Tafuta

Vatican News
Askofu mkuu  Kurian Mathew Vayalunkal ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Algeria Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Algeria  (Vatican Media)

Askofu mkuu Kurian Vayalunkali, Balozi wa Vatican Nchini Algeria

Askofu mkuu Kurian M. Vayalunkal alizaliwa tarehe 4 Agosti 1966 huko India. Tarehe 26 Desemba 1991 akapewa daraja takatifu ya Upadre. Tarehe 3 Juni 1988 alijiunga na utume wa diplomasia ya Kanisa mjini Vatican. Tarehe 3 Mei 2016, akateuliwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na kuwekwa wakfu hapo tarehe 25 Julai 2016. Tarehe 1 Jan. 2021, Algeria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Algeria. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea pamoja na Visiwa vya Solomon. Askofu mkuu Kurian Mathew Vayalunkal alizaliwa tarehe 4 Agosti 1966 huko Vadavathoor, nchini India. Baada ya masomo na majiundo yake ya kipadre, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 26 Desemba 1991 na Askofu mkuu Kuriakose Kunnacherry wa “Arcieparchia Kottayam”.

Kunako tarehe 3 Juni 1998 alijiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican na kubahatika kushirikisha karama na vipaji vyake kwenye balozi za Vatican nchini Guinea, Korea Jamhuri ya Watu wa Dominican, Bangaladesh, Hungaria na Misri. Tarehe 3 Mei 2016 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu hapo tarehe 25 Julai 2016. Tarehe 21 Septemba 2016, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa tena kuwa ni Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Solomon. Na tarehe Mosi Januari 2021, Baba Mtakatifu Francisko amemteua kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Algeria.

Nuncio Algeria
01 January 2021, 14:03