Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu amemteua Monsinyo Joseph Bernard Likolo Bokal'Etumba kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Lisala, DRC. Baba Mtakatifu amemteua Monsinyo Joseph Bernard Likolo Bokal'Etumba kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Lisala, DRC. 

Askofu Joseph-Bernard-Likolo Bokal Etumba- Jimbo la Lisala!

Askofu mteule Joseph-Bernard Likolo Bokal’Etumba alizaliwa tarehe 29 Agosti 1967 huko Kinshasa. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 30 Mei 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, amewahi kuwa Paroko-usu kati ya mwaka 1999 hadi mwaka 2004 na Mkuu wa Shule ya Msingi kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 2004. Ni Jaalimu na Mwana Liturujia.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Joseph-Bernard Likolo Bokal’Etumba kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Lisala, nchini DRC. Hadi kuteuliwa kwake, Monsinyo Joseph-Bernard Likolo Bokal’Etumba alikuwa ni Katibu mtendaji wa Tume ya Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa, Baraza la Maaskofu Katoliki DRC., “Conferénce Episcopale Nationale du Congo”; C.E.N.C.O. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Joseph-Bernard Likolo Bokal’Etumba alizaliwa tarehe 29 Agosti 1967 huko Kinshasa. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 30 Mei 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, amewahi kuwa Paroko-usu kati ya mwaka 1999 hadi mwaka 2004 na Mkuu wa Shule ya Msingi kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 2004. Kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2008 alitumwa na Jimbo kuu la Kinshasa kujiendeleza zaidi katika masomo ya Liturujia ya Kanisa hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamili kutoka katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Paris, nchini Ufaransa “l’Institut Catholique de Paris”.

Kati ya Mwaka 2008 hadi mwaka 2013 alijiendeleza zaidi katika Taasisi ya Kipapa ya Liturujia, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Anselmi, Roma na kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Liturujia ya Kanisa. Aliporejea Jimbo kuu la Kinshasa alipangiwa kuwa Mlezi wa Mapadre na Waseminari wa Jumuiya ya Emmanuel nchini DRC tangu mwaka 2010. Itakumbukwa kwamba, tangu mwaka 2013 amekuwa pia ni Jaalimu wa Liturujia Seminari kuu ya Mtakatifu Yohane XXIII “Grand Séminaire de Theologie Saint Jean XXIII”. Tangu mwaka 2014 hadi mwaka 2020 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Malezi na Msindikizaji wa Mapadre wenye matatizo katika maisha yao. Tangu mwaka 2016 hadi kuteuliwa kwake Askofu mteule Joseph-Bernard Likolo Bokal’Etumba wa Jimbo Katoliki la Lisala alikuwa ni Katibu mtendaji wa ya Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa, Baraza la Maaskofu Katoliki DRC., “Conferénce Episcopale Nationale du Congo”; C.E.N.C.O.

Uteuzi DRC

 

 

 

15 February 2021, 14:58