Tafuta

Vatican News
 Bado kuna haja ya kujikita kutunza wazee badala ya kuwabagua Bado kuna haja ya kujikita kutunza wazee badala ya kuwabagua 

Ask.Mkuu Paglia:wito wa kutazama kwa upya mifumo ya utunzaji wa wazee!

Katika kutano na waandishi kwenye fursa ya kuwakilisha Hati ya Taasisi ya Kipapa ya Maisha kuhusu“Uzee:wakati wetu ujao.Hali halisi ya wazee baada ya janga”,ni mwaliko wa kupokea janga kama fursa ya kuimarisha uhusiano kati ya vizazi,kwa kuzingatia kuwa wazee wametoa mchango mkubwa.Nimategemo ya maelekezo ya Hati yaweze kusikilizwa na mataifa.Hati mbili ya mbili kuhusu watoto na walemavu zitatolewa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumanne tarehe 9 Februari imewakilishwa kwa waandishi wa habari Hati ya Taasisi ya Kipapa ya Elimu kwa ajili ya Maisha inayoongozwa na kauli mbiu “Uzee:wakati wetu ujao. Hali halisi ya wazee baada ya janga. Mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao ambao umeona Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu kwa ajili ya Maisha; Monsinyo Bruno Marie Duffè, Katibu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu; Professa Etsuo Akiba, wa Chuo Kikuu cha Toyama, Japan; Msomi wa kawaida wa Chuo cha Kipapa kwa ajili ya Maisha, aliyeunganishwa moja kwa moja kutoka mji wa Japan. Katika uwakilishi wa hati hiyo kwanza amemshukuru Papa Francisko kwa ajili ya Kuanzisha “Siku ya wazee ambayo itafanyika kila mwaka tarehe 25 Julai ya Siku Kuu ya Mtakatifu Johakimu na Anna babu zake Yesu.  Askofu Mkuu anasema ni mwaliko kwa waamini ili waweze kukuza ndani mwao na yale yanayowazunguka uweelewa wa umakini wa babu, bibi na wazee.

Mara nyingi katika miaka ya mwisho mapapa wameingilia kati kutoa wito kwa wote juu ya umakini mpya kwa wazee. Inatosha kukumbua Barua kwa ajili ya Wazee ya Mtakatifu Yohane Paulo II na hotuba yenye thamani ya Papa Mstaafu Benedikto XVI na unyeti wa Magisterium ya Papa Francisko hadi kufikia kuhitisha siku kuu ya wazee jijini Roma kunako mwaka 20217. Papa ambaye haachi kukataa utumaduni wa kibaguzi ambao unaepelekea kuacha wazee peke yao na kutoa ushauri kwa namna moja ya kuwatunza kwa njia ya mtandao wa upendo na uhusiano unaounganisha vizazi ili familia na jumuiya ya kikristo iwe nyumba ya kukarimu wote  walio wadogo na wazee na kuenezea ndani humo utamaduni na imani kati ya vizazi vinavyoendelea na vilivyo hai.

Askofu Mkuu Paglia amesema Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha, inataka kusisitiza dharura ya umakini mpya kwa ajili ya watu wazee ambao kwa miaka kumi ya mwisho wameongezeka idadi yao kila sehemu. Lakini zaidi ya hayo iweze kuongezea ule ukaribu zaidi wa kuelekea wao,  kuwa na utambuzi zaidi kuhusiana na mbadiliko yanayohitajika haraka. Janga la Covid- 19 ambalo limesababaisha waathirika wengi wazee, limeonesha wazi ukosefu wa uwezo wa jamii ya sasa katika kutunza wazee inavyotakiwa. Janga, utamaduni wa ubaguzi  na ambao Papa mara nyingi amesisitiza, kiukweli umeonesha  balaa kubwa la idadi ya wazee waliokufa. Katika mabara yote janga limewashambulia wazee zaidi. Idadi ya waliofariki ni ya kinyama katika ukatili wao. Katika janga la sasa, inazungumziwa kuwa zaidi ya milioni  2, 300,000 ya wazee wamekufa kwa sababu ya covid-19, na sehemu kubwa ni zaidi ya umri wa miaka 75. Haya ni mauaji halisi ya wazee, amesisitza. Na sehemu kubwa ya waliofariki walikuwa wanatunzwa katika vituo vya kutunzia wazee. Takwimu za baadhi ya nchi kama Italia zinaonesha kuwa nusu ya wazee waathirika wa Covid-19 walikuwa kwenye vituo hivyo na wakati asilimia 24 tu ya wote wazee walikuwa wanaishi nyumbani.

Kubaki katika nyumba zao wakati wa janga, kulinganisha na hali halisi, imeweza kuwalinda zaidi. Hii imeonesha zaidi barani Ulaya, na hata katika maeneo mengine ya ulimwengu. Ni muhimu kutafakari tena ukaribu wa jamii kwa wazee. Mengi yanahitaji kupitiwa katika mfumo wa utunzaji na msaada kwa wazee. Kuwekwa wazee katika nyumba za kustaafu, katika kila nchi, sio kusema kwamba ni kuhakikishe hali bora za utunzaji, kidogo kwa wale ambao ni dhaifu. Papa Francisko alikumbuka kwamba, lazima kufikiria namna ya kutoka katika janga hilo, tukiwa kama hapo awali: ama sisi kuwa bora au sisi kuwa mbaya zaidi. Inategemea sisi na jinsi tunavyoanza kujenga siku zijazo leo hii. Ujumbe huu wa tatu ambao Taasisi imetoa kuhusiana na janga unakusudia kusaidia kujenga mustakabali mpya kwa wazee katika jamii amedhibitisha Askofu Mkuu Paglia.

Ni jukumu la Kanisa kuchukua wito wa kinabii ambao unaelekeza alfajiri ya siku mpya. Hatuwezi kushindwa kujitoa kwa ajili ya maono makubwa ambayo yanaongoza utunzaji wa kizazi cha tatu na cha nne. Tuna deni kwa wazee wetu, kwa wale wote ambao watakuwa hivyo katika miaka ijayo. Ustaarabu wa enzi hupimwa na jinsi tunavyowatendea wale ambao ni dhaifu na wanyonge zaidi. Kifo na mateso ya wazee zaidi hakiwezi kukosa kuwakilisha wito wa kufanya vizuri, kufanya tofauti, na kufanya zaidi. Tuna deni kwa watoto wetu, kwa wale ambao ni wadogo na wapo mwanzoni mwa maisha: kuelimisha maisha ya Injili pia inamaanisha kufundisha kwamba udhaifu hata ule wa wazee, sio laana bali ni njia ya kukutana na Mungu katika uso wa Yesu Kristo.  Udhaifu kwa macho ya Injili, unaweza kuwa nguvu na chombo cha uinjilishaji. Kanisa, mwalimu wa maisha, linatakiwa daima kutafsiri katika ulimwengu mpya na unaobadilik ule  wito wake wa kuwa kielelezo na nuru  kwa familia nyingi na kwa jamii kwa ujumla ili wale ambao wanazeeka wasaidiwe katika nyumba zao  na kwa hali yoyote wasiachwe  kamwe peke yao.

09 February 2021, 17:15