Tafuta

2018.06.28 PAPA FRANCISKO NA PAPA MSTAAFU BENEDIKTO XVI 2018.06.28 PAPA FRANCISKO NA PAPA MSTAAFU BENEDIKTO XVI 

Papa Francisko na Papa Mstaafu wamepata chanjo ya kuzuia covid!

Katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Mediaset Italia,Dominika iliyopitia alikuwa ametangaza juu ya utayari chanjo pia Papa Mstaafu amepatiwa chanjo leo hii.

Na Sr. Angela Rwezaula,-Vatican

Kampeni ya chanjo jijini Vatican inaendelea ambayo imeanza Jumatano asubuhi, tarehe 13 Januari 2021 baada ya kufika. Miongoni mwa waliokwisha pokea dozi ya kwanza ya chanjo ni Papa Francisko pia Papa Mstaafu Benedikto XVI. Papa Francisko alikuwa amekwisha sema wakati wa mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Mediaset Italia, “Tg, Canale 5”, alikuwa amebainisha kupokea chanjo wiki hii na Askofu Georg Gaenswein, alikuwa amethibitisha kwamba  hata Papa Mstaafu angeweza kupokea chanjo hiyo.

Itakumbukwa wakati wa mahojiano hayo ya Papa alivyokuw ametoa kuwa kielelezo cha chanjo ni kama “tendo maadili kwa sababu ukichezea afya, unachezea na maisha lakini hata kuchezea maisha ya wengine” .

14 January 2021, 15:40