Tafuta

Askofu mkuu Eugene Martin Nugent ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Kuwait na Qatar kuanzia tarehe 7 Januari 2021. Askofu mkuu Eugene Martin Nugent ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Kuwait na Qatar kuanzia tarehe 7 Januari 2021. 

Askofu mkuu Eugene Martin Nugent: Balozi Kuwait na Qatar!

Askofu mkuu Nugent alizaliwa mwaka 1958. Tarehe 9 Julai 1983 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 1 Julai 1992 alijiunga na utume wa diplomasia ya Kanisa. Tarehe 13 Februari 2010 akateuliwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 18 Machi 2010. Tarehe 15 Januari 2015 akateuliwa kuwa Balozi nchini Haiti. Tarehe 7 Januari 2021 ameteuliwa kuwa Balozi Kuwait na Qatar.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Eugene Martin Nugent kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Kuwait na Qatar. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Eugene Martin Nugent alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Haiti. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Nugent alizaliwa tarehe 21 Oktoba 1958 huko Gortaderra Scariff, nchini Ireland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 9 Julai 1983 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 1 Julai 1992 alijiunga na utume wa diplomasia ya Kanisa.

Baada ya kufanya utume wake katika diplomasia ya Kanisa: Mjini Vatican, Uturuki, Mjini Yerusalemu, Ufilippini na Hong Kong, tarehe 13 Februari 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Madagascar, Mauritius na Shelisheli (Seychelles) na Mwakilishi wa Kitume kwenye Visiwa vya Comoro. Tarehe 18 Machi 2010, akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu na Kardinali Tarcisio Pietro Evasio Bertone, S.D.B., Katibu mkuu mstaafu wa Vatican. Tarehe 15 Januari 2015, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Haiti. Na tarehe 7 Januari 2021 ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Kuwait na Qatar.

Uteuzi Qatar

 

07 January 2021, 14:51