Tafuta

Atakuwa Kardinali Cantalamessa atakayeongoza tafakari ya Majilio katika Ukumbi wa Paulo VI kuanzia tarehe 4 Desemba Atakuwa Kardinali Cantalamessa atakayeongoza tafakari ya Majilio katika Ukumbi wa Paulo VI kuanzia tarehe 4 Desemba 

Tafakari ya Majilio ni katika ukumbi wa Paulo VI na kuongozwa na Kard.Cantalamessa

Mahubiri yaliyokabidhiwa Kardinali mpya na mhubiri wa Nyumba ya kipapa kwa ushiriki wa Papa,tafakari itaongozwa na mada“Utufundishe ufupi wa maisha yetu ili tuweze kuwa na hekima kutoka kifungu cha Zab 90,12.Katika suala la janga na ulazima wa kuwa na nafasi kubwa kati ya washiriki,nafasi iliyochaguliwa ni katika ukumbi wa Paulo VI.

Ni katika Ukumbi wa Paulo VI, kuanzia tarehe 4 Desema saa 3.00 asubuhi majira ya Ulaya kwa ushiriki wa Papa, wataanza tafakari kwa ajili ya Majilio. Ni taarifa kutoka Makao makuu ya nyumba ya kipapa. Atakaye ongoza tafakari hiyo atakuwa ni Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa, Kardinali mpya Raniero Cantalamessa O.F.M. Kap. ambaye amechagua mwaka huu  mada “Utufundishe ufupi wa maisha yetu ili tuweze kuwa na hekima",  kifungu kilichotolewa katika Zaburi  90,12.

Ni tangu tarehe 23 Juni 1980 wakati Mtakatifu Yohane Paulo akiwa Papa alimchagua kama mhubiri  ndugu huyo mdogo mkapuchini na ambaye hadi leo bado anaendelea na safari yake. Pongezi kwake katika mchakato wa kipindi kwa upande wa mapapa wengine watatatu kama vile alivyo weza kusema hivi karibu katika mahojiano kwamba yanampa mshangao mkubwa. Kardinali Cantalamessa alisema:“Kwa kufikia  hatua ya kwamba Papa kama Yohane Paulo II, Papa Benedikto na baadaye Papa Francisko, wanapata muda wa kukaa na kusikiliza maskini rahisi, ndugu mdogo mkapuchini, ni mfano wa ambao wanauonesha kwa Kanisa lote , mfano mzuri wa Neno la Mungu. Kwa maana nyinngine ni wao wanao nihubiri mimi”.

Kwa maana hiyo eneo lililochaguliwa kwa ajili ya tafakari tatu kwa mwezi wa Desemba katika  kipindi cha maandalizi ya siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ni katika ukumbi wa Paulo VI, mahali mbamo panajibu hali halisi ya kuwezesha nafasi kubwa kati ya mshiriki mmoja na mwingine kwa ajili ya  kuzuia maambukizi ya covid. Katika mahubiri hayo wanawaalika makardinali, maaskofu wakuu, maaskofu, viongozi wakuu wa mabaraza ya kipapa, wanafanyakazi wa Sekretarieti kuu, wakuu wa mashirika ya Kike na Kiume ambao wanatoa huduma katika Makanisa ya Kipapa. Kwa mujibu wa kufuata utaratibu wa kipindi cha majilio, kuanzia wiki ya kwanza kwa maana hiyo itakuwa tarehe 4,  11  na 18 Desemba,  saa 3.00 asubuhi majira ya Ulaya.

 

01 December 2020, 16:53