Tafuta

Kampeni ya Chanjo dhidi ya Covid-19 inaendelea Kampeni ya Chanjo dhidi ya Covid-19 inaendelea 

Mons.Jurkovič:lazima kuhakikisha hupatikanaji wa chanjo ya Covid-19 ulimwenguni kote

Kuondoa vizuizi kwenye haki miliki ambavyo vinazuia ufikiaji wa chanjo ya Covid-19, ndiyo maombi ya askofu Mkuu Ivan Jurkovič,Mwakilishi wa Kudumu wa wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva,ambaye amezungumza katika kikao cha Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO).

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu Ivan  Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu wa wa Vatican katika ofisi za  Umoja wa Mataifa huko Geneva, akizungumza katika Baraza la Haki zinazohusiana na Haki Miliki (TRIPs) katika Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) amesema kuwa “wiki za mwisho tumeona jinsi nchi zingine na kampuni zinaendelea kupendelea makubaliano ya nchi mbili, kupandisha bei na kujaribu kuruka mstari” Hii imejitokeza  licha ya Baba Mtakatifu Francisko kuonya juu ya hatari ya kutoa kipaumbele cha kupata chanjo kwa walio matajiri. Kwa kuongezea, Mwakilishi wa Kudumu ameangazia jambo jinginge ambalo kwa upande mmoja, nchi nyingi ulimwenguni zinakabiliwa na ucheleweshaji wa mipango ya chanjo kwa sababu ya uzalishaji wake kuwa mdogo  na  kwa upande mwingine, kuna uzalishaji mwingi wenye uwezo wa kutoa chanjo salama na nzuri ambazo lakini haziwezi kufanya hivyo, kwa sababu ya kupata vizuizi vya haki miliki.

Chanjo zinapaswa kuzingatiwa kama wema wa umma

Kwa mujibu wa Vatican ikizingatia udharura wa chanjo hizi katika hali ya dharura ya kiafya, lakini pia pesa nyingi zilizowekezwa na Mataifa kwa maendeleo yao, zinapaswa kuzingatiwa kama wema wa umma ambayo kila mtu anapaswa kupata, bila ubaguzi, kwa misingi mali kwa wote akikimusha wito wa Papa Francisko.  Walakini mwakilishi huyo wa Kitume pia ameangazia njia ngumu za sasa za ulinzi halali wa haki miliki ambazo zinawakilisha kikwazo kwa maana hii. “Hata katika nyakati za kawaida utaratibu wa Kifungu cha 31kilichoongezwa cha Mkataba wa TRIPs, ulioanzishwa kusaidia nchi ambazo hazina uwezo wa kutosha wa utengenezaji wa dawa, umekosolewa sana kutokana na taratibu mbaya za taratibu zake, amebainisha, na kusisitiza kuwa “sera hizo na sheria zinapaswa kudumisha mtazamo unaozingatia kuheshimu na kuhamasisha  hadhi ya a binadamu, katika roho ya mshikamano ndani na kati ya mataifa”.

Kujitoa kwa nguvu kwa ajili ya wanadamu wote

Kufuatia na hayo ndipo ombi kutoka Vatican la kupunguzwa kutoka kwa utekelezwaji na  wa sehemu ya 1, 4, 5 na 7 ya sehemu ya pili ya makubaliano, ili kuzuia, au kutibu Covid-19. Uamuzi wa kutoa udhalilishaji huu utakuwa ishara ya nguvu ambayo itaonesha kujitoa kweli na kwa hivyo mapenzi ya kupitisha kutoka nadharia kwenda katika matendo kwa ajili ya masilahi ya familia nzima ya wanadamu, amehitimisha Askofu Mkuu Jurkovič.

24 February 2021, 15:29