Tafuta

Vatican News
 Papa Francisko wakati wa kukutana na Kiongozi wa Kanisa la Kiorthodox,wa Urusi ,Patriaki Kirill  mnamo tarehe 12 02 2016 2016. Papa Francisko wakati wa kukutana na Kiongozi wa Kanisa la Kiorthodox,wa Urusi ,Patriaki Kirill mnamo tarehe 12 02 2016 2016. 

Miaka mitano iliyopita mkutano wa kihistoria huko Cuba kati ya Papa na Patriaki Kirill

Tukio la kihistoria lililofanyika kwenye kisiwa cha Cuba lilikuwa ni kotovu cha Mkutano kwa njia ya mtandao ambapo wamejikita kujadili janga la sasa.Washiriki ni pamoja na Kardinali Kurt Koch,rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo,Askofu Mkuu Salvatore Fisichella,rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya na Metropolitani Hilarion wa Volokolamsk.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Mkutano kwa njia ya mtandao, ukiongozwa na mada “ Kanisa na janga:changamoto na matarajio, Kardinali Kurt Koch Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kristo ametoa hotuba yake kwa njia ya mtandao. Katika fursa ya mwaka wa tano wa kihistoria wa Mkutano kati ya Papa Francisko na Patriaki Kyrill katika uwanja wa ndege wa Havana nchini Cuba mnamo tarehe 12 Februari 2016 Kardinali Koch amesema anapenda kutoa salamu akianzia na Na mkuu wa kiorthodox Patriaki Hilarion, ambaye ni mwenyekiti wa Kitengo kwa ajili ya Mahusiano ya kiekumene, katika Kanisa katoliki, Askofu Mkuu Salvatore Fisichella, Rais wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaji mpya, anawashukuru kwa moyo wa kukubali kufanya mkutano huo kwa upande wa ukatoliki.

Kardinali amefafanua jinsi ambavyo kabla ya mkutano huo wa Papa Francisko na Patriaki Kyrill, walivyoamua huko Havana kufanya kumbu kumbu ya tukio hili kila mwaka ili kwa ajili ya umuhimu wa kihistoria. Na walipendekeza kuweka kiini cha tafakari, hatua kwa hatua juu ya Hati ya pamoja ambayo viongozi hao wawili wa Kanisa walitia saini. Katika fursa ya mwaka wa kwanza ilifanyika  katika Chuo kikuu cha Friburg nchini Uswisi, mkutano wao uliongozwa na mada ya mfungamano uliomo  katika hati hiyo ya pamoja. Katika fursa ya maadhimisho ya  Mwaka wa pili, iliyofanyika huko Vienna, chini ya mwaliko wa Kardinali Christoph Schönborn,  walijikita kutazama  juu ya umuhimu wa mada ya Wakristo wa Nchi za Mashariki na umoja wa kiekumene. Mwaka wa tatu, ulifanyika huko Moscow ambao uliunganishwa na Jukwaa la Kisayansi kuhusu matatizo ya Kitaalimungu na maadili ya Euthanasia. Na katika Mwaka wa nne ambao walifanyika jijini Roma, walitoa umakini wa “Uekuene wa watakatifu”.

Katika kuadhimisha mwaka wa tano ambao kwa maandilizi na uratibu umefanyika tena na upatriaki wa Kiorothodox huko Urusi, kwa sababu ya hali ya sasa ya ulimwengu uliozingirwa na mgogoro wa virusi vya corona amesema hawakuhitaji na wala kuangaika kutafuta mada kwa muda mrefu sana, kwa maana ya hali halisi. Kardinali Koch amesema “Janga la Covid-19 kwa hakika halipo ndani ya Hati ya pamoja iliyotiwa saini huko HaVana, kwa sababu hakuna ambaye angeweza kutengemea changamoto kama hii ya kidunia. Walakini kwa kuunganisha na janga yapo masuala mengi na matatizo ambayo yanakabiliwa katika hati hiyo ya pamoja. Kwa mfano sehemu ya kwanza inaonesha wazi matatizo yanayohusu jamii. Kiukweli janga limeweka mjadala mkubwa kwa mambo mengo yanayohusu hali hi ya mada ya pamja.

Kwanza, shida zinazohusiana na mshikamano wa kijamii hujitokeza. Kiukweli, janga hilo limeonesha  mambo mengi yanayochukuliwa kwa urahisi katika maisha ya kila siku na katika kuishi kwa watu, kama inavyooneshwa hasa na neno “kutengana kijami”. Wakati kivumishi cha kijamii kinapendekeza ukaribu na wa kuwa pamoja, neno kutenganishal inaashiria tendo la umbali. Kwa maana hiyo tunapokabiliwa na changamoto kama hiyo kwa namna ya pekee ya virusi,  tunalazimika kukaa mbali kutoka kwa kila mmoja, na hapo tunahisi hata zaidi ni kiasi gani tumeunganishwa na kila mmoja na tunaelewa kuwa tumeitwa kuwa na mshikamano mkubwa zaidi kwa kila mmoja . Pili janga limezaa matatizo mengi ya kisaikolija na hasa kutokana na kukaa pweke na matokeo ua karantini zilizotolewa na Serikali au mvutano wa ndani ya familia nyingi na katika nyumba nyingi za kutunzia wazee na kuweka wazi kabisa katika hali ambayo imejionesha wazi kuhusu mifumo ya kiafya katika nchi mbali mbali ulimwenguni. Tatu hatupaswi kusahahu matatizo ya kiuchumi, yaliyosababaishwa na mgogoro wa virusi vya corona. Watu wengi wamepoteza kazi, gepu kubwa kati ya matajiri na maskini, liimejionesha zaidi kwa idadi kubwa na  wazi, mataifa yanajikita kukakabiliana na masuala mazito ya kulipa kwa wakati ujao mabilioni ya madeni yaliyojitokeza katika dharura ya kijamii.

Nne yanafunguliwa  masuala  ya ngazi ya kisiasa na kiserikali. Na ili kuweza kupunguza madhara ya Covid – 19, kupunguza mfumo wa afya na kutunza afya ya raia kwa ujumla, serikali zimetoa vizuizi ambavyo vinaweka mipaka ya uhuru na uhuru wa mtu kwa kiwango ambacho haikuwahi kutendela tangu karne iliyopita, ambayo ni, tangu mwisho ya serikali za kiimla kwa mfano nchini Ujerumani na Umoja wa Kisovyeti. Kardinali amesema kuwa Vizuzi hivi leo hii siyo rahisi kukubalika , kwani inajionesha wazi katika maandamamo ya kupinga kwa wale wanaopiga kuwa hakuna virusi na kutokana na hali halisi ya ukosefu wa kazi. Tano, janga linakumba hata maish ya kanisa kwa ngazi ya chini. Nchi nyingi zimekosa uwezekano wa kuadhimisha misa na kuwa na  vikwanzo au kuzuiliwa kabisa wakati wa lock-down.  Hii ina maana si katika masuala ua kisials lakini kidini kwani linahusu masuala ya waamini kichungaji. Ni lazima kujiuliza ikiwa waamini watazoea kuokoa liturujia au watatafua njia ya Kanisa na masisha ya kiliturjiajia baada ya janga.

12 February 2021, 17:48