Tafuta

Papa Francisko amemteua Prof. Vincenzo Buonomo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran, kuwa Rais mpya wa Tume ya Nidhamu ya Secretarieti kuu ya Vatican, "Curia Romana". Papa Francisko amemteua Prof. Vincenzo Buonomo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran, kuwa Rais mpya wa Tume ya Nidhamu ya Secretarieti kuu ya Vatican, "Curia Romana". 

Prof. Vincenzo Buonomo Rais wa Tume ya Nidhamu Mjini Vatican

Papa Francisko amemteua Professa Vincenzo Buonomo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran kuwa Rais wa Tume ya Nidhamu ya Sekretarieti Kuu ya Vatican “Curia Romana”. Wajumbe wa Tume hii ni pamoja na Monsinyo Alejandro W. Bunge, Rais wa Idara ya Kazi Vatican pamoja na Dr. Maximino Caballero Ledo, Katibu mkuu wa Sekretarieti ya Uchumi mjini Vatican. Nidhamu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Professa Vincenzo Buonomo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran kuwa Rais wa Tume ya Nidhamu ya Sekretarieti Kuu ya Vatican “Curia Romana”. Wajumbe wa Tume hii ni pamoja na Monsinyo Alejandro W. Bunge, Rais wa Idara ya Kazi Vatican pamoja na Dr. Maximino Caballero Ledo, Katibu mkuu wa Sektrarieti ya Uchumi Vatican. Tume ya Nidhamu ya Sekretarieti kuu ya Vatican ambayo bado haijafikia kiwango cha kuitwa Tume ya Kipapa, ilianzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako tarehe 5 Oktoba 1981.

Tume hii inaundwa na Rais wa Tume anayesaidiana na wajumbe watano. Kazi kubwa ya Tume hii ni kutoa uamuzi wa kumsimamisha kazi mfanyakazi wa Sekretarieti kuu ya Vatican. Pili ni kutoa uamuzi wa kumwachisha kazi na tatu ni kutoa au kumwombea msamaha mfanyakazi wa Sekretarieti kuu ya Vatican. Askofu Georgio Corbellini alikuwa ni Rais wa Tume hii kuanzia tarehe 11 Mei 2010 hadi tarehe 13 Novemba 2019 alipofariki dunia.

Tume ya Nidhamu

 

09 January 2021, 14:51