Tafuta

Vatican News
2020.06.13 Cardinale Turkson visita associazione al polo ex fienile, Tor Bella Monaca 2020.06.13 Cardinale Turkson visita associazione al polo ex fienile, Tor Bella Monaca  (Vatican Media)

Kard.Turkson:Chanjo kwa ajili ya wote lakini hata dunia,nyumba

Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu kwa njia ya mtandao ametoa hotua yake katika mkutano wa Mwaka wa uchumi unaondelea katika mji Uswiss kwa njia ya mtandao.Covid imebadilisha sayari na kuonesha umuhimu wa uwajibikaji na mshikamano.Tunapozungumza juu ya utu wa mwanadamu,hatuwezi kutokuafikiana na lazima tuunge mkono.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuna ulimwengu ambao ununuzi unaweza kuletwa nyumbani, ukiepuka hatari ya umati wa watu, na ulimwengu mwingine ambao, ikiwa unataka kula, lazima upate chakula kutoka sokoni ambalo hakuna cha kuhifadhi umbali uliofafanuliwa. Kwa kufafanua kiurahisi zaidi, kuna ulimwengu ambao una nyumba ya kuweka familia salama na ulimwengu mwingine ambao hauna usalama huu kwa sababu hauna, au hauna tena nyumba inayostahili jina na kazi ya kuilipia. Ni ulimwengu wa umaskini, ambao pia unaletwa na uharibifu wa Covid, ambao Kardinali Peter Turkson  Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Bindadamu ameuwakilisha mbele ya Jukwa la Davos, ambapo mada  ya janga ndiy halisi ya kufafanua kwa njia ya mtandao

Ni ulimwengu ambao unahitaji uhakika wa nguvu zaidi kuliko ule uliobomoka na janga hilo. Kuanzia na matibabu ya kupambana na virusi ambayo ufikiaji wa wote ndiyo matashi mema  ya Papa na kuungwa mkono na mkuu wa Baraza la Kipapa la  Maendeleo Fungamani ya  Binadamu amethibitisha  na kwamba bado ni lengo ambalo haliko wazi kabisa. “Tunaona serikali zinajali watu wake tu na kisha wengine?”, amebainisha Kadinali anayejibu maswali kadhaa. “Nchi kadhaa pia zina uwezo wa kutengeneza dawa na ikiwa mali miliki ingechelewa inaweza kuleta uzalishaji kwa ngazi za ndani ya nchi mahalia  huku ukipunguza athari za maambukizi. Kuna aina mpya za virusi ambazo zinaleta wasiwasi, mfano ile ya Afrika Kusini, na ikiwa mtu anaweza kutafiti tiba mbadala, amesema Kardinali Turkson, hii inaweza kusaidia kudhibiti dharura na kupunguza viwango vya vifo”.

Suala la chanjo ni kipaumbele katika hali hii ya ulimwengu lakini sio pekee. Kikao cha Jukwaa ambalo Kardinali amezungumza ni fasaha, na  kutaka kumaliza  umaskini kabla ya kuwa virusi. Vatican imejikita kwa  haraka shukrani kwa Tume ya Covid-19 iliyoundwa na Papa, kwa kuunda kikosi kazi cha wataalam walio na jukumu la kusoma kinachotokea na kupendekeza maono ya siku zijazo. Kwa muda wamekuwa wakishirikiana na kile wanachokiita vikundi maarufu vya harakati, amesema kardinali. Na katika hili amebainisha kwamba wamegundua maeneo matatu muhimu: ardhi, kazi na nyumba. Malengo haya matatu ndiyo wanafuatilia sasa ili kuhakikisha kuwa watu wanakuwa na mahali pa kulala, na hii pia inamaanisha kulinda familia na usalama na ustawi wake.

Jaribio hili, ambalo Papa amekuwa akilitaka, mara kadhaa ametoa  wito  kwa miezi kadhaa ya kuwa na dhamiri ya ulimwengu ambayo ina vyombo vya lazima, na inawezekana ikiwa inaegemea thamani wazi yaani kumweka mtu katikati, kama kitovu. Mwaka jana ni Papa Francisko mwenyewe aliyemwomba, mwaka huu, Kardinali Turkson awe msemaji wake.Kwa maana hiyo   Kardinali amesema “Tunapozungumza juu ya utu wa mwanadamu, hatuwezi kutoafikiana na lazima tuunge mkono. Ni suala la umakini ambalo linakuwa chaguo la kisiasa na mwelekeo wa kupiga hatua”. Wakati fulani wananajaribu kuunda jukwaa na sera za kijamii za kiuchumi ambao zinazoweza kutunza wengine, kwa sababu familia ya wanadamu ni familia moja iliyounganishwa. Na mazoezi ya mshikamano, ya kutunza, ambayo yanahitimisha, yanaunda na kueneza udugu wa wanadamu.

29 January 2021, 15:10