Tafuta

2020.07.24 ASKOFU MKUU VINCENZO PAGLIA 2020.07.24 ASKOFU MKUU VINCENZO PAGLIA  

Kuteuliwa kwa wajumbe wanne wapya wa PAV ni tukio muhimu!

Rais na Kansella wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha (PSV) anamshukuru Papa kwa kuteua wajumbe wanne kutoka ulimwengu wa kisomo na kisayansi na kusisitiza mchango wao katika shughuli ya mipango kuhusu masuala muhimu ya maisha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika barua ya pamoja, rais na kansela wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia na Monsinyo Renzo Pegoraro, wanapongeza uteuzi uliofanywa na Papa Francisko wa wajumbe wanne wa kawaida kwa ajili ya Taasisi ya Vatican.  Kwa njia hiyo, viongozi hawa wanasema katika taarifa yao ni tukio muhimu na jitihada zao za kujitoa kwao zilioneshwa na Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba zake aliyowahutubia Chuo cha Kipapa cha Maisha katika miaka ya hivi karibuni na katika ufafanuzi wa malengo ya kimkakati ya kazi na masomo, iliyomo katika Barua “Humana Communitas ya 2019”.

Akinukuu washiriki wapya wa kawaida, kwamba ni, pamoja na Sr. Margarita Bofarull Buñuel, RSCJ, profesa wa Taalimungu ya Maadili katika Chuo Kikuu cha Amerika ya Kati cha  José Simeón Cañas huko El Salvador, na aliluwa tayari ni Mwandishi wa zamani wa Taaluma, kielelezo katika maeneo ya taalimungu ya maadili na ya bioethics; na Padre Paolo Benanti, TOR, mhadhiri anayesimamia Taalimungu  ya Maadili, Bioethics na Neuroethics katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, na Profesa Maria Chiara Carrozza, anayefundisha Uhandisi wa Viwanda katika Shule ya kawaidia ya Pisa, Chuo hicho kinapata ujuzi mpya juu ya mada ya teknolojia na athari zake katika nyanja za maadili na afya. 

Hatimayee na uteuzi wa Profesa Walter Ricciardi, profesa wa kawaida na mkurugenzi wa Idara ya  Sayansi ya Afya ya Wanawake, Mtoto na Sayansi ya Afya ya Umma katika Chuo Kikuu  Katoliki cha Moyo Mtakatifu Milano. Taasisi ya Kipapa ya  Maisha,  kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari inaandaa kwa ubora kwa mtazamo wa Mkutano ujao mnamo Septemba juu ya mada ya afya ya umma katika mtazamo wa ulimwengu. Ni mada yenye umuhimu wake mkubwa katika ngazi ya kijamii na afya, na kwa tafakari hiyo ya kimaadili isiyoweza kuepukika mbele ya ulimwengu uliobadilishwa na Covid 19, kwa wanawake na wanaume katika kutafuta maana na matumaini ya maisha yao. Kwa kuhitimisha taarifa hiyo inasema “Kwa niaba ya Wanataaluma wote,  tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa umakini anaofuata kazi yetu. Na tunathibitisha kujitoa kupelekea msukumo huo na wito wa kinabii unaotegemea Injili katika ulimwengu wetu, ili kuelekeza njia ya kufuata katika wakati mpya”.

15 February 2021, 16:11