Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Kurian Mathew Vyalunkal kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Tunisia na ataendelea pia kuwa Balozi wa Vatican nchini Algeria. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Kurian Mathew Vyalunkal kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Tunisia na ataendelea pia kuwa Balozi wa Vatican nchini Algeria.  (AFP or licensors)

Askofu mkuu Kurian Vayalunkali, Balozi wa Vatican Nchini Tunisia

Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal alizaliwa tarehe 4 Agosti 1966 huko Vadavathoor, nchini India. Baada ya masomo na majiundo yake ya kipadre, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 26 Desemba 1991 na Askofu mkuu Kuriakose Kunnacherry wa “Arcieparchia Kottayam”. Aliwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu tarehe 25 Julai 2016. Ni Balozi wa Vatican: Tunisia na Algeria!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Tunisia na ataendelea pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Algeria. Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal amewahi pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea pamoja na Visiwa vya Solomon. Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal alizaliwa tarehe 4 Agosti 1966 huko Vadavathoor, nchini India. Baada ya masomo na majiundo yake ya kipadre, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 26 Desemba 1991 na Askofu mkuu Kuriakose Kunnacherry wa “Arcieparchia Kottayam”. Kunako tarehe 3 Juni 1998 alijiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican na kubahatika kushirikisha karama na vipaji vyake kwenye balozi za Vatican nchini Guinea, Korea Jamhuri ya Watu wa Dominican, Bangaladesh, Hungaria na Misri.

Tarehe 3 Mei 2016 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu hapo tarehe 25 Julai 2016. Tarehe 21 Septemba 2016, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa tena kuwa ni Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Solomon. Tarehe Mosi Januari 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Algeria. Wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Kutolewa Bwana Hekaluni, sanjari na maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipoanzisha Siku ya Watawa Duniani, tarehe 2 Februari 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa tena Balozi mpya wa Vatican nchini Tunisia.

Balozi Tunisia
04 February 2021, 14:45