Tafuta

Askofu mkuu Giovanni D'Aniello ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya Uzbekistan na ataendelea kuwa pia Balozi wa Vatican nchini Urussi. Askofu mkuu Giovanni D'Aniello ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya Uzbekistan na ataendelea kuwa pia Balozi wa Vatican nchini Urussi. 

Askofu mkuu Giovanni D' Aniello: Balozi wa Vatican Uzbekistan!

Askofu mkuu Giovanni d’ANIELLO alizaliwa tarehe 5 Januari 1955, Jimboni Aversa, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 8 Desemba 1978 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 1 Juni 1983 akaanza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Kanisa. Tarehe 22 Septemba akateuliwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 6 Januari 2002.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Giovanni d’ANIELLO kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Uzbekistan na wakati huo huo ataendelea kuwa ni Balozi wa Vatican nchiniUrussi. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Giovanni d’ANIELLO amewahi pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Brazil. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Giovanni d’ANIELLO alizaliwa tarehe 5 Januari 1955, Jimboni Aversa, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 8 Desemba 1978 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 1 Juni 1983 akaanza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Kanisa.

Tangu wakati huo, akatumwa kwenda kutekeleza majukumu yake kwenye Balozi za Vatican nchini Burundi, Thailand, Lebanon, Brazil na baadaye, alirejea tena mjini Vatican na kuendeleza utume wake kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican, kitengo cha Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Tarehe 15 Desemba 2001, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini DRC. Tarehe 6 Januari 2002, akiwa na umri wa miaka 47 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu na Mtakatifu Yohane Paulo II.

Ilikuwa ni tarehe 22 Septemba 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Thailand, Cambodia, Myanmar na Laos. Tarehe 10 Februari 2012, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Brazil. Tarehe 1 Juni 2020, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Urussi. Na ilipogota tarehe 14 Januari 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteua kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Uzbekistan.

Uteuzi
15 January 2021, 12:14