Tafuta

2019.04.06: Msikiti mkuu wa Moscow nchini Urusi. 2019.04.06: Msikiti mkuu wa Moscow nchini Urusi. 

Waraka wa Fratelli tutti umetafsiriwa kwa lugha ya kirusi,uwakilishi 3 Machi!

Kwa mara ya kwanza utawakilishwa tafsiri ya lugha ya Kirusi ya Waraka wa Tatu wa Papa Francisko wa “Fratelli tutti”, yaani “Wote ni ndugu” kuhusu Udugu na urafiki kijamii.Tukio litakalofanyika tarehe 3 Machi 2021, saa 10 kamili katika Kituo cha Utamaduni cha “Pokrovskie vorota”,jijini Moscow nchini Urusi.Uchapishwaji wake utawakilishwa na kiongozi wa Kiroho wa Waislam wa Shirikisho la Urusi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Tarehe 3 Machi 2021 saa 10 kamili katika Kituo cha Utamaduni cha “Pokrovskie vorota”, jijini Moscow nchini Urusi, watawakilisha kwa mara ya kwanza tafsiri ya lugha ya Kirusi  ya Waraka wa Tatu wa Papa Francisko wa “Fratelli tutti”, yaani “Wote ni ndugu” kuhusu Udugu na urafiki kijamii. Uchapishwaji wake utawakilishwa na kiongozi wa Kiroho wa Waislam wa Shirikisho la Urusi. Sheikh Ravil Gainutdin, Balozi wa Kitume katika Shirikisho la Urusi Askofu Mkuu Giovanni D’Aniello, Askofu Mkuu Paolo Pezzi wa Jimbo Kuu la Mama wa Mungu, jijini Moscow. Kufuatia na tukio hili,  wanatoa  mwaliko kwa ushiriki wa  viongozi wakuu wa kidini na madhehubu yote ulimwenguni, tamaduni kama vile Korthodox, kiyahudi, wawakilishi wa Mashirika mengine raia, ulimwengu wa taaluma ya elimu na asasi zote za kirahia

Katika taarifa hiyo, inathibitisha kwamba, kazi hiyoya tafsiri imeandalia na kuchapishwa na nyumba ya uchapishaji  ya‘Madina’ pamoja na kikundi cha kisayansi cha Jukwaa  la Kimataifa la Waislamu, chini ya Mwongozo wa Kiroho wa Waislamu wa Shirikisho la Urusi, ambapo itakuwa  usiku wa moja ya mkesha  muhimu zaidi kwa Wakristo, yaani Noeli ya Kristo huko Urusi. Uchapishaji wa ‘Fratelli tutti’ yaani wote ni Ndugu kwa lugha ya Kirusi , inazidua safu kadhaa za  vitabu vyenye jina “Mazungumzo ya Kidini”, yenye lengo la kuhamasisha utafiti wa kisayansi na kutafakari juu ya masuala msingi yaliyomo katika kuoanisha maelewano ya uhusiano wa kidini, na vile vile kutajirisha sana mazungumzo ya kisasa ya dini. Katika muktadha wa safu hizi za vitabu, umakini utapewa mipango ya wanaharakati wa amani na watoa misaada ya kibinadamu, kutoka katika ujumbe uliotangazwa juu ya masuala haya na viongozi wa dini.

26 February 2021, 16:49