27 Februari ni Kumbu kumbu kiliturujia ya Mt.Gregory wa Narek
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Kwa mujibu wa Kalenda ya Kirumi, baada ya Kuchapishwa kwa Hati ya Papa Francisko kuhusu kuwekwa rasimi kila tarehe 27 Februari, kuwa kumbu kumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Gregorio wa Narek, Abate na Mwalimu wa Kanisa, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki na Baraza la Kipapa la kuhamasisha Umoja wa Kikristo, wameandaa maadhimisho mjini Vatican Jumamosi tarehe 27 Februari 2021 kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Armenia jijini Vatican.
Maadhiisho ya misa takatifu hiyo itaongozwa na Kardinali Leonardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Masharikia, asubuhi saa 4.30, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na kufuata baadaye sala ya kiekumene mbele ya sanamu ya Mtakatifu Gregory wa Narek iliyobarikiwa na Papa Francisko mnamo 2018 katika bustani za Vatican.
Pamoja na Kardinali wanatashiriki misa hiyo, Askofu mkuu Lévon Bogos Zékyian, wa Istanbul ya Kiarmeni na Mwakilishi wa Kipapa wa Shirika la Kiarmenia pamoja na Askofu Mkuu Brian Farrell, Katibu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Umoja wa Kikrsito. Katika Sala ya kikumene itaongozwa na mhemimiwa Khajag Ian, ambaye ni Mwakilishi wa Kanisa la kitume la Kiarmenia, Roma kwa uwepo wa Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo.