Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la Askofu mkuu Thomas Edward Gullickson la kutaka kung'atuka kutoka madarakani. Kwa miaka mingi amekuwa ni Balozi wa Vatican sehemu mbalimbali za dunia. Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la Askofu mkuu Thomas Edward Gullickson la kutaka kung'atuka kutoka madarakani. Kwa miaka mingi amekuwa ni Balozi wa Vatican sehemu mbalimbali za dunia. 

Askofu mkuu Thomas Edward Gullickson Ang'atuka Madarakani

Askofu mkuu mstaafu Thomas Edward Gullickson alizaliwa tarehe 14 Agosti 1950 huko nchini Marekani. Tarehe 27 Juni 1976 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 2 Oktoba 2004, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Pacific na hatimaye, kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu tarehe 11 Novemba 2004. Ameng'atuka 2020.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Thomas Edward Gullickson, Balozi wa Vatican nchini Uswiss na Liechtenstein la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mstaafu Thomas Edward Gullickson alizaliwa tarehe 14 Agosti 1950 huko Sioux Falls, Jimbo Katoliki la Sioux Falls, Kusini mwa Dakota, nchini Marekani. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 27 Juni 1976 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 2 Oktoba 2004, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Pacific na hatimaye, kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu tarehe 11 Novemba 2004.

Kunako tarehe 21 Mei 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Ukraine. Ilipogota tarehe 5 Septemba 2015, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uswiss na Liechtenstein. Tarehe 31 Desemba 2020, Baba Mtakatifu Francisko akaridhia ombi lake la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Kwa ufupi kabisa katika kazi yake ya kuongoza, kufundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu, amelitumikia Kanisa kama Padre kwa muda wa miaka 44 na kama Askofu mkuu na Balozi wa Vatican kwa muda wa takribani miaka 16.

Askofu mkuu Thomas

 

01 January 2021, 13:40