Tafuta

Vatican News

Parolin:Radio Vatican ni ufunguzi wazi&wito wake kwa ulimwengu

Katika maadhimisho ya Misa ya Kumbu kumbu ya miaka 90 ya kuzaliwa kwa Radio Vatican,Kardinali Pietro Prolin katibu wa Vatican ameongoza misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Katika mahubiri yake amesisitizia juu ya ufunguzi kwa ulimwengu na mawasiliano ya maisha halisi ya watu,kama miongozo ya utume unaoendelea na kujipyaisha kila wakati.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Uwakilishi mdogo kutokana na janga la sasa, wa wafanyakazi wa Radio Vatican wameudhuria Misa Takatifu Ijumaa tarehe 12 Februari 2021 iliyoongozwa na Kardinali Pietro Parolin, kwa ushiriki wa  Kardinali Marceloo Semnerao, Rais wa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza wenyeheri na Watakatifu, Mosninyo Adriano Ruiz, Katibu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na  Padre Federico Lombardi, aliywahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Radio Vatican na idadi kubwa ya mapadre wa Jumuiya ya kazi ya utangazaji wa kipapa, ambao wamejumuika wote katika Kanisa kuu la Mkatifu Petro, kwenye  fursa ya kuadhimisha Miaka 90 ya utume wa Utangazi wa Radio Vatican ulimwenguni kote.

Katika mahubiri yake Kardinali  Parolin amesisitiza juu ya ufunguzi mpana kwa ulimwengu na mawasiliano katika maisha halisi ya watu, kama  miongozo muhimu ya utume unaoendelea  na kujipyaisha kila wakati. Aidha pendekezo la pili ni kuhusu ulimwengu wote ambapo amekumbusha historia ya  Radio Vatican ilivyoundwa na mtandao mkubwa  ambao umeenea mahali popote katika ulimwengu wa Kanisa Katoliki na huduma ya Kipapa. Na zaidi imewafanya watu wa mbali kusali kwa pamoja. Kwa maana hiyo ni uthibitisho wa neno la kisasa la Pentekoste ya zamani ambayo imejikita katika ndimi nyingi kwa watu wengi kama  ishara ya Roho  ambayo wote wanafikiwa na kuunganika,.

Neno la tatu ambalo  Kardinali amependa kusisitiza kutokana na Injili ya mawasiliano ni kuwasiliana. Radio Vatican, wakati wa vita ya pili vya  dunia, amesma ilikuwa kama mkono hai, katika Ofisi ya Habari ya Sekretarieti Vatican, ambayo iliundwa kwa ajili ya kuweza kuwatafuta na kuwasiliano na familia zilizokuwa zimepotea na wafungwa. Waliweza kuunda mtandao wa mshikamano hadi kueneza kufikia milioni moja ya ujumbe na kuwaunganisha watu wengi na wapendwa wao. Mawasiliano yanahusu kuwasiliana moja kwa moja  na ni njia  moja ambayo kama  Baba Mtakatifu alivyokumbusha  katika ujumbe wa mwisho wa Siku ya Mawasiliano Duniani, akiangazia umuhimu wa kuwasiliana kwa njia ya kukutana na watu mahali na jinsi walivyo, amekazia Kardinali. “Neno hilo kwa hakika ni muafaka tu ikiwa  unaona na  ikiwa tu linakuhusisha katika uzoefu na ikiwa linagusa tu katika maisha”. 

Kwa namna fulani Baraza la kipapa la mawasiliano linatimiza miaka 90

Katika hitimisho la Misa Takatifu naye Monsinyo Luiz  kwa niaba ya Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Dk. Ruffini na wote amemshukuru Kardinali Parolin kwa neno lake na kwa maadhimisho hayo ya miaka 90 katika huduma ya utangazaji wa Radio Vaticana. “Huu ni wakati uliojaa neema kwetu kama Barazala wakati wa maadhimisho kumbu kumbu na mipango: tulianza Jubilei  zetu mnamo Desemba 24, na maadhimisho ya miaka 25 ya Tovuti ya Vatican (www.vatican.va) ambayo inakusanya maandishi ya Magisterium ya Papa,na ambayo ilimaanisha kutua katika mtandao mkubwa wa Intenet. Leo tunaadhimisha miaka 90 ya Radio Vatican na, mnamo Julai, tutafanya kumbukumbu ya miaka 160 ya kuzaliwa kwa gazeti la Osservatore Romano”.

Akiendelea kufafanua amesema  mosninyori Luiz amesema: “Kwa namna nyingine hata sisi Baraza la Kipapa la Mawasiliano iliyoundwa na Baba Mtakatifu Francisko, leo kwa njia fulani tunatimiza miaka 90. Kwa kuwa na jukumu la huduma na utume wa Radio Vatican, tunakuwa na msukumo mpya wa kimisionari, kwa sababu tunahitaji kujibu muktadha wa kitamaduni ambao mtu na kwa maana hiyo Kanisa, kutembea leo hii. Katika harambee ya muunganiko wa vyombo vya habari vyote, ambao ni mfano wa utamaduni huu wa digitali, utume umeajirishwa na kuzinduliwa tena!

Na hatimaye ameshukuru tena kwamba “Asante tena, kwa maadhimisho haya! Katika fursa ya wimbo wetu wa sifa, tunaelewa na kueleza uaminifu wetu kwa Baba Mtakatifu na kwa Kanisa, shauku yetu kama utume na upendo wetu kwa yule Mfufuka ambaye anatutuma kutangaza Injili hadi miisho ya Dunia”.

12 February 2021, 17:00