingi wake.

15 February 2021, 16:15