Tafuta

2020.10.28, silaha, makombora, vita, kusitisha silaha 2020.10.28, silaha, makombora, vita, kusitisha silaha 

Gallagher:Kuondoa silaha si chaguo la hiari,ni sharti la kimaadili

Katika fursa ya Mkutano wa ngazi za juu kwa mwaka 2021 wa Baraza kuhusu kusitisha silaha,Askofu Mkuu Gallagher,Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican,ameonesha umuhimu wa juhudi za pamoja zinazolenga kupunguza silaha na kutoa wito wa umuhimu wa kimaadili wakati huu ambapo ulimwengu huko katika mchakato wa kuelekea amani na udugu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Vatican imerudia kutoa wito wa kuondoa kabisa  silaha za  kinyuklia, au upunguzaji wa silaha, chini ya mifumo madhubuti ya kudhibiti na uthibitishaji, mbele ya vitisho vikuu vya amani na usalama ulimwenguni. Inasisitiza kuwa “kuondoa kabisa silaha si chaguo la hiari bali ni sharti la kimaadili”. Hayo yamethibitishwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican akitoa wito huo Jumatano tarehe 24 Februari katika ujumbe kwa njia ya video ulioelekezwa kwa Mkutano wa ngazi za juu kwa mwaka 2021 wa Baraza kuhusu kusitisha silaha, unaofanyika  jijini Geneva, Uswizi. Kukabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama ambazo jumuiya ya kimataifa inakabiliwa nayo leo ni muhimu kwamba Mkutano huu utambue kuwa masuala fulani yanapaswa kupitisha masilahi na sababu ya mchango wao kwa faida ya wote amesema Askofu Mkuu. Pia ameasilisha salamu kutoka kwa Papa kwa washiriki wa mkutano huo, huku akielezea matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba mambo haya yatashindwa kupitia hisia mpya ya udharura na uwajibikaji kwa wote.

Mwakilishi wa Vatican amesema kuwa shauku ya amani, usalama na utulivu ni moja wapo ya shauku  kubwa ya moyo wa mwanadamu, ingawa matamanio haya mazuri yanazuiliwa na mmomonyoko  wa maadili kwa pande nyingi na hali ya sasa ya kutokuaminiana, hasa katika uwanja huu wa silaha. Askofu Mkuu aidha amebainisha kuwa wakati unakuwa ni umuhimu kusitisha silaha ni dhahiri kwamba  silaha  hizo za nyuklia, kibaolojia na kemikali, zinatumika pia kwa ushindani wa kijeshi ambao umeongezeka katika anga na katika uwanja wa mtandao na akili bandia, kama inavyoonekana katika  mfano wa mauaji kwenye mifumo huru ya silaha. Jambo jingine la kujali kwa Vatican ni biashara haramu ya silaha ndogo ndogo, silaha nyepesi na silaha za kulipuka. Silaha hizi, ameeleza , zimetumika kusababisha maafa katika shule, hospitali na maeneo ya ibada, na kusababisha uharibifu wa miundombinu msingi kwa raia na kuathiri matarajio muhimu ya maendeleo ya binadamu.

Kwa kuzingatia umuhimu wa ugumu wa utumiaji silaha na udhibiti wa silaha, Vatican imetoa mapendekezo kwa Nchi wanachama katika mkutano huo: Kwanza, Vatican  inahimiza Nchi wanachama kushiriki katika utafiti wa wataalam juu ya suala la uthibitishaji,ambayo inaweza kufahamisha mazungumzo ya siku zijazo juu ya upunguzaji wa silaha na udhibiti wa silaha hizo.  Uthibitisho, wa pamoja na kuwa hatua muhimu ya kujenga ujasiri, ni sehemu  msingi katika kuhakikisha ufanisi wa mikataba chini utamaduni unaojulikana wa uaminifu na utambuzi. Kwa maana hiyo amehimiza utumiaji  fursa zinazotolewa na teknolojia mpya ili kuhamasisha  hatua za uthibitisho wa kuaminika, kwa sababu  ni muhimu sana kuhusiana na kusitisha  silaha za nyuklia na aina nyingine za silaha.

Ushauri wa pili  wa Vatican ni  kuanza tena kwa majadiliano rasmi juu ya upunguzaji wa silaha na juu ya kusitisha kabisa silaha chini ya mifumo madhubuti ya udhibiti ambao utaleta faida kwa wote katika mkutano huo, hasa kwa kuzingatia vitisho vya amani na usalama ikiwa ni pamoja na ugaidi, migogoro isiyo na kipimo, umaskini,  usalama wa kimtandao na shida za tabianchi. Akiangazia hitaji la ushirikiano wa kushikamana zaidi na uwajibikaji, Askofu Mkuu Gallagher amesisitiza juu ya wito wa mara kwa mara wa Papa Francisko kwamba:  "tunaweza kushinda shida ya sasa tu  ikiwa tutafanya kazi kwa pamoja, kwa sababu hakuna mtu aliye salama mpaka kila mtu awe salama". Kwa kuhitimisha ujumbe wake kwa njia ya video, Askofu Mkuu Gallagher amesisitiza kuwa usitishwaji wa  silaha hauwezi kuzingatiwa tena kama lengo la hiari, bali ni lazima na ni la kimaadili. Kwa maana hiyo kuna hitaji hali mpya ya dharura katika kujitoa kufikia makubaliano ya kudumu na kuelekea amani na ushirikiano na kwamba masuala kadhaa yanapaswa kuongezeka kuhusu makubaliano ili kushinda masilahi na ajenda kibinafsi!

24 February 2021, 15:40