Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Novatus Rugambwa kuwa Balozi wa Vatican Kisiwani Cook na ataendelea kuiwakilisha Vatican kwenye visiwa mbali mbali vilivyoko kwenye Bahari ya Pacific. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Novatus Rugambwa kuwa Balozi wa Vatican Kisiwani Cook na ataendelea kuiwakilisha Vatican kwenye visiwa mbali mbali vilivyoko kwenye Bahari ya Pacific.  (ANSA)

Askofu mkuu Novatus Rugambwa, Balozi wa Vatican Kisiwani Cook

Askofu mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa tarehe 8 Oktoba 1957, Bukoba, nchini Tanzania. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre mikononi mwa Askofu Nestorius Timanywa kunako tarehe 6 Julai 1986. Akajiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican hapo tarehe 1 Julai 1991. Tarehe 18 Machi 2010 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Novatus Rugambwa kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Kisiwa cha Cook. Ataendelea pia kuwa Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Marshall, Kiribati, Nauru na Tonga. Amebarikiwa pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini New Zealand, Fiji, Palau na Mwakilishi wa Kitume kwenye Bahari ya Pacific. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa tarehe 8 Oktoba 1957, Katika Jimbo Katoliki la Bukoba nchini Tanzania. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre mikononi mwa Askofu Nestorius Timanywa kunako tarehe 6 Julai 1986.

Akajiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican hapo tarehe 1 Julai 1991. Baada ya kufanya kazi mbali mbali katika Balozi za Vatican, kunako tarehe 28 Juni 2007 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI akamteuwa kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la shughuli za kichungaji kwa ajili ya wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi maalum. Ilipogota tarehe 6 Februari, 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, akamteuwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Angola, Sao Tome na Principe na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu na Kardinali Tarcisio Bertone, aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican kwa wakati ule hapo tarehe 18 Machi 2010.

Na tarehe 5 Machi 2015 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Honduras. Na kunako tarehe 29 Machi 2019, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican huko New Zealand na Mwakilishi wa Kitume kwenye visiwa vya Bahari ya Pacific.Tarehe 2 Februari 2021, wakati wa Sikukuu ya kutolewa Bwana Hekaluni, sanjari na Jubilei ya Miaka 25 ya Siku ya Watawa Duniani, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa tena Askofu mkuu Novatus Rugambwa kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Kisiwa cha Cook.

Askofu mkuu Novatus
04 February 2021, 15:01