Tafuta

Kampeni ya chanjia imeanza mjini Vatican Kampeni ya chanjia imeanza mjini Vatican 

Kampeni ya chanjo imeanza mjini Vatican

Kuanzi leo mjini Vatican nakuendelea ni zoezi la kampeni ya utoaji chanjo dhidi ya virusi vya corona.Wameanza na watu mbalimbali ambao wako hatarini kuanzia na wazee kama ilivyokuwa imepangwa.

Na Sr. Angela Rwezaula,- Vatican

Kampeni ya chanjo dhidi ya Covid-19 imeanza leo hii katika maingilio ya  Ukumbi wa Paulo VI, Jijini Vatican. Hii imethibitishwa na Msemaji wa Vatican, Dk. Matteo Bruni, katika  Ofisi ya Wanahabari akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari. Kipaumbele amebainisha kwambi, ni kama ilivyokuwa imewasilishwa tayari na Idara ya Afya na Usafi ya Serikali ya mji kwamba inapewa  wafanyakazi wa afya na usalama wa umma, kwa wazee na kwa wafanyakazi ambao mara nyingi wanawasiliana na umma.

Hata hivyo pia raia, wafanyakazi na wastaafu watapewa chanjo, lakini pia wanafamilia wanaofaidika na msaada wa FAS (Mfuko wa Huduma ya Afya). Kampeni kwa wakati huu ni ya hiari kabisa. Kwa sasa, watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wametengwa kwenye chanjo hiyo kwa sababu bado kufanyiwa tafiti ikiwa ni pamoja na kikundi hiki ambacho bado hakijafanyiwa.

13 January 2021, 15:56