Tafuta

2021.01.14 Filaret wa  Minsk na Papa Benedikto XVI 2021.01.14 Filaret wa Minsk na Papa Benedikto XVI 

Kard.Koch.Filaret alifanya kuzaliwa upya kiroho Belarusi

Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo,katika barua yake kwa ajili ya Upatriaki wote wa Belarusi,amekumbuka sura ya Patriaki mstaafu Filaret,aliyeaga dunia hivi karibuni kwa sababu ya virusi vya corona.

Na Sr. Angela Rwezaula,-Vatican.

Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo katika kuelezea salam zake za rambi rambi kufuatia na kifo cha Patriaki mstaafu Filaret, wa Esarca huko Belarusi yote,  aliyeaga dunia tarehe 12 Januari 2021 akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kulazwa kwa muda mrefu katika hospitali kwa  maambukizi ya Covid-19, anasema alikuwa mwanaume mwema na aliyefanya kuzaliwa upya Belarusi. Katika barua yake aliyomwelekeza Mkuu wa Kanisa  kwa ajili ya Kanisa lote la Esarca, Belarusi yote, Kardinali Koch anaonesha maskitiko  kwa kuondokewa na kiongozi huyo, huku akiwahakikishia sala zake na kumshukuru Mungu kwa sababu ya huduma yake kwa muda mrefu aliyoitoa kwa miaka mingi.

Mwanume wa mazungumzo

Wakati wa huduma yake Patriaki Filaret, alichangia kwa kiasi kukubwa kuzaliwa kwa upya maisha ya Kanisa, huku akikarabati na kujenga makanisa mapya na monasteri;  na si hayo tu lakini pia katika harakati za kujikita kutoa chachu mpya katika mafundisho ya kidini na mipango ya elimu katika Kanisa lote  la Belarusi. Alikuwa ni mtu wa upatanisho kati ya Wakristo wa Mashariki na Magharibi kwa namna ya pekee kuweka nguvu ya uhusiano wa kidugu kati ya Kanisa la kiorthodox na Kanisa Katoliki pia akijenga mtandao wenye kuleta matunda ya urafiki kiroho kwa ndugu wengi wakatoliki. Mazishi yamefanyika tarehe 15 Januari 2021 katika Kanisa la Minsk kwa kuongozwa na Askofu Mkuu Tadeusz Kondrusiewicz kwa ajili ya roho yake.

15 January 2021, 16:08