Tafuta

Vatican News
2018-08-01 Picha ya Mtakatifu Maroni, Mmonaki na mwanzilishi wa Kanisa la Kimaroniti 2018-08-01 Picha ya Mtakatifu Maroni, Mmonaki na mwanzilishi wa Kanisa la Kimaroniti 

Kard.Sandri:kwa maombezi ya Mt.Maroni waangazwe watoa maamuzi nchini Lebanon

Katika simu ya madhimisho ya Mkatakatifu Maroni Kardinali Sandri amemwomba ili kwa maombezo yake waangaziwe wanaotakiwa kufanya maamuzi kwa faida ya Ardhi ya Mwerezi wa Lebano kwa faida na wema wa nchi hiyo.Akinukuu maneno ya Papa Francisko amsema ni muhimu viongozi wote wa kidini na kisiasa kuweka masilahi yao kandoni ili kujitoa kwa ajili ya kufuata haki na kutekeleza mageuzi ya dhati kwa faida ya raia wake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 10 Februati imeamisha Liturujia ya Kanisa Siria ya Antikio ya Kimaroniti  katika Kanisa  La Taasisi ya Kipapa ya Kimaroniti huko Urbe Roma kwa ajiri ya fursa ya mwanzilishi wa Kanisa la Kimaroniti, Mmonaki Mtakatifu Maroun. Aliyeongeza misa misa takatifu ni Kardinali Leonardo Sandri, rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya mashariki ambaye mawazo yake yameende anchi ya Lebanon mahali ambapo katika Karne ya V Mtakaifu Maroun alianzisha Shirika la Kiroho la Kimonaki.

Katika salamu yake, kardinali amekumbuka mlipuko wa kutisha wa tarehe  4 Agosti iliyopita  katika bandari ya Beirut na juhudi za watu wa Lebanon ambao, ingawa walikuwa wameinamiwa na mgogoro wa kiuchumi, kijamii na kisiasa, walifanya kazi kwa bidii ili kukidhi mahitaji ya wale walioathirika zaidi. Hii ni kwa sababu waliwezesha barabara zipitikea kukaribisha waliobaki bila nyumba, kusambaza mahitaji msingi, kufikiria juu ya kukarabati miundo itumiwayo na jumiya  kama vile hospitali na shule. Kulikuwa na mashindano ya kukuza ufahamu, na ziara za kimataifa zililenga kutoa tumaini, wito, maneno ya kutia moyo, pamoja na ushindani thabiti wa mshikamano na taasisi na watu binafsi, mifuko, ya watu wa Lebanon walioko ughaibuni na wengine wengi amesisitiza Kardinali Sandri.

Kardinali kwa maana hiyo amemwomba Mtakatifu   Maroni aombee ili hasa wale ambao wameitwa kufanya maamuzi kwa faida ya Ardhi ya Mwerezi waangazwe,  pia akanukuu maneno ya Papa Francisko: Ni muhimu viongozi wote wa kidini, na kisiasa kuweka  masilahi yao kandoni na kujitoa kwa ajili ya  kufuata haki na kutekeleza mageuzi ya kweli kwa  faida ya raia, wake  kutenda kwa uwazi na kuchukua jukumu la matendo yao  ya dhati. Kardinali pia ameorodhesha yaliyofanywa kwa ajili ya Lebanoni, kwa mfano ziara  ya mjumbe maalum wa Papa, Kardinali  Pietro Parolin, Katibu wa Vatican mwezi mmoja baada ya mkasa huo wa tarehe 4 Agosti.

Vile vile misaada ya ufadhili, isiyo ya kawaida baada ya mlipuko, ilioonekana, kikao muhimu  cha ROACO kwa ajili  Lebanon na uratibu wa mipango ya ufuatiliaji na ujenzi na baadhi ya Wakala fulani. Kwa mujibu wa Kardinali, amesema hizi ni ishara zote za Kanisa lililo hai ambalo linataka kuishi katika barabara za ulimwengu pamoja na watoto wake wote wa kike na kiume wenye mapenzi mema, wakitoa tena picha hiyo ya Msamaria Mwema ambayo Papa Francisko ameielezea katika Waraka wake wa ‘Fratelli tutti’ yaani ‘Wote ni ndugu’. Kardinali Sandri anasema ni ushuhuda kiukweli wa Ardhi ya Mwerezi, kuwa na uwezo wa kuishi vema kwa upendo kati ya Wakristo na Waislamu wa asili tofauti na maungamo.

10 February 2021, 16:40