Tafuta

Vatican News
Siku ya XXV ya Watawa duniani sambamba na siku Kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni Siku ya XXV ya Watawa duniani sambamba na siku Kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni 

Kard Braz de Aviz,ahimiza watawa kutoa kipaumbele cha Waraka wa Fratelli tutti!

Kardinali Braz de Aviz,Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume ameandika barua kwa watawa katika fursa ya Siku ya XXV ya Watawa duniani itakayofanyika tarehe 2 Februari,sambamba na Siku Kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni.Katika barua hiyo inaongozwa na mada ya“ Fratelli tutti mizizi ya kinabii",ambapo anahimiza mashirika yote kutoa kipaumbele cha 'Waraka wa Fratelli' tutti katika maisha yao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Liturujia ya Siku Kuu ya Kutolewa kwa Bwana Hekaluni sambamba na Siku ya Watawa duniani ifanyikayo kila tarehe 2 Februari, Kardinali João Braz de Aviz, Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume ameandika barua yake kwa watawa wote ikiwa imetiwa pia saini na katibu wake , Askofu Mkuu José Rodríguez Carballo, o.f.m. ambayo inaongozwa na mada “Fratelli tutti mizizi ya kinabii".  Katika barua hiyo Kardinali  Joao anapenda awafikie wote katika siku muhimu kwao kama watawa wa kike na kiume,  ambayo imetolewa kwa wito wao wa kushangaza katika mitindo mbali mbali ambayo inafanya kuangaza upendo wa Mungu kwa kila mwanamke na mwanaume na ulimwengu wote. Kardinali Joao anaandika kuwa tarehe 2 Februari itaadhimisha siku ya XXV ya Siku ya watawa. Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 11.30 jioni, Papa Francisko ataongoza maadhimisho ya Misa Takatifu na ambayo inafunua ishara na sura zenye furaha ambazo zilikuwa zinaangaza miaka iliyopita, lakini ambayo daima ni kielelezo cha furaha ya kuzaa matunda kama tabia ya maisha ya kitawa. 

Kardinali katika barua hiyo ameelezea kuhusu suala la ukosefu wa kuungana kwa pamoja kimwili kutokana na sababu za janga la corona lakini wakionesha ukaribu wao kwa kila jumuiya, na kwa wale wote wanaofanya kazi katika baraza lao. Kardinali pia ameandika juu ya habari wanazo zipokea na jinsi ambavyo kila jumuiya katika mataifa wanazungumzia mahangaiko, maambukizi, vifo na matatizo mengine ya kibinadamu na kiuchumi ambayo yanajumuisha hata hofu ya kupungua kwa miito katika mashirika. Vile vile majaribu ya imani na mateso, maambukizi, ushuhuda mtulivu licha ya uchungu na ukosefu wa uhakika, mshikamano na kila jeraha, utunzaji na ukaribu kwa walio wa mwisho, upendo na huduma hata kwa gharama ya maisha (taz Fratelli tutti II). "Hatuwezi kutamka majina yote, lakini kwa kila mmoja wetu tunaomba baraka ya Bwana ili aweze kuondoa katika hali hii ngumu na kifika  tukijua kuwa  sisi sote tuko kwenye mtumbwi moja, wote wadhaifu na tuliochanganyikiwa, lakini wakati huo huo ni muhimu, na wote tunaitwa kupiga kasia na kusonga mbele pamoja "(taz. Mambo ya Papa Francisko, Ijumaa 27 Machi 2020). Kuwa Wasamaria wa siku hizi, kushinda jaribu la kugeukia upande mwingine na kujililia mwenyewe, au kufunga macho mbele ya maumivu, mateso, umaskini wa wanaume na wanawake wengi, na watu wengi.

Katika waraka wa Fratelli tutti, Baba Mtakatifu Francisko anatualika tuchukue hatua pamoja, kufufua kwa wote azma ya ulimwengu kwa udugu (8), kuota pamoja (Ft. 9) "ili katika mchakato wa njia tofauti za sasa za kuondoa au kupuuza wengine, tunaweza kukabiliana na ndoto mpya ya ushirikiano na urafiki kijamii”(Ft. 6). Watawa wa kike na kiume wa taasisi zote, za kimonaki, vyama vya kitume, washirika wa ordo virginum, Wahermits, wanawaombwa wote kuweka kipaumbele cha "Waraka wa Fratelli tutti" katika maisha yao, malezi na utume.  “Kuanzia sasa hatuwezi kupuuza ukweli huu: sisi sote ni kaka na dada, kama kweli tunaomba, kwa ufahamu mwingi, sala ya Baba Yetu, kwa sababu ni uwazi kuwa ni Baba wa wote, kinyume chake hatuwezi kuwa na sababu thabiti na imara kwa wito wa udugu (Ft. 272)”, anaandika Kardinali.

Waraka huu uliandikwa katika wakati wa kihistoria, ambao Baba Mtakatifu Francisko mwenyewe alifafanua kuwa ni saa ya ukweli, Kardinali anabainisha kuwa ni zawadi ya thamani kwa kila aina ya maisha ya kujitoa ambayo, bila kuficha vidonda vingi vya udugu, inaweza kupata ndani mwake mizizi ya unabii. Tunakabiliwa na wito mpya wa Roho Mtakatifu. Kama vile Mtakatifu Yohane Paulo II, kwa kuzingatia mafundisho juu ya muungano wa Kanisa, alikuwa amewataka watu walioweka wakfu kuwa wataalam wa kweli katika muungano na kutekeleza hali yake ya kiroho (Vc, 46), Papa Francisko, kwa kuongozwa na msukumo kutoka kwa Mtakatifu Fransis wa Assisi, mwanzilishi wa taasisi nyingi za maisha ya wakfu, amepanua upeo wa macho yake na kutualika kuwa wasanii wa udugu wa ulimwengu, walinzi wa nyumba ya pamoja: ya dunia na ya kila kiumbe (taz. Laudato si '). Kaka na dada wa wote, bila kujali imani ya kila mtu, tamaduni na mila, kwa sababu siku zijazo sio zenye rangi moja (Ft. 100) na ulimwengu ni kama umbo lenye sura nyingi zinazo ruhusu uzuri wake uangaze, hasa kupitia sura zake tofauti.

Kwa njia hiyo ni suala  la kufungua michakato ya kusindikiza, kubadilisha na kuzalisha; kukuza mipango kwa ajili ya kuhamasisha utamaduni wa kukutana na mazungumzo kati ya watu na vizazi tofauti; kuanzia jamii ya ufundi hadi kufikia kila kona ya dunia na kila kiumbe, kwa sababu, kama wakati huu wa janga, tumepata uzoefu kwamba kila kitu kimeunganishwa, kila kitu kinahusiana, kila kitu kimeunganishwa (taz.Laudato si'). Katika barua imeandikwa kuwa:“Tunaota kama ubinadamu mmoja, kama wasafiri waliotengenezwa na mwili uliosawa  wa kibinadamu, kama watoto wa nchi hii ambayo inatuhifadhi sisi sote, kila mmoja na utajiri wa imani yake, kila mmoja na sauti yake, wote ni ndugu! (Ft. 8). Kwa upeo huo wa ndoto ambayo imekabidhiwa mikononi mwetu, kwa shauku yetu, kwa uvumilivu wetu, tarehe  2 Februari ijayo pia itakuwa sikukuu nzuri ambayo itakuwa ni  kumsifu na kumshukuru Bwana kwa zawadi ya wito na utume wetu! Tunamkabidhi kila mmoja kwa Maria, Mama yetu, Mama wa Kanisa, mwanamke mwaminifu na kwa Mtakatifu Josefu, mwenzi wake, katika mwaka huu uliowekwa wakfu kwake. Imani hai na yenye upendo iimarishwe ndani ya kila mmoja wenu, tumaini fulani, la kufurahisha, upendo mnyenyekevu na wenye bidii. Kwa njia ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Mungu wetu mwenye huruma, tunaomba baraka juu ya kila mmoja wenu”.

26 January 2021, 18:11